With all due respect, kwa differing opinion ya baadhi yetu, kwanza naheshimu mawazo ya wengi na kuna sehemu tuko pamoja, ile sehemu ya Mhe. Masele hakupaswa kuyasema haya!. Aliyepaswa kuyasema ni MFA, Mhe. Benard Membe!.
Sasa naomba niwarudishe nyuma kidogo, tangu enzi zile za kuupinga mfuko wa Jimbo, kuna "watu" walitoa fedha kwa NGO zikafanya uhamasishaji wa hali ya juu, zikaweka hadi kambi Dodoma wabunge waupinge mfuko wa jimbo, lakini wengi wa wabunge wetu walivyo njaa kali, walivyo walafi, walivyo wachumia matumbo, very few can say no to ulaji!, mfuko wa jimbo ukapita!. TISS wanajua who was behind!, JK anajua!, Membe anajua!, ilikuwa ni kinyume cha Viena Convention!, lakini wote walijinyamazia kimya simply kwa kitu kinachoitwa "Diplomasia!".
Eti huwezi kulikata tawi la mti ulioukalia!, au mkono unaokulisha ukipakwa ma..!, huwezi kuukata!, utausafisha tuu na kuendelea kuutumia kula chakula!, na ikitokea hakuna maji ya kuusafishia, unaufuta tuu na kuulia!, au ufe njaa?!. Hiki ndicho Tanzania tunachokifanya siku zote!. Tumeonewa Kiasi cha Kutosha, Tumenyanyaswa Kiasi cha Kutosha, Tumedhalilishwa kiasi cha Kutosha, Tumepuuzwa Kiasi cha kutosha!. Unyonge wetu ndio umetofanya, tuonewe, tunyanyaswe, tupuuzwe na kudhalilishwa!. Mhe. Masele ametufundisha tunaweza kusema no!.
Lilipokuja suala la gesi asilia, sio wengi humu mnafahamu ni kampuni gani ndilo lenye vitalu vingi na wanaendelea kuomba vitalu!. Hilo kampuni lilipanga wajenge LNG Plant floating kule kule high sea ili watuibie vizuri gesi yetu!. Serikali ilipopitisha uamuzi wa LNG Plant lazima ijengwe on the land!, uamuzi huo ukawa ni pigo kwa mabeberu, wakoloni mambo leo hawa, ambao wameamua kutuibia mchana kweupe!. Ule upinzani wa bomba la gesi ulichochewa ili bomba lisijengwe!, TISS wanamfahamu "mchochezi huyo!", JK anamfahamu!, Membe anamfahamu, Mhongo anamfahamu!, wenye ufahamu, wanamfahamu!, ila wote walimnyamazia kwa kile kile kinachoitwa "Diplomasia ya Beggars Syndrome Cowardice!".
Kwenye hili la gesi, nililizungumza siku nyingi Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- Watanzania Tunaibiwa Mchana Kwepee! tangu 27th July 2012 04:34 masikini wana JF, ni wachache wetu wenye uelewa wa baadhi ya haya mambo, thread ile ya iliishia page 1!.
Lilipokuja suala la Bajeti ya Nishati na Madini, "insiders" walijua nini kinachoendelea, bahati nzuri wizara ile sasa imeshikwa na really people who plays real game! na sio kuendelea kuwategemea hawa "kujikomba komba politicians kwa jina la diplomasia!" Mhe. Masele (by nature Wasukuma ni masikini jeuri!, sio watu wa kujikombakomba kwa lolote na kwa yoyote!), akaamua to hell with what is called "diplomsia na kuamua to take the bull by its horns!", kama ni kumuua nyoka!, you start by hitting the head! not the tail, and when you decide to strike, you just hit the target and where it hurts most and not the usual way of beating around the bush!.
Tuhuma zile ni nzito!, zimetolewa bungeni!, nilitegemea au Ikulu ingetoa official statement ku clarify!, na waziri Membe angekuja na kauli ya serikali bungeni!, kama Masele amezungumzia Bungeni, official channel!, kisha Balozi Sefue anajibia "gengeni" huku Membe yuko kimya na sasa Balozi anakuja kujisafisha kwa jinsi walivyotusaidia na watakavyoendelea kutusaidia! badala ya kujibu tuhuma!, unategemea nini?!.
Huu umasikini wetu, uomba omba wetu, utembezaji bakuli wetu, usitufanye tuendelee kudhalilishwa!, wengi mnaujua "uwezo wa JK" na boldness yake ya "udhaifu" and so does Membe!, hawangethubutu!, nilidhani by now Masele angeishafanywa ndiye "kondoo wa kafara!", ikibidi punda afe lakini mzigo ufike!.
Mhe. Masele ameonyesha ushupavu wa hali ya juu sana! na kitendo alichokifanya ni cha kishujaa sana mpaka pale hoja zake ama zitapojibiwa kibunge!, au zipanguliwe hoja kwa hoja na sio kama hali ilivyo sasa hoja zinapanguliwa na viroja! halafu watu wanashangilia ujinga!.
NB. Kama mtaninote sizungumzii kabisa "fedha na escrow account" that is pure bussiness!. Hapa tunazungumzia kitu kinaitwa "patriotism, sovereignty na national pride!", Tanzania is never poor!, huku kuomba omba na kutembeza bakuli kila siku ni tabia!. Gesi ni yetu!, tunabembeleza as if hakuna mwingine yoyote mwenye kuweza kuichimba!.
Tufike mahali Watanzania wote tuwe kama Wasukuma!, ukitendewa visivyo, unasema No! no matter what and you mean no!, Mwanza walisema No to ujinga ujinga, Nyamagana pia wakasema no tu ujinga ujinga!, japo ukabila sio kitu kizuri!, lakini kuna makabila fulani fulani kazi yao ni kujikombakomba tuu, kamwe hawawezi kusema no kwa ujinga ujinga wowote!, hata wafanywe vipi, wao watacheka tuu!, kama huamini shuhudia jinsi baadhi ya omba omba wanapotupiwa pesa na wenye magari, wanavyozikimbilia kwa furaha!, au nenda kampe omba omba noti yoyote huku unamtukana aone atakavyokushukuru!. Hivi ndivyo tulivyo!. ikibidi sasa, tuyahamasishe yale makabila machache ya "no nonsense!" yaseme no kwa ujinga ujinga ndipo tutaweza kutoka humu tulimo vinginevyo we are doomed!!. Mhe. Masele ni shujaa!, ameonyesha njia!, he has the guts to say no to nonsense!.
Wale wengi wenzangu na mimi, wenye high sense of nationalism na patriotism, lets join forces to say no to ujinga ujinga wowote against our sovereignty for restoration of our national Pride!. Nyerere aliweza na kuna wakati aliwagomea Waingereza!, aliigomea IMF na WB, japo watt walivaa magunia na uniform zilikuwa madurufu, but we were proud Tanzanians!.
Yes We Can!.
Pasco