Urusi haina habari ya ISIS, yaipiga Ukraine kwa nguvu kulipiza kisasi

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
Kufuatia shambulia kubwa kwenye ukumbi wa starehe jijini Moscow ambapo kundi la ISIS lilijitaja kupitia vyombo vya magharibi kuwa ndilo lililohusika.Urusi imeonekana kutoshawishika na uozo wa taarifa hizo.

Watu kadhaa walikamatwa mara tu baada ya shambulio hilo kutokea ambapo watu zaidi ya 130 wamefariki dunia.

Tangu taarifa hizo za tukio na tuhuma za washukiwa kutoka nchi marafiki wa Ukraine kwa upande wake Urusi haijaonekana kutaja chochote kuhusu kikundi chochote cha kiislamu. Badala yake jeshi la Urusi limeshambulia kwa nguvu kubwa maeneo mbali mbali ya Ukraine yote. Shambulio ambalo ni kubwa kufanyika kwa siku za karibuni.

Kwa upande mwengine Urusi imeitaka Marekani isaidie kupatikana kwa wahusika kufuatia kauli yake kwamba Ukraine sio waliotekeleza shambulia hilo.
 
Lete link acha kubuni habar....
 
Marekani isaidie kutafuta nini?

Russia siyo Afrika NATo wanataka kuitreat Russia kama Afrika
Hayo ni majaribio mbalimbali ya kuidhoofisha Russia lakini hapa mbinu imefeli kwa kiwango kikubwa kabisa
Maneno ya Marekani kuwa ukraine hausiki
Inatafsirika kwamba anayehusika wanamjua
Ndiyo maana ya kusema wasaidie kumtafuta muhusika

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Lakin waliwapa taarifa mapema Russia wakapuuza
 
Ndio maana wameambiwa wasaidie kutafuta wahusika kama wamadhani ukraine haihusiki
Mrusi bhana! Yani Mrusi usaidiwe habari bure bila kuomba (alimtonya japo sio rafiki yake)ili achukue Tahadhari. Sasa hiyo imekuwa nongwa eti tena sasa baada ya shambulio anamtaka Mmareekani amsaidie kuwakamata wahusika. Mrusi ni pasua kichwa. Hakuona umuhimu wa kuifanyia kazi ile taarifa ila sasa anaona amshinikize huyo huyo Mmarekani kutoa msaada wa kutafuta watuhumiwa. Anakimbilia haraka kutoa adhabu kwa Ukraine ambayo haikuhusika na shambulio.
 
Naongea tu. Niambie zinatokaje
Kaa kimya basi. Huyo aliyewafikishia na aliyepokea washamalizana. Coz washapewa taarifa nzima zilivyo ila baada ya kutokuchukua hatua ndio watu wanatafutaga wakumpa lawama mbele ya umma. Kumbuka black war ni kubwa kuliko live war. Na ili Russia apate uhalali wa kushambulia maslah ya west anatakiwa aje na ushahid usio na mashaka kuwa ndio waliohusika. Na sasa hiv utamuona Russia wakizifanyia kaz zile taarifa rasmi. Inawezekana Isis ni branch ya marekan kawautumia waislam bila wao kujua Lakin hiyo haimpi Russia uhalali wa kuwashawishi watu kuwa wametumwa na West. Dunia haiendeshwi kienyeji hivyo. Hapo Congo kila mtu anajua vita vile Ni vya Kagame Lakin leta ushahid mezan huna so unabaki kuwachanganya watu wengine watamuunga mkono wengine watampinga.
 
Ukitumia ubongo wako vizuri utagundua kwamba mrusi sio kwamba anaomba msaada. Anawaambia wanao ona kupondwa kwa mukraine kufuatia shumbulio la kigaidi ni uonevu. Kama wanaona ukraine hahusiki basi wawakamate watu wengine wanao ona wanahusika. Inahitaji akili iliyopevuka kuelewa hilo
 
Ukraine kapigwa tofauti na anavyopigwa kwa miaka mi3 nyuma au ni yale yale?
 
Kaa kimya basi. Huyo aliyewafikishia na aliyepokea washamalizana. Coz washapewa taarifa nzima zilivyo ila baada ya kutokuchukua hatua ndio watu wanatafutaga wakumpa lawama mbele ya umma. Kumbuka black war ni kubwa kuliko live war. Na ili Russia apate uhalali wa kushambulia maslah ya west anatakiwa aje na ushahid usio na mashaka kuwa ndio waliohusika. Na sasa hiv utamuona Russia wakizifanyia kaz zile taarifa rasmi. Inawezekana Isis ni branch ya marekan kawautumia waislam bila wao kujua Lakin hiyo haimpi Russia uhalali wa kuwashawishi watu kuwa wametumwa na West. Dunia haiendeshwi kienyeji hivyo. Hapo Congo kila mtu anajua vita vile Ni vya Kagame Lakin leta ushahid mezan huna so unabaki kuwachanganya watu wengine watamuunga mkono wengine watampinga.
Ukiwa hapo yombo unaamini kabisa mrusi hakuzifanyia kazi? Unaamini mrusi hakuwa na taarifa zake binafsi? Taarifa za shambulio hata ukiwa nazo wewe na ndie raisi wa nchi ila taarifa hizo hazijataja eneo husika hata uwe na shirika la usalama wa taifa imara kiasi gani utashambuliwa tu. As long as taarifa ulizo nazo hazitaji eneo husiika. Tuneona imetoka israel na sasa urusi na marekani pia ilitokea na hata hapo Dar ilitokea.
NB: KUNYAMAZA SIWEZI!!
 
Russia ni dude la kutisha
Hizo nchi za Magharibi wanajaribi kuwahadaa kwa kutumia ISIS lakini hawajui intelenjesia ya Russia iko juu

Hapo wameyakanyaga

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hizo nchi za Magharibi ndizo ziliombwa zimtaje Mhusika au ni mhusika mwenyewe (ISIS) alitamka kwamba yeye ndiye amehusika? Mbona ISIS na Marekani hawaendani ni vitu tofauti?
 
Back
Top Bottom