Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow


Posted by: Saed Kubenea


RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.


“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Pata habari kamili yenye mahojiano na Marando, Jumatano wiki hii.





Eti Marando naye kaamua kusaka Kiki kupitia escrow kwa Habari za kukariri , Marando mbona umewasahau ndugu zako Mbowe, slaa, Mnyika , Lema na Wenje ambaye ndiye aliambatana na Mbowe kwenda Kenya kuchukua mkwanja. Pesa za escrow zimeliwa sana humo Chadema na wajanja wa chama, lakini Marando aliachwa na njaa yake, Sasa kakumbuka shuka kumekucha , kapewa vijicenti na Mengi kaamua kuropoka .
 
Sikutegemea karibia Taifa lote lingecheze ngoma ya Nimrodi Mkono kiasi hiki kwenye sakata la Tegeta ESCROW. Gharama za uwekezaji wa 100MW wa IPTL ni TZS50,00? 'Capacity charge' ikokotolewe kutokana na TZS50,000 ambazo IPTL aliwekeza? Hivi tunajua kweli 'Capacity Charge' ni nini au tunashabikia siasa tu?
View attachment 222485
Huu hapa chini ndio ulikuwa ushauri kitaalam kwa kuzingatia maana hasa ya 'Capacity Charge'
View attachment 222484
 
Liazboni, kama huna hoja za kutetea jambo kaa kimya, vinginevyo unazidi kumuharibia unayedhani una mtetea! Hivi kweli intelijensia yetu watu wakutetea kwa hoja wameisha kabisa kabisa kiasi kwamba hawaoni vile unaharibu, wamweke mwingine badala yako na Mussa Allan?

Kubenea ameandika au amesema kile kilichosemwa na M​abere Marando, lakini wewe umekazania Kubenea, Kubenea, kubena...! Na Kesho mfanye kama siku ileee, mliponunua magazeti karibu yote ya Mawio kila kona na kuyatia kiberiti! Safari hii tutaomba Mhariri wa Mawio, airudie story hiyo kwa wiki 3 mfululizo!

Au malipo yako ni ili mradi useme chochote?

Kubebea kaamua kupakazia Kwa Jk tu, lakini ndugu zake Akina Mbowe walikula pesa Nyingi kaamua kuwafichia siri .
 
Eti Marando naye kaamua kusaka Kiki kupitia escrow kwa Habari za kukariri , Marando mbona umewasahau ndugu zako Mbowe, slaa, Mnyika , Lema na Wenje ambaye ndiye aliambatana na Mbowe kwenda Kenya kuchukua mkwanja. Pesa za escrow zimeliwa sana humo Chadema na wajanja wa chama, lakini Marando aliachwa na njaa yake, Sasa kakumbuka shuka kumekucha , kapewa vijicenti na Mengi kaamua kuropoka .

Hata kama maneno yako yakithibitishwa kwamba ni sahihi siyo utetezi wa JK na familia yake ktk wizi wa Escrow!
 
Sikutegemea karibia Taifa lote lingecheze ngoma ya Nimrodi Mkono kiasi hiki kwenye sakata la Tegeta ESCROW. Gharama za uwekezaji wa 100MW wa IPTL ni TZS50,00? 'Capacity charge' ikokotolewe kutokana na TZS50,000 ambazo IPTL aliwekeza? Hivi tunajua kweli 'Capacity Charge' ni nini au tunashabikia siasa tu?
View attachment 222480
Huu hapa chini ndio ulikuwa ushauri kitaalam kwa kuzingatia maana hasa ya 'Capacity Charge'
View attachment 222484

Mtahangaika sana lkn ndiyo hivyo tena jahazi linazama! Likisha pinduka kabisa tutasimuliwa mengi ambayo Watanganyika hawajawahi hisi hata kama watawala wao wako capable kuiba na kupora mali ya umma kiasi hicho! Usione watu wanahangaika kuhujumu kila jambo litakalo warudishia wananchi madaraka na mamlaka ya kuwawajibisha wazembe,wabadhirifu,wala rushwa,nk ukadhani ni jambo dogo. Wanaogopa aibu na jela!
 
Rugemalila ni mtu ambaye anatakiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Nashangaa kwa nini ukawa hawashinikizi hilo. Hata kwenye maazimio ya bunge hakukuwa na azimio la kumtaka Rugemalila kuwajibishwa

Kwani kosa la Rugemalila ni lipi ?
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

We huku hapakufai uwezo wako wa kuchambua mambo kwa kina ni mdogo sana nenda kule kwa watoto wenzio mnaogombania soda zenye majina Le kubwa jingaaazzzzzz.
 
Kwani kosa la Rugemalila ni lipi ?

Hana kosa kwani Si alilipa Kodi faida yake akagawana na jamaa zake, akiwemo Mbowe , Mnyika,lema , wenje na wenzao ingawa wengine wasanii akina Lema na Mnyika walivuta pesa Kote Kote mpaka Kwa Sethi kabla ya kuhamia Kwa mengi wakavuta nyingi na kuwa full vigeu geu, Hiki ni kipindi cha kuvuna pesa Kwa Wabunge hususani wale wabunge Wenye Asili za usanii na wizi , kila mmoja Yupo busy anabuni yake ili atokee huko huko apate pesa za Kampeni humo humo.
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
krapu!
damnit-763.jpg
 
Rais ni Mwizi hakuna jinsi hapo. Lazina ashitakiwe tu huyu akiacha madaraka.
 
Unajenga hoja kwa kutumia kigezo gani sioni mantiki ya hoja yako unabwabwaja tu kama ndege mkiwa juu ya mti.

Utaonaje mantiki na ushashindilia bk saba mfukon?
Mlaaaniweee na vizaz vyenu
 
Uwazi unajionyesha kabisaaa wakati,boss wetu alivyokuwa anasua sua kufanya maamuzi. Sasa taratibu aliyewaripua wataanza kumripua. Tutayasikia yote. We unadhani tibaijuka zile hasira za kusema thitoki, thitoki, thijiuzuru..zimekwisha? Mi nakwambia patawaka hadi pateketee ili kuwapunguzia kazi ya kupasafisha wanaokuja kupatumia baada ya0. Ccm oye!!!
 
That is why report ya PCCB wameishikilia. Wanapaswa kutambua kuwa hakuna dhuruma isiyo kuwa na hadhabu, kama siyo leo miaka ijayo watakuja kuwajibika. Ni pesa za walalahoi wanaokufa kwa kukosa dawa hospitali.
 
Back
Top Bottom