Mashabiki wa Japan baada ya mpira kuisha wakusanya taka uwanjani na kuondoka

Kama huwa wanafanya hivyo mara nyingi na sisi hatujajifunza kutoka kwao, basi tuna matatizo sisi
Kuna mechi walifungwa ila walifanya kama ivyo kusafisha uwanja kombe lilopita na walitoka ila ni wastaarabu.

Sisi bado kwa kweli hata maofisini kwetu kabisa kukuta kikombe cha chai kichafu kipo juu ya meza siku nzima fresh tu.

Matatizo sana wabongo ukienda nchi za watu utashangaa sana hapo Qatar tu ni kusafi mpaka mtu unaona aibu hata kuangusha Ganda la pipi ila bongo ni uchafu tu ..Tunapata magonjwa ya ovyo daily.
 
Ni kawaida ya hao jamaa wana miiko sana.
Kuna clip moja inaonesha jinsi watoto wa kijapan wanavobehave sawa kulingana na tamaduni zao.
Nafahamu kuwa wana tabia nzuri

Jaribu ku imagine kama wangepigwa goli 7-0 huo usafi wangefanya?
 
Hii tabia ni ya kipekee kabisa, heshima ni kitu cha bure. Mpira ulivyoisha tu, wakakusanya taka zilizopo maeneo walipo wao, zote, na kuzitupa kwenye mifuko ya rambo na kutupa mahali pa taka na kuondoka...
Unajua watu tuna kasumba moja ya ajabu sana, tunapenda mno ukubwa kwa kudhani kuwa usipojimwambafy utadharaulika wakati siyo, kasumba mbaya sana hii.

Niliwahi kwenda Ulaya kipindi fulani halafu nikawa naishi kwenye hostel moja na watoto wa kizungu miaka 20-25, wa kike na wa kiume. Shida ilikuwa ni kwenye kudeki hostel yetu pamoja na kuosha vyombo baada ya kuwa tumekula chakula.

Baada ya mimi kuona tunaanza kusihi mazingira kama hatuko Ulaya tena, nikaamua kuwa nadeki floor mwenyewe na kusafisha vyombo vyote wakishamliza kula. Baada ya kuwa nimefanya hivyo mara mbili-tatu biia kuwambia kitu, wao wenyewe walijiongeza; kuanzia pale hostel ikawa iko safi muno, na vyombo vya chakula nikawa sivioni tena vikiwa vimetelekezwa kwenye masink ya kuoshea vyombo.

Mimi wakati huo nilikuwa 30+ na nilikuwa nimejipachika uongozi kwenye misafara tuanpokuwa tunasfari kwenda sehemu. Nilikuwa natangulia mbele halafu msururu wa watoto wa kizungu uko nyuma yangu tunakimbia kwenda kupanda treni za kwenda Malmo na Lund, Sweden.

Haipo burudani kubwa hapa duniani kuzidi ile ya mtu mzima kuwa na urafiki na watoto
 
Bro kombe la dunia 2018 walifanya usafi Hadi siku waliyofungwa na kutolewa kwenye mashindano, had kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji walifanya usafi na kuacha ujumbe wa kushukuru
Fatilia kwenye mitandao utaona hao jamaa wana nidham sana
hawa waliofanya usafi changing room na kuacha ujumbe walikuwa South Korea ila ni jamii moja
 
Back
Top Bottom