Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,228
Watanzania hamjiamini ndio sababu mnaipinga rwanda hata kwa mazuri yake,sasa nikuulize nilini mikataba ya EAC ilikua implemented kama ilivyo sasahivi? na jiulize kwanini sasa hivi EAC inapigwa na mataifa ya ulaya na amerika,jiulize wanaogopa nini?ndugu yangu ukiona wazungu na watu wengine wakitamani kuona EAC inakufa ujue wameishaona kwamba itakua tishio kwao mbeleni kiuchumi na kiulinzi,sasa wewe kalia majungu wao wameisha ona mbele na wameona faida iliyomo katika ushirikiano.
Heshima yako Mukamantare, unajua sana kujieleza hata kiswahili unanishinda; baadhi ya points zako zina-substance - labda nikukumbushe kitu: Tanzania na watu wake tunajiamini sana - don't U forget that, sisi ni watu wapenda amani, haki, ushirikiano na binadamu wenzetu na mifano tunayo tele ya kulithibitisha hilo - jaribu kudadisi raia yeyote anayeishi katika nchi zilizo katika kanda ya Kusini mwa Africa usikie watakweleza nini kuhusu Taifa letu na Viongozi wake, ukiwambia Watanzania hawajiamini na awapendiushirikiano watakushangaa sana!!
Majority ya Wanyarwanda including wewe hatuna matatizo nao, baadhi yao wana undugu wa damu na baadhi ya Watanzania - wengine tumewahi kufundishwa na baadhi ya Mawaziri ambao wapo kwenye Serikali ya Rwanda, sisi tunao msema sema sana PK sio kwamba tuna chuki binafsi dhidi yake kama binadamu, tusicho penda sisi ni matendo hatarishi/reckless yanayo fanywa na REGIME yake OVERTLY au COVERTLY ndani na nje ya Taifa lake analoliongoza, kibaya zaidi badala ya kujirudi anaokena kuwa carried away na adventure zake, sasa kundi kama hilo ambalo liko highly unpredictable unaweza kujua kesho wanaweza ku-spring up surprise gani kwa majirani zake ambao anahisi wanamuwekea kiwingu katika Grandiose Plans zake za operation "BABAROSA au SEALION" akishirikiana na ma fourstar Generals wenzake?? Hapa naleta utani lakini raia wanao toka mipakani hawataki tena kuendelea kusikia majirani zao wakilia "NDAFUYE NDAWELEYE"
Labda nimalizie kwa kusema Watanzania hatuhitaji somo kuhusu mazuri na mabaya katika ushirikiano ndani ya EAC - we've been there before na tunajua vizuri mazuri na machungu yake, actually sisi kama nchi we paid a high price kwa kuvunijka kwake - so "once bitten twice shy" we learnt our lesson the hardway, hivyo hatuwezi tena kukurupukia mambo na kujikuta tuna-jump kwenye bandwagon ambalo navigator,dreva na injinia - oh yes all three rolled in one anakuwa ni mtu mmoja tu, one "PK".
PK akumbuke kwamba 4 the time being nchi yake ni kama an invited guest na ajaribu ku-behave kistaarabu, amuhige Nkuruzinza ,awaheshimu members wahanzilishi wa EAC, asihingize/lete Military Mentality uraiani akifikiri anaweza ku bulldoze members wenzake na kuwasema vibaya members wengine ambao kwa mawazo yake anawaona ni kikwazo kwa malengo yake ya siri.
Mukamantare nimalizie kwa kusema unanishangaza sana, una maana gani unaposema mikataba ya EAC haijawahi kuwa implemented kikamilifu kwa kuwa members wahanzilishi ni wavivu wa kufikiri, MukamaSIMBA bwana!! - Yaani unataka kueleza wana JF kwamba EAC imeshamiri baada ya Mtume na Nabii PK kuingilia kati?? Mukamantare kasahau kwamba EAC iliwahi kuwa na vitego vya HABOURS, RAILWAYS, POST&TELCOMS, CUSTOMS, MARINE vitengo vyote hivyo vilikuwa vinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, tuliwahi vile vile kutumia CURRENCY moja.
Sasa hapo Rwanda inaweza kupendekeza kitu gani kipya ambacho hakijawahi kuwa implemented na former member Countries? Mnacho fanya nyinyi ni kutaka ku-reinvent the wheel i.e mnataka muonekane "HAMVUMI LAKINI MMO" hamna jipya hapo ndugu yangu MUKAMANTARE - ukisema Rwanda imefanikisha kuondoa viza za kwenda kuangalia Sokwe na Ngedele wa Rwanda na Uganda hilo ntakubaliana nawe.