Siri mauaji ya bilionea wa madini na mwanaye

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,313
Siku moja baada ya kifo cha mfanyabiashara wa madini, Marwa Masese (45) na mwanaye, John Marwa (28), dada wa marehemu, Grace Marwa amesimulia mkasa huo akidai kuwa mdogo wake alisaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri fedha iingie benki.

Marehemu hao, wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kuuawa na marafiki zao mkoani Ruvuma walikokwenda kwa shughuli za kibiashara.

Akisimulia mkasa huo kando mwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO), Grace alidai kuwa kaka yake alikuwa ametoka kununua dhahabu Mbeya, kwenye gari alikuwa na mali nyingine nyingi na fedha taslimu.

Alidai kuwa baada ya kuuawa, watuhumiwa walitoroka.

Grace alisema wameitambua miili ya ndugu zao na wameona walivyoumizwa lakini wanasubiri uchunguzi wa daktari.

Alisema wakikabidhiwa miili hiyo wataamua kama watapata nafasi ya ndege waisafirishe kesho kwenda Dar es Salaam na wakikosa watasafirisha kwa magari.

Grace alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu marehemu ni mdogo wake anayemfuata, alikuwa msaada mkubwa kwake na juzi walikuwa waende India kwenye matibabu yeye na mwanaye na walishakata tiketi za ndege kwa ajili ya safari hiyo.

“Nimeumizwa sana na hili tukio, ni baya na linaumiza sana, sina cha kusema ila nawashukuru Jeshi la Polisi, wametusaidia na wameonyesha uaminifu mkubwa,” alisema Grace.

“Kabla ya kuuawa, aliniambia ameshasaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri pesa zake ziingie benki na tayari alishanunua hisa.

“Nimeumia kumpoteza mdogo wangu na mwanaye, najua wameuawa kikatili ila Mungu atawalipia,” alisema Grace.

Mwanamke huyo alisema kabla ya Marwa kukumbwa na mkasa huo, alikuwa akiwasiliana naye kila siku, lakini baadaye alipompigia simu, haikupatikana.

Alisema anawashukuru polisi kwa kuwapatia mkufu wa dhahabu wa marehemu wenye thamani ya Sh3 milioni waliouokota ndani ya gari lake.

(Imeandikwa na Joyce Joliga).

Mwananchi.
 
Kwahio alitoka kununua madini mbeya ya billion 2, akaenda kuuza Ruvuma, rafiki zake wakammaliza, au sijaelewa vizuri

Alisaini dili ya 2bil kwenye vitalu vyake vya madini, Mbeya walikwenda kwenye baishara nyingine ya madini.

Kwenye hiyo dili ya 2bil inaonekana kuna mtu alikuwa anataka kuingia yeye aipige hiyo hela..

Tuache kuaminiana sana na kupeana ramani au hata kuwa karibu na binadamu incase una dili bado haijamature.
 
Naweza kumuamini mtoto wangu wa kiume kwenye dili zangu tena niwe nimemtrain na kumuivisha na kujua ana uelekeo gani.

Ni hatari kiumbe binadamu kujua una hela kwenye gari yako au nyumbani kwako, ukiwa na hela kwenye gari au nyumbani kwako hakikisha unajua mwenyewe tu, kama una mchongo ulio kwenye pipeline acha kuhusisha watu.
 
alisaini dili ya 2bil kwenye vitalu vyake vya madini, mbeya walikwenda kwenye baishara nyingine ya madini.

kwenye hiyo dili ya 2bil inaonekana kuna mtu alikuwa anataka kuingia yeye aipige hiyo hela..

tuache kuaminiana sana na kupeana ramani au hata kuwa karibu na binadamu incase una dili bado haijamature.
Hao hao waliomuua ndiyo walikuwa wanafanikisha hilo dili la mkataba wa 2b.

Ova
 
Kwahio alitoka kununua madini mbeya ya billion 2, akaenda kuuza Ruvuma, rafiki zake wakammaliza, au sijaelewa vizuri
Nilisikia Redioni Kamanda Ruvuma anaongea. Walitoka Kunduchi Dar, Dreva, Baba na Mtoto Kwenda Ruvuma Songea wana kitalu cha Madini fulani kwahiyo walienda kuingia mkataba na muwekezaji, baada ya kupewa visenti vya awali na nyingine watasubiri.

Waliwasha ndinga kurudi Dar, walipofika Makambako, washikaji waliowatafutia hao wawekezaji wakishirikiana na Dreva wao wakawapa ramani ya kununua dhahabu Mbeya. Wakaenda Mbeya na Kufanya hivyo, then wakaanza safari ya kutoka Mbeya kuja Dar.

Walipofika Makambako Dreva wao akasema amechoka anaomba kupumzika, inavyoonekana Dreva alimuuza boss, Dreva akamuekea dawa za kulevya boss na Mtoto wakalala kwenye gari hapo Makambako. Then Dreva na kundi lake walianza safari kurudi tena Songea badala ya Dar, wakawaua kwa kuwagonga na kitu kizito kati ya Njombe na Songea.

Halafu wakatengeneza ajali kwa kuiacha gari kwenye korongo upande wa Songea. Dreva akaenda polisi huko Songea kwamba amepata ajali. Polisi wameenda kukagua ajari wameshangaa Dreva kapona boss na mtoto wamekufa, polisi wakajiongeza, wakakuta sindano ya dawa za kulevya kwenye gari iliotumika ili wasinzie, pia miili imepimwa na kuonekana walipondwa na kitu kingine sio ajali.

