Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Mungu bwana muache aitwe Mungu,Ndege wanazopanda raia wema zinapotea au kutumbukia baharini ili hizi wanazopanda hawa watu wetu hazipotei bana?

Mfumo ndio tatizo, akiondoka fisadi mmoja mwengine anashika nafasi ile na wizi unaendelea kama kawa.
 
Mfumo ndio tatizo, akiondoka fisadi mmoja mwengine anashika nafasi ile na wizi unaendelea kama kawa.
Mkuu tatizo si mfumo,tatizo ni hii mijitu iliyomo kwenye huo mfumo.Watanzania tulitaka kubadilisha huu mfumo kupitia rasimu ya katiba mpya maarufu kama Rasimu ya Walioba unakumbuka nini kilitokea na kinachoendelea kutokea?Ila kama ingetokea ndege iliyowabeba ikazama bahari ya hindi basi tutakuwa tumepata nafasi ya kubadirisha huu mfumo bila kumwaga damu za watanzania masikini wasio na hatia
 
UKAWA ni Muungano wa ajabu sana, Profesa wa Uchumi anamuiga LEMA, mhitimu wa std 7.
 
- Rais wa Jamhuri aache kazi zake za Taifa akahangaike na no body Marando ni nani kwani?

Le Mutuz

Tunakushangaa pia wewe hapa unahangaikia nini kama ni no body? Kinachoonekana ni Mijizi inatetea mijizi mingine. ZNSMAOSAOS099jaisapsksa kabisa
 
Haitoshi tu kusema kuwa JK anahusika au mnufaika wa fedha za escrow bali mchekeshaji kubenea anapaswa kutuambia jinsi JK alivyonufaika na fedha hizo
 
Mwandishi mwenyewe said kubenea lile jizi lenye mdomo mwekundu ha ha ha ha.

kubenea kichwa chake kinawaza kupewa hela mda wote ni zaidi kunguru aliwahi kupewa hongo ndogo sana ili kumchafua mtu.

Pathetic....! Hivi mnaandika kumfurahisha nani? How do you judge other people's looks when you can't create even shit???
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
Hi lemtuz , mshua anatamani kuwa malaika. Anatamani kuwa mtoto
 
Pathetic....! Hivi mnaandika kumfurahisha nani? How do you judge other people's looks when you can't create even shit???
Mkuu, umezoea kuandika kwa kufurahisha watu nini?
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
Mkuu umesema kweli, vistory vya kuungaunga tuu ili mradi Rais achafuliwe. Marando aliambiwa athibitishe ataweza?
 
Ingekuwa Amri yangu LIPUMBA asingeingia uraiani mpaka baada ya mwaka.

sema hawa watawala sasa hivi wana huruma sana, mtu anavuruga Amani ya Nchi na bado anaachiwa kwa dhamana?
 
Mkuu umesema kweli, vistory vya kuungaunga tuu ili mradi Rais achafuliwe. Marando aliambiwa athibitishe ataweza?
Mkuu, hakika hawezi na hatakuja kuweza. Marando naye ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine waliojazana ndani ya ukawa
 
Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Pata habari kamili yenye mahojiano na Marando, Jumatano wiki hii.

huo ndo ukweli na ndomana mawaziri wake hawakuona sababu ya kujiuzuru wakati muhusika ni yeye jk. alitaka awatoe kafara wakakataa
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Nakuuliza maswali mafupi tu, je hiki ninachokinukuua hapa chini ni kweli au si kweli? na je katika report ya PAC hiki ninachokinukuu hapa chini hakikuonyeshwa?

''Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.''
 
Back
Top Bottom