Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

ingekuwa amri yangu lipumba asingeingia uraiani mpaka baada ya mwaka.

Sema hawa watawala sasa hivi wana huruma sana, mtu anavuruga amani ya nchi na bado anaachiwa kwa dhamana?
maandazi republic.
 
i concur with you, Kikwete ni part of the game. Natamani Rugemarila azungumze ya moyoni
Rugemalila ni mtu ambaye anatakiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Nashangaa kwa nini ukawa hawashinikizi hilo. Hata kwenye maazimio ya bunge hakukuwa na azimio la kumtaka Rugemalila kuwajibishwa
 
Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Pata habari kamili yenye mahojiano na Marando, Jumatano wiki hii.

Awamu ya nne ni majanga na bado.....!
Hayati Mwl Nyerere alituonya tukampuuza
 
I have been daying the same from day one of my comments on this saga.

Bongo watu wanamuogopa sana rais.

JK mwenyewe amenukuliwa akisema keamba ana shaka akistaafu atashitakiwa.

Hiyo sheria haipo nchini labda akifukuzwa.
 
Ruge katembeza mgao kwa familia nzima mama Wama kachukua bilioni zake na watoto pia hawakusahaulika ndio sababu list ya mgao kupitia Stanbic inafanywa siri kubwa sana ili wezi na wapokea rushwa ndani ya Ikulu wasiadhirike.

List ya Stanbic itawekwa wazi mwezi wa pili. Kaeni mkao wakuwafahamu waliyonufaika na zile fedha hizo!
 
JK alisema pesa za escrow siyo za umma na kwake yeye IPPTL kumbe naye amevuta mkwanja wa kutosha hapo ccm itaangamiza taifa.
 
List ya Stanbic itawekwa wazi mwezi wa pili. Kaeni mkao wakuwafahamu waliyonufaika na zile fedha hizo!
wale ni malaika wa ccm wakitajwa nchi itatisika lakini baada ya kufukuzwa muhongo tutashudia mengi sana kuna kumwaga ugali na mboga
 
Mkuu, yaani kwa huu upuuzi wa Kubenea na Marando unataka tukae kimya?

Unauita upuuzi halafu hutoi hoja yoyote ya msingi kuonesha kuwa alichosema Marando ni upuuzi. Wenzio wamejenga hoja na kuonesha ni jinsi gani Rais na familia yake wanahusika na fedha za escrow. Wanaweza kuwa waongo lakini wameonesha logically namna walivyofikia hitimisho lao. Wewe unasema tu ni wapuuzi, halafu unaishia hapo na kwa fikra zako unatarajia watu wakuamini tu bila kujenga hoja mujarabu. Kwa kusema tu Marando ni mpuuzi, hakuna ulichobadili bila kuonesha bayana upuuzi wa Marando. Ni bora ukae kimya kwa kuwa unapoteza tu muda wako na hufanyi utetezi wowote kama unavyofikiri.

Kwa ushauri, subiri usome mahojiano yote kwenye gazeti kabla hujakurupuka kutetea. Na una haki ya kutetea endapo tu wewe ni Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa ndiye anayetuhumiwa. Huwezi kujitetea kwa niaba ya Jakaya Kikwete simply because it does not work that way. Kama wewe ni msemaji wake na amekutuma uje useme Marando ni mpuuzi, basi weka wazi ili tujue kuwa Kikwete amemwita Marando mpuuzi. Short of that, tutakuuliza umejuaje kuwa Kikwete na familia yake hawakupokea mgao wa fedha za escrow?
 
Hii ishu ambaye alikuwa hajui kuwa Kikwete ndio mwizi namba moja wa escrow lazima ni mbumbumbu. Hotuba yote ya tar 22 ilikuwa ni kutetea escrow na Singasinga akasahau kabisa maslahi ya nchi kwa vile anajua maslahi ya Singasinga ni yake pia. Kilichokosekana ni wa kumvika paka kengere. Ndio maana wanahaha kutumia mabavu ya polisi kuua UKAWA kwa vile wanajua wizi aliofanya Kikwete ni zaidi ya Mkapa
 
- Habari imeandikwa na Saeed Kubena kwa niaba ya nani? hahahahahahaha

Le Mutuz
Wiliam grate minds deals with issues and not personalities!hata kama ni Kubenea ameandika nawe humpendi?deal na hoja alioileta jamvini siku mua attack yeye binafsi!only poor minds discuss people!wewe ni msomi hili unalijua vema..
 
Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Pata habari kamili yenye mahojiano na Marando, Jumatano wiki hii.

Bunge si limeanza! Pachimbike tu ili tujue MNAMAANISHA basi!
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
Wewe Le Mutuz kwa sababu uko karibu na jikoni tuambie basi ukweli wa sakata hili. Huwezi kumpinga Kubenea bila kutaja ukweli ni upi. Umebadilika sana tangu ulipokuwa New York.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Liazboni, kama huna hoja za kutetea jambo kaa kimya, vinginevyo unazidi kumuharibia unayedhani una mtetea! Hivi kweli intelijensia yetu watu wakutetea kwa hoja wameisha kabisa kabisa kiasi kwamba hawaoni vile unaharibu, wamweke mwingine badala yako na Mussa Allan?

Kubenea ameandika au amesema kile kilichosemwa na M​abere Marando, lakini wewe umekazania Kubenea, Kubenea, kubena...! Na Kesho mfanye kama siku ileee, mliponunua magazeti karibu yote ya Mawio kila kona na kuyatia kiberiti! Safari hii tutaomba Mhariri wa Mawio, airudie story hiyo kwa wiki 3 mfululizo!

Au malipo yako ni ili mradi useme chochote?
 
Le Mutuz, you always amaze me kwa uchangiaji wako tu.

Nahisi kwa wakati fulani kichwa (akili) chako kinakosa busara kabisa.
Nadhani huyu alipoondoka New York aliacha sehemu ya brain yake huko.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom