Marekani wahangaika kumtafuta aleivujisha taarifa za siri za kijeshi kuhusu vita ya Ukraine

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Serikali ya Marekani pamoja na wizara ya Ulinzi na makao makuu ya kijeshi Pentagon bado wapo na kitendawili cha kutegua mtu alievujisha taarifa za siri za kijeshi kuhusu vita ya Ukraine.

Hadi sasa imefahamika kuwa taaarifa hizo zilitokea katika mchezo wa computer yaani "online game" na zilikuwa katika vipande vipande yaani "slides", zikielezea mipango yote ya majeshi ya Ukraine dhidi ya Russia kuanzia mwishoni mwa mwezi March mwaka huu.

Lakini uthibitisho kuwa taaarifa hizo ni za kweli bado haujawa wazi ingawa zaonesha udhaifu mkubwa wa majeshi ya Ukraine na matumizi ya hovyo ya silaha jambo linopelekea kumaliza akiba ya silaha walokuwa wakipewa na nchi za NATO.

Pia taarifa hizo zaonyesha idadi kubwa ya majeshi maalum yaani "special forces" kutoka nchi za NATO vikiwemo vikosi vya UK ambao Russia yawachukulia kuwa ndo wachagizaji wakuu wa vita hiyo.

Uvujaji wa taarifa hizo umewastua maofisa wengi wa serikali ya Marekani akiwemo mkuu wa Pentagona ambae nae amesema hafahamu imekuwaje na kudai kuwa taarifa hizo zilikuwa mahala fulani mtandaoni na "hata hata yule aliekuwa amezipata kwa wakati huo hajulikani", amedai waziri wa Ulinzi Llyod Austin.

Shirika la habari la AP limedai kuwa taarifa hizo za siri huenda zilianikwa katika ukumbi wa mazungumzo au "Chart Room" utumiwao na wachezaji michezo ya computer ujulikano kama Discord na haijulikani idadi halisi ya taarifa hizo na yasadikiwa kuwa ni mamia kwa mamia.

Taarifa hizo pia zaelezea jinsi udhaifu wa majeshi ya Ukraine ulivyo, idadi na aina za silaha ambazo Ukraine imekuwa ikipata na pia kuonyesha kila nchi ambayo inasaidia nchi hiyo na misaada ya aina gani. Nchi nyingi ambazo zimekuwa zikiisaidia Ukraine kwa siri zote zimetajwa katika taarifa hiyo na serikali za nzhi hizo hazijakataa wala kukanusha taarifa hizo.

Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Pentagon amekiri kwua taarifa hizo zahatarisha usalama wa Marekani na washirika wake.

Jambo kubwa ambalo taarifa hizo zimeonyesha ni idadi ya majeshi ya nchi za NATO nchini Ukraine ambapo lapingana na kauli ya NATO ziku zote kwamba haina majeshi nchini Ukraine. Idadi ya majeshi ya NATO nchini humo imewekwa wazi na taarifa hizi kuwa ni 97 ya kutoka nchi za UK (50), US(14) France (15), Latvia (17) na Uholanzi (1).

Taarifa hizi hazikusema eneo halisi yalipo majeshi hayo na yajishughulisha na nini na wizara ya Ulinzi ya Uingereza imekanusha taarifa hizo na kusema zisichukuliwe kuwa ni za kweli.

Taarifa hizo pia zimedai kuwa Marekani imekuwa ikizichunguza nchi za Misri na UAE kwamba zimekuwa zikijishughulisha na kupeleka silaha nchini Russia kwa njia za magendo. Misri ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani na ambayo hupewa msaada mkubwa wa fedha za kijiendesha, imekuwa ikipeleka makombora yapatayo 40,000 Russia. Raisi Al Sisi amedaiwa kwenye taarifa hizo kuhimiza uzalishaji wa silaha hizo na kusisitza kuweka jambo hilo liwe siri.

UAE nayo imedaiwa katika taarifa hizo kushirikiana na idara ya ujasusi wa kijeshi ya Russia GRU na kuziweka pembeni idara za kijausi za Uingereza na Marekani jambo ambalo UAE imekanusha na kusema hazina ukweli wowote.

Je, ni hatua gani serikali ya Marekani imechukua?

Kwanza serikali ya Marekani kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama wameamua kuzipitia kanuni za ndani zihusuzo usalama wa taifa na kuangalia ni kiasi gani taarifa hizo zimeathiri hali ya usalama.

Pili, kupunguza idadi ya watu ambao wana ruhusa ya kuzipata na kusoma hadidu za rejea za mikutani mifupi yaani "daily briefing" pamoja na kuangalia wapi taarifa hizo zaelekea mitandaoni jambo ambalo laweza kuwa limechelewa.

Na mwisho ni wizara ya sheria chini ya mwanasheria mkuu wa serikali kuanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini mhusika wa uvujishaji wa taarifa hizo za siri zilipatikana vipi na pia ni kwa namna gani ziliweza kusambazwa.

Vyanzo: AP, Guardian
 
Hiyo ni mbinu na hata Russia wamesema wana mashaka na hizo taarifa.
... Russia inatilia shaka taarifa hizo ila Kwa Mpalange wako kwenye sherehe siku ya tatu kushangilia uvujaji wa taarifa hizo muhimu! Ha ha ha!
 
Urusi keshawambia hizo ni propaganda za kizamani sana.. wamevujisha wenyewe halafu wanajijambisha wenyewe....
 
Back
Top Bottom