Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

Marando: Kikwete mtuhumiwa Escrow

marando is somebody more than your father mother and you chap.alafu uoni hata aibu how dare you compare your self with marando!!hata huyo raisi wako unaemlamba viatu hamfikiii marado.
au kwa kuwa marando sio pfofesa wa kichina
?
 
Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Nikweli Mh. Marando amenena na HILI SUALA 99% YA WATANZANIA WAEREVU WANALITAMBUA KUWA MKUU AMELAMBA JOKA NAYE PIA. Ila sasa katika serikali hii ya CCM hakuna UWAJIBIKAJI ukiwa mwizi ni sifa KUU KWAO.

Hivyo basi hata MAFISADI HAWA WAWAJIBIKE WASI WAJIBIKE KIAMA CHAO KINAKUJA MUDA SI MREFU KUTOKA KWA ALLAH NA KWETU PIA SISI WATANZANIA KWA KUWAONDOA MADARAKANI IFIKAPO OCTOBER 2015, THEN MOTO WA JEHANAMU BAADAYE WAKAKUTANE NA MUUMBA WAO NA KUJIBU MASWALI YAO.
 
Hii ishu kweli bado ni mbichi na hii ndio itaimaliza ccm,pesa imepigwa halafu haijafika kwenye chama imeishia mifukoni mwa familia ya raisi safi sana.cham kitafanya kampeni na nini sasa?pinda naye kapiga sasa hapo ndipo patamu na kweli hii inaila ccm na wahusika wote watatajana,tunaendelea kupata majina ya wezi wa pesa zetu,Mungu wangu wakati maskini hawana chakula,hawajalipwa pesa zao za mazao jamani serikali haina huruma.Mungu iangalie Tanzania kwa jicho la pekee
Mkuu Elinewinga, msiharakie kusema hivi. Uchaguzi ni mwezi wa kumi sasa inawezekana bado pesa ilikuwa imehifadhiwa sehemu ikisubiri muda mwafaka ili ipelekwe kwenye matumizi stahiki!

Nikweli Mh. Marando amenena na HILI SUALA 99% YA WATANZANIA WAEREVU WANALITAMBUA KUWA MKUU AMELAMBA JOKA NAYE PIA. Ila sasa katika serikali hii ya CCM hakuna UWAJIBIKAJI ukiwa mwizi ni sifa KUU KWAO.

Hivyo basi hata MAFISADI HAWA WAWAJIBIKE WASI WAJIBIKE KIAMA CHAO KINAKUJA MUDA SI MREFU KUTOKA KWA ALLAH NA KWETU PIA SISI WATANZANIA KWA KUWAONDOA MADARAKANI IFIKAPO OCTOBER 2015, THEN MOTO WA JEHANAMU BAADAYE WAKAKUTANE NA MUUMBA WAO NA KUJIBU MASWALI YAO.
Comment nzuri, wote wenye uelewa wanajua kuwa hakuna uwajibikaji katika serikali ya ccm lakini kuwajibika kupo pale pale. Mfano ni wote waliokwisha wajibika hadi sasa nguvu iliyowasukuma kufanya hivyo imetoka nje ya ccm kwa mchango mkubwa wa kiumbe mdogo sana, tumbili! Nguvu hii inaendelea kuwepo na itawasukuma wengine pia.
 
Ktk kipindi cha mkasi wiki hii, Tundu Lissu alisema, katiba inamlinda Rais akiwa madarakani na hata akitoka madarakani, hawezi shitakiwa!

Hivyo, zitapigwa kelele ila ndo basi tena!
Akiingia kichaa katiba inabadilishwa na anashitakiwa Ref: Zambia
 
mambo makubwa yanachukuliwa kilaini,majibu laini,action laini,mfano escro ila mambo madogo action kubwa mfano malalamiko ya wafanyabiashara,maandamano ya cuf,issue ya ponda,huko polic na mahakama wanajifanya wanajua kweli,ila haya makubwa wako kama nyoka wa morogoro.aibu sana hii nchi.
 
Rugemalila ni mtu ambaye anatakiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria. Nashangaa kwa nini ukawa hawashinikizi hilo. Hata kwenye maazimio ya bunge hakukuwa na azimio la kumtaka Rugemalila kuwajibishwa
Mkuu kwa mtu mwenye akili anajua kabisa kuwa Rugemalira is Innocent, Ametumika tu .Rugemalira hana ubavu wa kugawa pesa kama njugu kwa Viongozi wa serikali, Tetea ukijua kuwa kuna siku utatoa hesabu yake.
 
Inawezekana sana kuwa Ikulu imehusika 100% ... Ila JK kama JK nitakuwa wa Mwisho kuamini kuwa alihusika moja kwa moja! Mamlaka aliyokuwa nayo Rais wa Nchi hii makubwa mmno kiasi cha yeye kuweza kuamuru kupewa matofali ya dhahabu kutoka kwa Wakwapuaji wa ndani na nje kama alivyokuwa akifanya Mkapa! ...
 
Posted by: Saed Kubenea

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Saed Kubenea anaandika…(endelea)

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

hakuna ulichobakisha hapo swadakta.
 
- Mara anasema kwa uhakika mara ameambiwa mara taarifa zinasema, zile zile habari za kawaida za Kubenea toka alipoamua kujiunga na kundi linalomchukia Rais kazi kuandika uchonganishi na uzushi kama huu wa kitoto kabisa ila kwa vile kuna wanaoamini wanaweza kutumia uzushi huu kushika Ikulu basi ngoja wajipe moyo, hii habari ni ya kupikwa pikwa ndio maana haina uhakika mkajipange tena!!

Le Mutuz

Yaani unajitoha ufahamu kwa makusudi, yule mnufaika Albert Marwa aliyemuoa Salam Kikwete aliyetajwa bungeni sio sehemu ya familia yake, Je huyo katibu wake siye mhusika katika taasisi yake ya Urais? Jaribu kukuza kichwa sio kuparamia thread ambazo tunaziamini zizidi kutupa ukweli wa pesa zilizopotea Stanbic kwa kubebwa na lumbesa
 
- Habari imeandikwa na Saeed Kubena kwa niaba ya nani? hahahahahahaha

Le Mutuz

Kwa niaba ya watanzania masikini na wanyonge wanaolipa kodi na kuwanufaisha watu wachache kwenye taifa hili ambao wanajilimbikizia mali na bado haitoshi kwa kuhofia maisha ya huko mbele na mali zao wanawaingiza watoto wao kwenye mamlaka za serikali na uongozi wa taifa ili baadae waje kuwa watetezi wao.
The end is near.
 
marando is somebody more than your father mother and you chap.alafu uoni hata aibu how dare you compare your self with marando!!hata huyo raisi wako unaemlamba viatu hamfikiii marado.
au kwa kuwa marando sio pfofesa wa kichina
?
Kwani marando anakitu gani cha maana kwenye hii jamii zaidi ya kuomba rushwa kwa matajiri na kutoa matamko ya kitoto.

kila siku wale tunaomfahamu marando kwanza hatumuweki hata kwenye kundi la watu wenye upeo wa kutafakari mambo.

Wewe unayedhani kuwa marando anaupeo wa maana pole sana umepotea tena unakwenda kwenye kiza kinene.
 
Wakili kama marando anaitwa ana upeo Mdogo.
Hivi hawa watanzania wenye division five sijui huwa unawatukana tusi gani
 
Back
Top Bottom