Mariam Ditopile: Tegeni sikio Jumapili Rais Samia ana jambo zito sana

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
TEGENI SIKIO JUMAPILI RAIS SAMIA ANA JAMBO ZITO SANA-MBUNGE DITOPILE

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile leo amejumuika na wanaCCM wenzake katika Kata ya Bulungwa kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga, Emmanuel Cherehani huku akiwataka watanzania kutega sikio siku ya Jumapili kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Ditopile amesema Cherehani ambaye alipitishwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa mgombea Ubunge wa Ushetu anatosha na ana sifa zote za kuwa muakilishi wao bungeni.

"Jumapili Mama Samia ana jambo Kubwa na Zito kweli kweli nawaomba wana Ushetu na watanzania kwa ujumla Nchi nzima Mtege Sikio, Mama huyu yupo kazini anahangaika na shida za watanzania, tukae kwenye redio, na TV tumskilize, na tukitoka tukawasimulie wengine.

Tunaye Rais mahiri na shupavu na nyie mmeona anafaa mmempa Uchifu leo kwenye historia ya nchi yetu pamoja na kwamba tuna Rais wa kwanza mwanamke tuna Chifu Mwanamke Chifu Hangaya Samia Nyota inayong’aa "
Mbunge Mariam Ditopile, Ufungaji Kampeni Jimbo la Ushetu,

Nawaomba wana Ushetu watuletee Cherehani kule bungeni nimelelewa na wasukuma najua ukarimu wenu, nitashirikiana naye kule Bungeni hatokuwa mgeni atawapambania kuwaletea maendeleo"

Amesema Ditopile Akimuombea Kura Mgombea Ubunge Kwa Tiketi Ya Ccm Jimbo la Ushetu Leo.

Jimbo la Ushetu limeingia kwenye Uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo na aliyekua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kuandikwa.

IMG-20211008-WA0112.jpg
IMG-20211008-WA0132.jpg
IMG-20211008-WA0115.jpg
 
Yaani nawewe ni kihoja.

Umeamua kukopi kila kitu kutoka kwa mleta thread.
 
Kazi kujipendekeza nyie. Rais mwanamke kwa wengi sio hoja kama hakuvaa viatu vya magufuli kama alivyodai eti ni kitu kimoja na huyo mwamba. Ameanza na kuwafurahisha chadema na wapinga maendeleo kwa kumtosa kijana sabaya. Sasa anawarudisha uwaziri waliyomkejeli jpm kwa sera yake kupiga vita ufisadi na mafisafi bila huruma.
 
Back
Top Bottom