Fitina gani mkuu? si unasema kagame yuko sahihi na ni bora kuliko rais wako? au unapokuwa unaandika huwa unakuwa umekunya viroba/burudani? na washabiki wako ni akina mukamasimba na murutongore ambao wenyewe wanamsifu rais wao.
Wewe siku zote ni kuiponda serikali ya kibongo.
Nitake radhi mkuu. Sijawahi kuiponda serikali yangu. Nikiwa mwanachama hai wa CCM I take offense. Ukisoma post zangu nyingi ni kumsifu Rais JK kwa mazuri anayofanya, hili halina ubishi.Msimamo wangu kuhusu suala la Rwanda unatokana na ukweli usiopingika kuwa Rais Kagame ana haki ya kuilinda na kuitetea nchi yake bila ya bugudha kutoka kwa majirani. Ushauri alioutoa Rais JK kwa Rwanda haukuwa sahihi kwani kuna mengi yamejificha nyuma yake ama kwa kujua au kwa kutokujua. Mfano, kuna "madai" kuwa waasi wa FDLR wanapata misaada na kubebwa na Tanzania ikiwa ni pamoja na logistics na silaha. Sasa kama Rais analijua au halijui hili sifahamu. Ila kwa ushauri wangu, Rais JK angehakikisha kwanza hakuna watu ndani ya utawala wake wanaoipaka matope administration yake kwa kushirikiana na wauaji wa FDLR kabla hajamshauri Kagame aongee na waasi wa FDLR. Lakini vile vile, ushauri si shurti. Rais Kagame ana haki ya ku-react anyway he pleases ikija suala la usalama wa nchi yake. Sioni hatia juu yangu na wala sioni ni vipi nimeudhihaki u-Tanzania wangu kwa kuhoji masuala ya msingi. Hizi tabia za kusifia sifia kila lisemwalo na viongozi ni la ki-imla huko North Korea, Iran etc.