Pia walikuta faini za polisi kutoka Makambako Kwenda Njombe na ushahidi mwingine. Alipobanwa sana Dereva akataja kundi lingine ambalo lipo mbaroni kwa sasa. Dereva alimuuza boss kule Songea, ile zunguka zunguka ya Mbeya, Makambako ilikuwa kutafuta site ya kuulia.
 
Hao hao waliyomua ndiyo walikuwa wanafanikisha hilo dili la mkataba wa
2b

Ova

Jamaa tamaa ziliwaingia, japo marehemu alipaswa kuwa kwenye machale muda wote na sio kuwaamini all the time. Hela ni shetani hatari anayeweza kubadili akili ya mtu kila sekunde.

Iliwahi nikuta hii issue ugenini, tumesafiri na jamaa yangu kwenda kufanya biashara fulani na plan ilikuwa iwe tukifika tunamaliza na kila mtu anakufa na chake tunasambaa, tukakuta wenyeji wametupangia hoteli na kutuambia dili ni next day huku wakijua tumesafiri na hela.

Tuliingia hotel vyumbani tukaoga, then tukaset ramani yetu, around saa moja usiku nikaenda kwenye breaker nikazima umeme hotel nzima, mimi na mwanangu tukasepa na hela zetu huku funguo za vyumba tukiziacha ndani, jamaa wakawasha generator bado umeme hakuna, wakagundua breaker imetrip.

Usiku saa sita kuelekea saa saba ile hoteli ikavamiwa na target ni room zetu jamaa wakakuta kweupe. Jamaa walivyokuwa mafala usiku saa nane wanatutafuta kwenye simu, tukapiga nyundo simu zetu, next day tukachukua uelekeo mwingine kuwapoteza maboya.
 
Jamaa tamaa ziliwaingia, japo marehemu alipaswa kuwa kwenye machale muda wote na sio kuwaamini all the time.
Hela ni shetani hatari anayeweza kubadili akili ya mtu kila sekunde.

Iliiwahi nikuta hii issue ugenini, tumesafiri na jamaa yangu kwenda kufanya biashara fulani na plan ilikuwa iwe tukifika tunamaliza na kila mtu anakufa na chake tunasambaa, tukakuta wenyeji wametupangia hoteli na kutuambia dili ni next day huku wakijua tumesafiri na hela.

tuliingia hotel vyumbani tukaoga, then tukaset ramani yetu, around saa moja usiku nikaenda kwenye breaker nikazima umeme hotel nzima, mimi na mwanangu tukasepa na hela zetu huku funguo za vyumba tukuziacha ndani, jamaa wakawasha generator bado umeme hakuna, wakagundua breaker imetrip, usiku saa sita kuelekea saa saba ili hotel ikavamiwa na target ni room zetu jamaa wakakuta kweupe. Jamaa walivyokuwa mafala usiku saa nane wanatutafuta kwenye simu, tukapiga nyundo simu zetu, next day tukachukua uelekeo mwingine kuwapoteza maboya.
Akili kubwa sana congrats mkuu 👍
 
Siku moja baada ya kifo cha mfanyabiashara wa madini, Marwa Masese (45) na mwanaye, John Marwa (28), dada wa marehemu, Grace Marwa amesimulia mkasa huo akidai kuwa mdogo wake alisaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri fedha iingie benki.

Marehemu hao, wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kuuawa na marafiki zao mkoani Ruvuma walikokwenda kwa shughuli za kibiashara.

Akisimulia mkasa huo kando mwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO), Grace alidai kuwa kaka yake alikuwa ametoka kununua dhahabu Mbeya, kwenye gari alikuwa na mali nyingine nyingi na fedha taslimu.

Alidai kuwa baada ya kuuawa, watuhumiwa walitoroka.

Grace alisema wameitambua miili ya ndugu zao na wameona walivyoumizwa lakini wanasubiri uchunguzi wa daktari.

Alisema wakikabidhiwa miili hiyo wataamua kama watapata nafasi ya ndege waisafirishe kesho kwenda Dar es Salaam na wakikosa watasafirisha kwa magari.

Grace alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwa familia kwa sababu marehemu ni mdogo wake anayemfuata, alikuwa msaada mkubwa kwake na juzi walikuwa waende India kwenye matibabu yeye na mwanaye na walishakata tiketi za ndege kwa ajili ya safari hiyo.

“Nimeumizwa sana na hili tukio, ni baya na linaumiza sana, sina cha kusema ila nawashukuru Jeshi la Polisi, wametusaidia na wameonyesha uaminifu mkubwa,” alisema Grace.

“Kabla ya kuuawa, aliniambia ameshasaini mkataba wa Sh 2 bilioni na alikuwa anasubiri pesa zake ziingie benki na tayari alishanunua hisa.

“Nimeumia kumpoteza mdogo wangu na mwanaye, najua wameuawa kikatili ila Mungu atawalipia,” alisema Grace.

Mwanamke huyo alisema kabla ya Marwa kukumbwa na mkasa huo, alikuwa akiwasiliana naye kila siku, lakini baadaye alipompigia simu, haikupatikana.

Alisema anawashukuru polisi kwa kuwapatia mkufu wa dhahabu wa marehemu wenye thamani ya Sh3 milioni waliouokota ndani ya gari lake.

(Imeandikwa na Joyce Joliga).

Mwananchi.
RIP hao watafutaji kina Marwa.
Kweli dunia hadaa!
 
Back
Top Bottom