Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Marekani kuitikisa Tanzania kwa vikwazo

Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.
Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC. Hata hivyo serikali ya Tanzania bado haijatilia maanani jambo hilo huku ikioneknana kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki ichukue mkondo wake.
Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika mwezi october mwaka jana ambao ulielezwa kuwa huru na wa haki.
safi sana kama ni kweli huwezi kupora haki ya wananchi kiujanjaunja wa mwaka 47.eti mimi jecha kwa mamlaka niliyonao nafuta uchaguzi
 
Unajua viongozi wa Afrika huwa wajinga, Iran inafurahia hivi sasa baada ya sanctions kuwa lifted.....
Sisi hata matchstick twaagiza sasa itakuwaje wakipiga sanction
Matchstick tunatengeneza wenyewe kaka kuagiza miaka 10 nyuma MO naye anatengeneza. USA walikuwa na urafiki na JK hayupo na JPM hawamsomi ndio maana wanamjambisha tu.
 
Usilinganishe Tanzania na Iran na Russia.Wale uchumi wao wote unategemea mafuta na gesi wanazouza nchi za magharibi.Wakisusa tu kununua uchumi hoi na maisha hoi maana maisha yao yote hutegemea wapate pesa wanunue hadi chakula nje ya nchi.Tanzania tuna nini cha kuuza nchi za magharibi? Kila siku bidhaa zetu twazila wenyewe.Wanatupa visingizio kibao mara ziko viwango vya chini.Sisi wenyewe twala wala hatufi.

Ndio maana hata wakiweka vikwazo vinalenga kwenye luxury goods kama hiyo misaada ya umeme ambao ni kwa ajili ya wale ambao maisha bora kwa kila mtanzania yalishawafikia.

Mzee acha kuota...Tanzania tuna import 100%,wakifunga tu utanunua wapi wewe kama sio unajidanganya?

Eti tunajenga tunajilia wenyewe nchini?Tulishajenga nini?Tunaimport kila kitu,na wana block,tutakula matako yetu...nyie CCM ni useless
 
Huna jinsi ya kuepuka rungu la Wazungu, kumbuka wao kila kukicha wanashughulika jinsi ya kututawala. Na wamefanikiwa, hata hizi siasa tunazofanya wametutengenezea wao kwa kibwagizo cha uongo eti demokrasia

Upende usipende lazima uwapigie magoti tu, unajidai kuwa na maliasili nyingi wakati huna elimu. Una madini lakini huna hata katapila ya kuchimba. Pia bei wanakupangia wao, sisi bado tunashida sana kama hatutagundua jinsi ya kutengeneza siasa zetu wenyewe zilizojaa upendo haki na kuheshimiana. Sisi tuna nyama lakini kisu na vifaa vya kupikia wanavyo wao wazungu lazima tunyooke tu
 
Chanzo cha Irani kuwekewa vikwazo unakijua?Je wangekataa vikwazo wangefika hapo walipofika kwenye suala lililowasababishia vikwazo?
Wakamuulize muiran alikuwa kama amezibwa pumzi ya pua,kafunguliwa muone anavyonunua vitu kwa fujo kama ndo nchi inazaliwa leo, acheni kabisa kwenye vikwazo wazungu walicheza sana
 
Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.
Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC. Hata hivyo serikali ya Tanzania bado haijatilia maanani jambo hilo huku ikioneknana kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki ichukue mkondo wake.
Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika mwezi october mwaka jana ambao ulielezwa kuwa huru na wa haki.
kwa utawala huu na jinsi usivyo jali matatizo ya wananchi wako radhi wananchi wateseke kuliko kuachia madaraka au kutoa haki kwa wapinzani
 
Na wewe utakimbilia kwa mabwana zako huko magharibi

Majibu jibu yako yasio na mantiki reveals is greymatter is grossly mis-wired!!!!
kama nchi za scandinavia na japan ndio wangeweka vikwazo ningeshituka kwani marekani msaada wao huwa hauna nguvu pesa nyingi zinarudi kwao na kwa kasi ya kukusanya mapato ya tra sioni tishio lolote kama maji yakizidi unga itabidi tubane matumizi yasiyo ya lazima kama posho za wabunge,ruzuku za vyama na mifuko ya jimbo nawashukuru sana wakizuia misaada kwani ndio tutaona uwezo wa watendaji wetu

Mkuu siku hizi hata nchi za Scandinavia zinafuata maelekezo ya Merikani - ndio maana na wao waliwekea URUSI vikwazo vya kiuchumi wanashiriki vile vile kwenye mazoezi ya kivita na NATO wakati wao si wanachama, Japan ndio kabisa ni marafiki wakubwa wa Merikani.
 
