Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Hivi hujiulizi raisi wa nchi mwenye mamlaka ya kuagiza karibu kila kitu anashindwa kumshitaki Marando?

Nasema hivi kwasababu najua hawatathubutu kumshitaki.

sijawahi kuona mwenye akili timamu akajibizana na kichaa, zaidi sana ukifanya hivyo utaonekana wewe ndio kichaa
 
Hivi hujiulizi raisi wa nchi mwenye mamlaka ya kuagiza karibu kila kitu anashindwa kumshitaki Marando?

Nasema hivi kwasababu najua hawatathubutu kumshitaki.

Bonge la komentiiii, leo umefunguka bila shinikiZo. Big up
 
Hivi mzee wetu aliyepigwa stop kugombea uraisi kwa sababu ya udini wake hajapata mgao kweli pale Stanbic
- Wewe umechaguliwa lini kuwa msemaji wa mtaani? hahahahahah kumbe unajipendekeza so unadhani wengine wote ni kama wewe unaona unajivua nguo mwenyewe

Le Mutuz
 
Hii kitu imeliacha Taifa uchi, japo kuna vijiutetezi vya kulazimisha Ili tuamini kuwa hili suala halihusu wakuu lkn bado wingu ni Zito sana,Sasa Marando kaamua kujilipua ngoja tuone na kumtaja Mkuu wa kaya waziwazi namna hii Ni wazi ana uhakika na akisemacho.

Hawatajibu chochote hapo, wakijitahidi saaaaaaana saaaana basi watakanusha lkn sio kumshitaki, kumpeleka mahakamani hawaweziii
 
nyaucho ndio ameamka sasa hivi? maana ameongea kama mtu aliyetoka usingizini...yeye anajua kuwa familia ya kikwete imechota hela halafu akakaa kimya akaacha CAG na Takukuru wakafanya ukaguzi na uchunguzi bado hakuwaambia kamati ya bunge mpaka maazimio yametoka ndio anakuja na wimbo uliochuja....kama ni ukumbini wa dansi Marando angerushiwa chupa za maji lakini kwenye uzi naona tum-mbedye tu

Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Sio jambo la ajabu kwa huyu mburula kuandika ujinga huu; anajipendekeza pengine anaweza kuambulia makombo wakati huu wa lala salama wa mkweree!! Si mnaona jinsi baba yake na mama yake wa kambo walivyokumbukwa wakati huu wa majeruhi; mkweree is trying to mend fences!!
 
Si tu anatakiwa kujibu bali anapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani akatoe ushahidi huko

Thubutuuuuu!!! Waanzie wapi kufanya ivyo? Labda wamuue lakn kumfikisha mahakamani hawawezi ng'oo, hata wewe ukiwashauri hivyo watakushangaa saaana. Jaribu tuone
 
I have been daying the same from day one of my comments on this saga.

Bongo watu wanamuogopa sana rais.

JK mwenyewe amenukuliwa akisema keamba ana shaka akistaafu atashitakiwa.

Katiba hairuhusu mtu aliyekua rais kushitakiwa. Wizi wake uzembe wake na makosa yake yanalindwa na katiba. Tukibadili katiba tutaweza kumfanya raisi pindi awapo madarakani kuwa na nidhamu na ofisi kuu ya nchi.
 
....rais anajua na alikuwa anajua kuhusu fedha hizo,nakubaliana na msomi Marando
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz
Lazima umsifie, si unajua mazeri kapewa ulaji. Nguvu ya kumsema unaitoa wapi:wacko:
 
- Wewe umechaguliwa lini kuwa msemaji wa mtaani? hahahahahah kumbe unajipendekeza so unadhani wengine wote ni kama wewe unaona unajivua nguo mwenyewe

Le Mutuz
Wewe umechaguliwa lini kuwa msemaji wa rais, ikulu, serikali. Kweli nyani haoni............
 
Si tu anatakiwa kujibu bali anapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani akatoe ushahidi huko
Afikishwe kwenye mahakama hizi ambazo majaji wamepojea rushwa. Hivi unawaza kwa kutumia kichwa au kitu kingine. Aliyewateua mchafu, walioteuliwa wachafu unategemea nini. Kuhusu kujiuzulu Muhongo ulitoka povu sana nadhani kwa kilichotoke unajijua upo kwenye kundi gani kati ya toilet paper au mti😛oa
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Kwani wewe Mwana wa Malecela hii habari mbona unaisemea kwa ukali na uhakika inakuhusuje binafsi? si uwaache wenyewe waje wajisemee? Tukisema pia umelipwa kwa hayo unayoyaandika tutakuwa tumekosea?
 
Jk is partly responsible kosa lake negligence!

Taarifa za malipo ya escrow zilifikishwa Ikulu na Governor kabla kulipa. Ikulu ambaye ni rais wakasema fuateni maelekezo ya mwanasheria mkuu.

So that marando guy over there ana point kidogo.

Tatizo ni kwamba mkubwa hakosei ndio maana Mhongo kang'oka kumpa ahueni rais na serikali.
 
Mkuu kwa mtu mwenye akili anajua kabisa kuwa Rugemalira is Innocent, Ametumika tu .Rugemalira hana ubavu wa kugawa pesa kama njugu kwa Viongozi wa serikali, Tetea ukijua kuwa kuna siku utatoa hesabu yake.

Mtu anayeuza chake ana haki ya kukitumia atakavyo. Wezi ni wale waliochukua pesa kutoka Benki Kuu wakazipeleka Stanbic wakagawana kwenye lumbesa na hawatajwi kwa sababu wakubwa wamo.
 
@W.J.Malichela Hongera naona umeajiriwa Ikulu kufanya kazi za
Salva Rweyemamu!!
Twambie huyo Mbene ni nani !!
 
Upuuzi mtupu marando ndio mwenye habari za uhakika?
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

William aka baharia, unapaswa kuelewa kwamba mtu makini hujibu kwa hoja lakini wewe unaonyesha uwezo wako wa kufikiri una utata, unasukumwa kwa ushabiki na utumwa wa fikra.

Kubenea hafanani na wewe kwani ni mtu makini kuliko wewe maana ameandika yale ambayo wakili Marando ameyabaini na kuyasema na ana uhakika nayo ikiwa ni pamoja na vielelezo.

Kama wewe au Rais mnaona kuwa Marando au mwandishi wa habari hizi ni mzushi na mchonganishi mna haki ya kwenda kushitaki mahakamani; tuone kama mnajeuri hiyo.
 
Back
Top Bottom