#COVID19 Mashabiki walimponza Mwl. Kashasha, aliambukizwa COVID-19

Hayo ndio maneno.
Mzee Kashasha alikuwa na ugonjwa wa figo bado ndugu wanashadidia amekufa kwa Covid 19 na ameipata wakati wa safari ya kutoka Dar Kig na kurudi. Hakika familia zingine zinatia huruma.
kuna watu wana akili nzito. huyu unamkuta mbishi huku hajui kitu
 
KIFO ni fumbo. Hutamsoma tena Mwalimu Alex Kashasha kwenye kolamu yake aliyokuwa akiandika kwenye ukurasa wa 12 wa Mwanaspoti kila Jumamosi. Kifo kimemchukua, atazikwa Dar es Salaam Jumatatu.

Hutasikia tena ile misemo, mbwembwe zake akitangaza mpira kwenye TBC au akifafanua jambo kwenye Mwananchi Digital.

Soma zaidi: TANZIA - Mwalimu Alex Kashasha, mchambuzi nguli wa Soka afariki dunia

Kaka wa Marehemu, Deus Alexander alisema alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Uviko-19 ambao aliupata akitoka kwenye mechi ya Simba na Yanga mjini Kigoma baada ya kupiga picha na kila aliyekuwa akimuomba kwenye vituo mbalimbali akiwa kwenye basi kurejea Dar.

Alisema watamzika Jumatatu ya Agosti 23 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mchana.

“Kwa kuwa mdogo wangu alikuwa mtu wa watu hatutaki kuwanyima mashabiki na wanasoka wenzake uhuru, hivyo tunatafuta eneo la wazi ambalo litakuwa rahisi kumuaga na tutawaambia mapema,kumuaga itakuwa Jumapili, kiukweli tuna maumivu kumpoteza mtu mwenye upendo sana kwenye familia,” alisema na kuongeza Kashasha alianza kuumwa tangu alipotoka kwenye fainali za Kombe la ASFC mjini Kigoma Julai 25.
 
KIFO ni fumbo. Hutamsoma tena Mwalimu Alex Kashasha kwenye kolamu yake aliyokuwa akiandika kwenye ukurasa wa 12 wa Mwanaspoti kila Jumamosi. Kifo kimemchukua, atazikwa Dar es Salaam Jumatatu.

Hutasikia tena ile misemo, mbwembwe zake akitangaza mpira kwenye TBC au akifafanua jambo kwenye Mwananchi Digital.

Soma zaidi: Mwalimu Kashasha afariki dunia

Kaka wa Marehemu, Deus Alexander alisema alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Uviko-19 ambao aliupata akitoka kwenye mechi ya Simba na Yanga mjini Kigoma baada ya kupiga picha na kila aliyekuwa akimuomba kwenye vituo mbalimbali akiwa kwenye basi kurejea Dar.

Alisema watamzika Jumatatu ya Agosti 23 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mchana.

“Kwa kuwa mdogo wangu alikuwa mtu wa watu hatutaki kuwanyima mashabiki na wanasoka wenzake uhuru, hivyo tunatafuta eneo la wazi ambalo litakuwa rahisi kumuaga na tutawaambia mapema, kumuaga itakuwa Jumapili, kiukweli tuna maumivu kumpoteza mtu mwenye upendo sana kwenye familia,” alisema na kuongeza Kashasha alianza kuumwa tangu alipotoka kwenye fainali za Kombe la ASFC mjini Kigoma Julai 25.
credit MWANANCHI
 
Back
Top Bottom