Sina hakika kama unaelewa unachokiongea mkuu; ukiwekewa vikwazo vya kiuchumi, misaada ni sehemu ndogo sana ya vikwazo hivyo, nchi kama Irani na Iraq enzi ya Sadam Hussein sidhani kama zimewahi kuishi kwa misaasa, wanacho kifanya hawa jamaa kama kwa mfano wakiamua kukuwekea vikwazo kwanza hawafanyi biashara na wewe, wanawaambia raia au makampuni yanayofanya biashara na sisi kuondoa biashara zao nchini na ikumbukwe USA ni kama ndio kilanja wa Ulaya, akisema hafanyi biashara na wewe mataifa mengi (sio yote) ya Ulaya nayo yata copy na ku paste, kwa nchi kama Tanzania wakifanya hivyo kwa siku walau 20 tu nakuhakikishia tunashika ADABU na kurudia kile wanachotaka, nadhani ungeyaona makosa yanayofanywa na ccm kuhusu Zanzibar kwanza ndipo useme ulichokisema hapo