Vita ya Ukraine ni alama nyingine ya kushindwa kwa Marekani na NATO

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111470429452.jpg

Moja ya maeneo tata ya siasa za kimataifa ni kuwa nchi kubwa na zenye uwezo zaidi wa kijeshi zimeshindwa vita katika nchi ndogo katika miaka 50 iliyopita, kuanzia vita ya Vietnam mpaka ya hivi sasa ya Ukraine.

Hapa “kushindwa,” maana ni kushindwa kijeshi, kulazimishwa kuondoka (kama ilivyotokea Iraq,) kushindwa kuungwa mkono na watu wa sehemu husika, na kukabiliwa na mkanganyiko linapokuja suala la kutimiza hatua zinazodaiwa kuwa nzuri, kama vile kutambulisha haki za binadamu, demokraisa, uhusu ama uhuru kwa wanawake.

Pia, kutokana na gharama kubwa ya binadamu, hususan katika Mashariki ya Kati, madai ya Marekani ya “vita dhidi ya ugaidi” tangu Septemba 11, 2001 pia yamekuwa majanga makubwa ya kiakili na kimaadili.

Marekani, ambayo ni nchi inayotumia fedha nyingi zaidi katika mambo ya kijeshi, mvamizi, mpiganaji, na mjenzi wa sera za kigeni za kijeshi duniani, iko katika tabaka la kipekee, na hii pia inahusisha kushindwa katika vita.

Marekani na washirika wake wanashusha kwa kasi uhalali, mahusiano na uaminifu katika macho ya nchi nyingine duniani mbali na washirika hao.

Kwanza, matukio haya ya kivita yamekuwa kinyume na busara na yamejaa majivuno ya nguvu, ubaguzi wa rangi na kiburi. Pili, baada ya kushindwa – kama ilivyotarajiwa, kama vile nchini Iraq, unakuja muda ambao propaganda, operesheni za kisaikolojia, ushawishi wa vyombo vya habari na mawazo ya kujilinda kisiasa haviwezi kufanya kazi tena. Pia, muda unakuja, ambapo hata nchi mtumiaji mkubwa wa fedha katika mambo ya kijeshi na yenye uchumi mkubwa inashindwa kufadhili uraibu wake wa silaha, na hifadhi yake ya silaha inamalizika.

Kuhusu Ukraine, Jumuiya ya NATO iliweka kambi yake nchini humo mara baada ya kupata uhuru wake, na mwaka 2008, NATO ilitangaza kuwa, Ukraine itakuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo. Huo ulikuwa ukiukaji mkubwa wa ahadi zilizotolewa kwa aliyekuwa rais wa Russia, Michael Gorbachev, lakini hiyo ilikuwa ni kawaida ya hisia za kwamba, ‘tunaweza kufanya chochote tunachotaka.’

Kwa akili zake, NATO ilikataa kusikiliza wasiwasi wa haki wa Russia na pia haikujishughulisha kuhusu ukweli kuwa, kulikuwa na kundi dogo kati ya watu wa Ukraine wanaokubali nchi hiyo kujiunga na NATO. Badala yake, mabadiliko ya uongozi nchini Ukraine ndiyo pekee yalikuwa yanahitajika, na kuweka uongozi unaounga mkono nchi za Magharibi, kuulipa vizuri na kuupa chaguo ambalo hauwezi kulikataa kwa kuwavuta hatua kwa hatua kujiunga na Jumuiya hiyo inayoendelea kupanuka.

Russia ilipinga kihalisi hatua hiyo, na nchi za Magharibi zikatoa ahadi hewa kwa Ukraine, kwamba zitaisaidia nchi hiyo hadi pale itakapofanikiwa kushinda vita dhidi ya Russia na kupunguza ushawishi wake. Matokeo yake ni kwamba, Ukraine haijapewa uanachama wa NATO, na kwa sasa, nchi hiyo imeachwa na wale waliokuwa wategemezi wake, na kwa sasa, Umoja wa Ulaya ndio umeachiwa jukumu la kusuluhisha mgogoro huo.

Baada ya hapo, vita kati ya Palestina na Israel ikaanza, na kuondoa ufuatiliaji wa vyombo vya habari na wanasiasa kutoka Ukraine hadi Palestina. Wakati majibu ya mashambulio ya Ukraine dhidi ya Russia yamesitishwa, vurugu ndani ya nchi hiyo zimeongezeka, na NATO imeanza kile inachojua kufanya, ambacho ni kuitupia lawama Ukraine.

NATO inadai kuwa, imeipatia Ukraine silaha inazohitaji na mafunzo, lakini nchi hiyo imeshindwa kudhibiti jeshi lake vizuri, uongozi wa nchi hiyo unavurugika,na kwamba Ukraine haina shukrani kwa NATO kama jumuiya hiyo ilivyotarajia, na mambo mengine mengi, na zaidi ya yote, kusema kuwa kamwe nchi hiyo haitakuwa mwanachama wa NATO wala Umoja wa Ulaya.

Kwa upande mwingine, Umoja wa Ulaya, ambao ni mwenzi wa Marekani, umeshindwa kuendeleza sera zake yenyewe kuhusu mgogoro wa Ukraine. Hifadhi ya silaha ya Umoja huo imeendelea kupungua kwa kasi, na sasa, Umoja wa Ulaya unakabiliwa na hali tete ya kisiasa huku ikipitia wakati mgumu wa kiuchumi katika historia yake.

Wakati Marekani ikilindwa kiasi fulani kutokana na athari hasi za matokeo ya sera zake, wenza wake wa Ulaya wanakabiliwa na hali ngumu. Mzigo wa kiuchumi kwa raia wake unaotokana na vita, mambo ya kijeshi, kuongeza silaha na wimbi la wakimbizi linalosababisha kumalizika kwa rasilimali zinazohitajiwa kwa dharura kwa miundombinu ya nchi za Ulaya, hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uwekezaji katika ustawi, hivi vyote vinaleta picha ya kutisha ya siku zijazo.

Kadri muda unavyokwenda, watu wataandamana barabarani, kwa ajili yao ama kwa kuunga mkono wengine, kama vile Wapalestina, jambo ambalo linafanyika hivi sasa. Wakati huohuo, nchi za mrengo wa kulia zitaona mapambazuko yake wakati mgogoro wa kiuchumi ukiongezeka.

Wakati nchi za Magharibi zikididimia taratibu, moja ya jambo linaloweza kutokea katika muongo ujao ama zaidi, ni kudhibiti mgawanyiko na uwezekano wa kuvunjwa kwa Jumuiya ya NATO.
 
View attachment 2847817

ASANTE SANA!! kuongezea kidogo tu!! U.S.A alishapigwa pale AFGHANSTAN mpaka wakatoka nduki {TALEBAN noma sana], lakini aibu kubwa waliipata SOMALIA,,,,,waligongwa na silaha ndogondogo tu kama SMG,LMG mabomu ya kurusha kwa mko na kutega ardhini,,,,yaani kubwa kwa WASOMALI ilikuwa ROCKET RANGER na RPG,,dhidi ya misilaha mikubwa na kutisha ya wamarekani!!
 
Back
Top Bottom