Mashabiki wa Japan baada ya mpira kuisha wakusanya taka uwanjani na kuondoka

Hii tabia ni ya kipekee kabisa, heshima ni kitu cha bure. Mpira ulivyoisha tu, wakakusanya taka zilizopo maeneo walipo wao, zote, na kuzitupa kwenye mifuko ya rambo na kutupa mahali pa taka na kuondoka.

Uhusiano wa Qatar na Japan kwa kitendo hiki aisee, itajenga urafiki mkubwa sana kidiplomasia.

Nimejifunza mengi sana kwa maisha ya Japan na nje ya Japan.
Hiyo ni kawaida Yao hata michuano iliyopita walifanya pia Ni ustaarabu uliotukuka.

Ingekuwa mashabiki wa Cuba chini YA mfalme Zamaridi ungeona wanan'goa Viti Na kujisaidia Choo kikubwa kwenye sink la kunawia mikono.
 
Wenzetu wanaishi kwa miiko, ukijaribu kwenda kinyume na hiyo miiko adhabu yake ni kifo.
Miiko ndiyo mpango mzima hata ngedere wanatambua uwepo wa miiko, wakilala juu ya mti usiku kamwe hawadiriki kuangusha kinyesi ardhini, ni mwiko kabisa, mmoja akidiriki basi anashughulikiwa vilivyo, sisi tunazidiwa utii hata na wanyama.
 
Japan ni Moja ya jamii yenye kiwango kikubwa Cha utu na ustaarabu.

Kwao kitu kinachowaunganisha watu ni ubinaadamu tofauti na baadhi ya mijitu itumiayo vitabu vya dini kubagua wengine ambao hawajakubali mafundisho ya vitabu vyao ambao kwao huona binaadamu au mwenzao ni yule anayefuata mafundisho Yao.

Hii inakubaliana na Moja ya nukuu ya mwanafilosofia JEREMI BENTHAM aliyewahi kusema" Watu hawatendi mema au mabaya kwa sababu ya uwepo ama hofu ya Mungu, watu hawafanikiwi au kutokufanikiwa kwa sababu ya kusali Sana au kutokusali. Kama Mungu asingeluwepo au akawa yupo lakini Hana muda wa kumfuatilia binaadamu bado wengekuwepo watenda mema na watenda mabaya, wangekuwepo matajiri na maskinj nk.

Ukiangalia hili kombe Kuna mijitu imetumia nguvu kubwa na kulifanyabkama ni uenezi wa Imani Yao lakini hawafanyi matendo yoyote tofauti kama hawa kuwatofautisha na jamii nyingine zaidi ya kusema dini yetu ni nzuri Sana njoo huku, kifungu ama sura Fulani inasema hivi Fanya hivi lakini kwao hakuna lolote unapomfanyia tathmini ya Maisha ya kawaida tofauti na ayasemayo kwa mdomo na anavyovaa
 
Wajapan baada ya mechi
Screenshot_20221124-002635.png
Screenshot_20221124-002629.png
 
Hii tabia ni ya kipekee kabisa, heshima ni kitu cha bure. Mpira ulivyoisha tu, wakakusanya taka zilizopo maeneo walipo wao, zote, na kuzitupa kwenye mifuko ya rambo na kutupa mahali pa taka na kuondoka.

Uhusiano wa Qatar na Japan kwa kitendo hiki aisee, itajenga urafiki mkubwa sana kidiplomasia.

Nimejifunza mengi sana kwa maisha ya Japan na nje ya Japan.
Wangefanya wabongo mngesema walikuja na uchawi wao sasa wanaukusanya ki aina,ila kwakuwa ni wa Japana mnasema wanafanya usafi...
 
Hapa nilipo ninagombana na watu wazima tena graduate wanakunywa maji,juice na kutupa hovyo chupa badala ya kuziweka kwenye chombo cha taka.

Ni tabia yetu hasa watanzania wengi hatuna ustaarabu hata kidogo.
Sijui nani ataweza kutusaidia hizi akili zibadilike
 
Uyaambie mashabiki ya makolo yafanye usafi Taifa baada ya mechi thubutuu!!!
Hapo Yanga tuwe tumeyatupia tatu mtungi.....
Huwa tanachanganyikiwa yale
 
Sio uwanjani tu kombe la dunia lililopita wachezaji wao walikuwa wanafanya usafi ktk vyumba vya kubadilishia nguo kabla hawajaondoka... Such a purest gesture!...
 
Sio mara ya kwanza wanafanyaga ivyo ni kawaida kila kombe la dunia..Japan ndo inaongoza kwa watu wastaarabu hawapendi vurugu na wasafi sana yaani wanajiremba mpaka wanaume hao na Korea ni jadi zao...Nilishawahi sikia nchi izo unaweza kukosa kazi katika baadhi ya sehemu kama sio smart na una muonekano mbaya.
Na hawapendi vitambi kule Tokyo ukiwana kitambini aibu

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom