Maria Sarungi na chuki dhidi ya Rais Samia na wazanzibar

Maria Sarungi na chuki dhidi ya Rais Samia na wazanzibar

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
Inasikitisha kuona mtu kama Maria Sarungi anayejiita mwanaharakati wa haki za binadamu, akiendelea kuonyesha chuki waziwazi dhidi ya Rais Samia na Wazanzibari kwa ujumla. Kila jambo linalotokea nchini kwake linageuzwa lawama kwa Rais Samia, hata yale yasiyomhusu moja kwa moja.

Mbaya zaidi, anajaribu kupandikiza dhana ya kuwa Wazanzibari wanatawala au kunyanyasa wengine, kitu ambacho ni hatari kwa mshikamano wa kitaifa. Huu ni ukabila wa kisasa unaokuja kwa sura ya harakati.
Kipindi cha awamu ya Tano alitumia kila njia kuhakikisha anapata nafasi ya msemaji mkuu wa serikali na hata ikafikia hatua akatoa kitumbua watu wakakila lakini bado hakufanikia adhima yake na ndio maana akageuka kuwa mwiba na kuanza siasa zake za chuki

Cha kushangaza, Mtu huyu huyu na familia yake imenufaika na serikali ya awamu za nyuma, lakini leo baada tena ya kukosa nafasi katika awamu hii ya sita anayarudia yake yale aliyomfanyia magufuli,anatengeneza ajenda ya mgawanyiko kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa na kukosa Uteuzi Kama kweli ana uchungu na nchi hii, ni vyema afanye harakati zenye kujenga, si kugawa watu.

Uchaguzi unakuja 2025. Watanzania hawahitaji chuki wala uchochezi, tunahitaji hoja, sera, na umoja.
 

Attachments

  • IMG_0795.jpeg
    IMG_0795.jpeg
    146.1 KB · Views: 39
Yaani unamsema Maria ana chuki na wazanzibar kwa kutumia hisia zako tu, halafu hapo hapo unamtolea maneno ya kashifa ambayo nna uhakika we mwenyewe huwezi kuyadhibitisha eti aliliwa kitumbua? Una uhakika na hizi tuhuma?

Pamoja na hivyo kama ambavyo wazanzibar wanaona ni haki yao kutuchukia watu wa bara na huwezi kuwakemea, basi acha hata sisi watu wa bara tuwachukie kabisa bila kificho.
 
Maria Sarungi kazaliwa familia ya mboga saba, hana dhiki kama zako mleta mada, ya kumfanya yeye kugawa kitumbua kwa ajili ya kupata cheo
 
Back
Top Bottom