Marekani yafungua ubalozi wake Cuba baada ya miaka minne

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Ubalozi wa Marekani Nchini Cuba umeanza kutoa visa wiki hii kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka minne tangu madai ya mashambulizi ya mfumo wa sauti (Sonic Attacks) dhidi ya wafanyakazi wa kidiplomasia.

Marekani ilifunga huduma za kibalozi Cuba mwaka 2017 baada ya wafanyakazi wa Marekani na familia zao kuugua magonjwa ya ajabu yaliyojulikana kama Havana Syndrome.

Kufungwa huko kulikuwa pigo kubwa kwa raia wa Cuba wengi wanaotarajia kusafiri kwenda Marekani.

Marekani ilitangaza miezi miwili iliyopita itaanza kufungua tena kidogo na taratibu, kwa ubalozi wake na huduma za kibalozi.

Ubalozi huo ulifungwa Septemba, 2017 baada ya Rais wa wakati huo, Donald Trump kuelezea madai ya shambulizi hilo la Sonic.


Source: Aljazeera

Ubalozi Marekani.jpg
 
Back
Top Bottom