kwan bila marekani tutakufa njaa
japo siafik ubakaji wa demokrasia uko ZNZ lkn shobo za kuwashobokea WHITE FORKS sizipendi kinoma mbna KOREAKASKAZINI wameweza bila marekani japo wakati wanaanza kukaza uzi walibezwa sana najua HATUWEZI KUJIFANANISHA NA KOREA KASKAZINI ila zama za sasa tujitengenezee mazingila ya kujitegemea wenyewe muda ndo huu wa kujenga nchi yetu TANZANIA afrca kwa ujumla tufufuke tuache uchu wa MADALAKA wangapi wababe walikuwapo leo awapo duniani
koba
MOBUTU SESESEKO JONAS SAVIMBI SANKARA wako wapi wamefukiwa na Bado maisha yanaendelea dunia tunapita tu
-Internet mnayoitumia ya mzungu
-Umeme mnaoutumia asilimia kubwa wa mzungu
-Watalii mnaowategemea ni wazungu
-Magari yote mnayoendesha ya wazungu
-Vifaa vyote vya kielectroniki (simu, computer, tv, fridge etc) mnaagiza toka nje
-Mbolea mnazotumia mnaagiza kwa mzungu
-Bank zenu zote ni local, mnategemea international banks kufacilitate international payments.
-Vifaa vyenu vyote muhimu vya kijeshi mnatoa nje.
NI KICHAA PEKE YAKE NDO ANAYEWEZA KUBEZA UTEGEMEZI WETU KWA US NA ALLIES WAKE.
 
Unajua viongozi wa Afrika huwa wajinga, Iran inafurahia hivi sasa baada ya sanctions kuwa lifted.....
Sisi hata matchstick twaagiza sasa itakuwaje wakipiga sanction
Hawawezi kukuelewa mkuu, watu wa ndio mzee ni shida, hata mavi wanaweza kusema ni mazuri
 
-Internet mnayoitumia ya mzungu
-Umeme mnaoutumia asilimia kubwa wa mzungu
-Watalii mnaowategemea ni wazungu
-Magari yote mnayoendesha ya wazungu
-Vifaa vyote vya kielectroniki (simu, computer, tv, fridge etc) mnaagiza toka nje
-Mbolea mnazotumia mnaagiza kwa mzungu
-Bank zenu zote ni local, mnategemea international banks kufacilitate international payments.
-Vifaa vyenu vyote muhimu vya kijeshi mnatoa nje.
NI KICHAA PEKE YAKE NDO ANAYEWEZA KUBEZA UTEGEMEZI WETU KWA US NA ALLIES WAKE.
Unategemea wao ni wa hovyo watakubari kupoteza soko lenye walaji zaidi ya milioni 40? Hivi mnafahamu kwa vikwazo huwekwa? Au mikumbo tu?
 
Unategemea wao ni wa hovyo watakubari kupoteza soko lenye walaji zaidi ya milioni 40?
Hah ha ha ha ha ha...you are kidding asee! Tz is not a potential market for the World giants ina any way. Labda kidogoo ungesema influence yetu ya natural resources.
 
Hah ha ha ha ha ha...you are kidding asee! Tz is not a potential market for the World giants ina any way. Labda kidogoo ungesema influence yetu ya natural resources.
Though unaonekana kuwa kidded, ila umesaidia kuonyesha upande wa pili why kuiwekea nchi vikwazo si jambo la kuamka tu na kutenda.

Unafahamu ni kwa kiasi gani china, uturuki, etc wanauza na wamewekeza Tanzania?
 
The voice of Mr Bush and Mr Blair can't decide who shall rule in Zimbabwe,who shall rule in Africa,who shall rule in Venezuela,who shall rule in Iran,who shall rule in Iraq.

We've said we can't collapse,never ever.We may have our droughts our poverty but as people we'll never collapse,never ever.

We don't mind having sanctions banning us from Europe as we aren't Europeans." Robert Mugabe
 
Majibu jibu yako yasio na mantiki reveals how u're greymatter is mis-wired!!!!

Mkuu siku hizi hata nchi za Scandinavia zinafuata maelekezo ya Merikani - ndio maana na wao waliwekea URUSI vikwazo vya kiuchumi wanashiriki vile vile kwenye mazoezi ya kivita na NATO wakati wao si wanachama, Japan ndio kabisa ni marafiki wakubwa wa Merikani.
Hizi ni post za kioga, watu kama nyie enzi Zile tunagoma vyuoni- huwa mnakutwa lecture halls mnajisomea.

Hivi unataka kuniambia Mnorway anaweza kuweka vikwazo au ajitoe huko Mtwara kwa uwekezaji wake kupitia stateoil? Huyo mnorway akichomoa basi mchina au mrusi anakuja, hatutaki misaada ya malaria, na kondom kupitia T-Mark na umarekani wao.
 
Back
Top Bottom