Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

"Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu," ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, "Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe."

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

"Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais," ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni "mmiliki mpya wa IPTL/PAP," Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, "Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa."

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, "Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake."

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
 
Escrow kumbe bado ni mbichi?

Ndio maana Muhongo alisema nchi itatikisika... sasa tunaanza kuelewa.

Maana nasoma mbapa hasira
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Htushangazwi na majibu yako.
 
Hivi hujiulizi raisi wa nchi mwenye mamlaka ya kuagiza karibu kila kitu anashindwa kumshitaki Marando?

Nasema hivi kwasababu najua hawatathubutu kumshitaki.
 
Nadhani wewe ndiye mtoto,kiakili,huku tu mtaani wananchi wanajua rais na familia yake wanahusika moja kaw moja,ngoja nikuelimishe kwa swali dogo,je inawezekana kwa waziri yeyote kupiga hela bila rais kujua?hata mtoto wa chekechea atasema haiwezikani!unapinga kwakujipendekeza labda unatafuta kitu fulani na ni kwasababu sheria za nchi hii ni mbovu tu,hatavrais alipaswa kuwajibishwa na kufikishwa mahakamani.
 
- Rais wa Jamhuri aache kazi zake za Taifa akahangaike na no body Marando ni nani kwani?

Le Mutuz
 
Nadhani wewe ndiye mtoto,kiakili,huku tu mtaani wananchi wanajua rais na familia yake wanahusika moja kaw moja,ngoja nikuelimishe kwa swali dogo,je inawezekana kwa waziri yeyote kupiga hela bila rais kujua?hata mtoto wa chekechea atasema haiwezikani!unapinga kwakujipendekeza labda unatafuta kitu fulani na ni kwasababu sheria za nchi hii ni mbovu tu,hatavrais alipaswa kuwajibishwa na kufikishwa mahakamani.

- Wewe umechaguliwa lini kuwa msemaji wa mtaani? hahahahahah kumbe unajipendekeza so unadhani wengine wote ni kama wewe unaona unajivua nguo mwenyewe

Le Mutuz
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Le Mutuz wewe unabebeleza na kutengeneza mazingira ili Jina lako lisijekatwa jimbo la MTERA.

Ukisimama kupambana na MWENDAWAZIMU NA MROPOKAJI LUSINDE atakushinda na Utaambulia aibu ya mwaka 2015.
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Je wewe Li-mutuz utamweza kibajaji? baba yako alishindwa
 
Ktk kipindi cha mkasi wiki hii, Tundu Lissu alisema, katiba inamlinda Rais akiwa madarakani na hata akitoka madarakani, hawezi shitakiwa!

Hivyo, zitapigwa kelele ila ndo basi tena!
 
Kikwete anajua kwamba hajaweza kukusanya kiasi alichotaka awe nacho na pesa za ESCROW zilikuwa ndizo tumaini lake la mwisho!
Pesa alizotegemea kupata kutoka Muscat anasema ni kiasi kidogo sana kwa watu wenye hadhi ya uraisi!
*Kikwete anategemea kununua shares kwenye makampuni ya nje na sasa hivi anataka vumbi likishapita ajiondokee kwa amani akaanze biashara ya Security Equipments (deal lake la kwanza litakuwa kuuza vifaa vya kijeshi!!!!!!)
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Nasikia utagombea ubunge yahke! Naona umeanza kuanalaizi ishu sensitivu japo ulivyoanalaizi ni sawa tu na hamna
 
Ruge katembeza mgao kwa familia nzima mama Wama kachukua bilioni zake na watoto pia hawakusahaulika ndio sababu list ya mgao kupitia Stanbic inafanywa siri kubwa sana ili wezi na wapokea rushwa ndani ya Ikulu wasiadhirike.
 
Back
Top Bottom