Mashabiki wa Japan baada ya mpira kuisha wakusanya taka uwanjani na kuondoka

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,098
2,459
Hii tabia ni ya kipekee kabisa, heshima ni kitu cha bure. Mpira ulivyoisha tu, wakakusanya taka zilizopo maeneo walipo wao, zote, na kuzitupa kwenye mifuko ya rambo na kutupa mahali pa taka na kuondoka.

Uhusiano wa Qatar na Japan kwa kitendo hiki aisee, itajenga urafiki mkubwa sana kidiplomasia.

Nimejifunza mengi sana kwa maisha ya Japan na nje ya Japan.
 
Sio mara ya kwanza wanafanyaga ivyo ni kawaida kila kombe la dunia..Japan ndo inaongoza kwa watu wastaarabu hawapendi vurugu na wasafi sana yaani wanajiremba mpaka wanaume hao na Korea ni jadi zao...Nilishawahi sikia nchi izo unaweza kukosa kazi katika baadhi ya sehemu kama sio smart na una muonekano mbaya.
 
Hao jamaa ndio wanaongoza kwa ustaarabu na tabia nzuri duniani.

Na hapo hawamjui Yesu wala Allah wa Mtume muhammad.

Ila kina sisi wakristo na waislamu ibada nyingii ila tabia mbovuu
Umenena vyema wengi wetu haswa wale tulioletewa hizi dini tuna ubaguzi wa kijinga kiasi hata hatuna akili, tena wakati mwingine unakuta hata Wapagani wanatuzidi upendo
 
Walikusanya taka kwenye ile mechi ya kwanza ya Qatar na Ecuador video ikasambaa,ila nafikiria wangekua waAfrica wameokota wangetrend hivi? Au wangeonekana ni kazi yao,,,,Just saying!

Japan hata world cup zilizopita. Mashabiki walikuwa wanafanya usafi.. ni utamaduni wao.

Kikwao japan ni utamaduni kufanya usafi kabla hujaondoka sehemu iliyo chafu
 
Sio mara ya kwanza wanafanyaga ivyo ni kawaida kila kombe la dunia..Japan ndo inaongoza kwa watu wastaarabu hawapendi vurugu na wasafi sana yaani wanajiremba mpaka wanaume hao na Korea ni jadi zao...Nilishawahi sikia nchi izo unaweza kukosa kazi katika baadhi ya sehemu kama sio smart na una muonekano mbaya.
Kama huwa wanafanya hivyo mara nyingi na sisi hatujajifunza kutoka kwao, basi tuna matatizo sisi
 
Hii tabia ni ya kipekee kabisa, heshima ni kitu cha bure. Mpira ulivyoisha tu, wakakusanya taka zilizopo maeneo walipo wao, zote, na kuzitupa kwenye mifuko ya rambo na kutupa mahali pa taka na kuondoka.

Uhusiano wa Qatar na Japan kwa kitendo hiki aisee, itajenga urafiki mkubwa sana kidiplomasia.

Nimejifunza mengi sana kwa maisha ya Japan na nje ya Japan.
Hawa si ni wale wanao amka rasmi saa 11 alfajiri? 🤔
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom