Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Very 'interesting' observation...'interesting' indeed....
Kwanza nisahihishe neno moja ....wajihudhuru.......>>>>>>>>>>>>wajiuzulu

Ikiwa mtu unataka kufanya analysis kwa jambo ni vema uwe sober na objective....usitangulize hisia zako mbele kwani hisia hizo zitakupofusha katika uchambuzi wako...Hilo la kusema eti 'mawaziri wanakosa ile hali ya kujiamini' ni hisia zako wewe.....Aidha kwamba eti Nape 'anawasilisha malalamiko ya Braza la Mawaziri' ni hisia na pia matamanio yako ukiombea hali iwe hivyo...

Ukweli ni kuwa ukitaka kuchambua suala la Mhe. Nape ni kuangalia taratibu, kanuni na utendaji wa Baraza la Mawaziri ...ukifanya hivyo utagundua kuwa Mhe. Nape alitenda kosa la insubordination (au dharau mbaya) kwa bosi wake ambaye ni Rais...

Kama Rais ametamka kuwa wewe 'Makonda chapa kazi', Nape hakuwa na sababu tena ya kuendelea na kamati ile 'uchwara'...natumia neon 'uchwara' kwa kuwa kamati ile in the first place haikustahili iwepo...

Kamati ile imeteuliwa na Waziri kuchunguza issue ya Mkuu wa mkoa....utaona kabisa kuwa kuna walakini hapa....Ninavyoelewa mimi mabosi wa wakuu wa mikoa ni Rais na Waziri Mkuu na siyo mtu mwingine....Kwa maoni yangu hao ndio wanaopaswa kuunda kamati...Halafu wajumbe wa kamati ni lazima wawe na nyadhifa nzito wakiwemo majaji na hata makamishna wa polisi na wengineo wazito na siyo waandishi wa habari wenye 'maslahi' na suala lenyewe....kamati ni lazima iwe huru.

Kamati 'uchwara' ya Nape ilihusisha wengi wa waandisi wa habari wa print media, je wakati suala lenyewe linahusu televisheni....hii ni kasoro nyingine ya kamati hiyo 'uchwara'...

Jambo jingine Mhe. Nape hata hiyo kamati 'uchwara' haijatoa taarifa yeye alishasema kuwa Mhe. Makonda amenajisi tasnia ya habari...maana yake ni kuwa tayari ameingilia kazi za kamati hiyo aliyoiunda mwenyewe...
Jambo jingine ni namna waandishi wa habari wenyewe walivyokosa weledi kwa kutanguliza kuwa mhe. Makonda 'alivamia' Clouds bila hata ripoti ya kamati haijatolewa...

Aidha hakukuwa na sababu yoyote kutoa taarifa ya upande mmoja bila kumhoji mtuhumiwa ambaye ni Mhe. Makonda....
Kwamba Mhe. Makonda 'hakuhojiwa' na kamati hiyo 'uchwara' ni jambo lililotarajiwa na wajuzi wa mambo...Mhe. Makonda asingeweza kukubali 'kuhojiwa' na kamati hiyo isiyo na kichwa wala miguu.

Suala hili la Mhe. Makonda na Clouds limejaa ushabiki zaidi kuliko uhalisia...uko ushabiki wa kisiasa, ushabiki wa chuki kutoka makundi mbalimbali na pia njama...

Mtu hahitaji kuwa mjuzi wa mambo kutambua kuwa yapo makundi mbalimbali yenye njama dhidi ya Mhe. Makonda....namna suala hili lilivyochukuliwa inadhihirisha kuwepo kwa njama hizo...

Makonda anaweza kuwa ana makosa kwenda clouds na kuingia studio, lakini namna wabaya wake walivyolishupalia jambo hili wamekosa 'weledi' wa kuandaa njama....

Kinachojitokeza ni kuwa makundi ambayo ni wabaya wa Mhe. Makonda wanafanya shinikizo kwa Rais ili amuondoe Makonda....Kiongozi mzuri hawezi kukubaliana na shinikizo la aina hiyo....

Mhe. Makonda anaweza akaondolewa Dar es Salaam lakini siyo katika kipindi hiki, anaweza kuondolewa 'wakati muafaka' siyo sasa...

Wako wanaosema kuwa Nape ni shujaa...binafsi sioni hivyo....Mhe. Nape alifanya insubordination kwa Rais kwa hiyo kutumbuliwa kwake ni halali....huwezi kwenda kinyume na Rais halafu ukaachwa...

Na katika historia ya nchi hii hakuna Waziri ambaye ameondolewa madarakani aliyewahi kujaribu kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kuelezea kuondolewa kwake kwenye Baraza la Mawaziri kama alivyofanya Mhe. Nape....Hili nalo ni tukio la aina yake, na inaonesha kwamba Mhe. Nape bado hajaiva sawasawa kiutendaji na kisiasa.
Pamoja na maelezo yako marefu, hebu tusaidie majibu ya maswali haya machache:
1. Nape ni mara ya kwanza ameteuliwa kuwa waziri. Amekuwa na uzoefu wa mwaka na ushee kabla ya kufikwa na kilichomfika. Kama kulikuwa na tatizo (kiutendaji) katika ku handle suala la Makonda kulikuwa na ulazima wa Rais kumwondoa wakati msimamo wake Rais katika suala hilo aliuonyesha wakati tayari Nape ameishaunda hiyo kamati na iko field?

2. Katika mazingira haya, ni nani alipaswa kumpigia simu mwenzake katika hili; mkuu wa nchi au Nape?

3. Pamoja na kwamba haijathibitishwa kimahakama, lakini watu wengi wanakichukulia kile kitendo cha Makonda aka Bashite kuvamia Clouds kwa mujibu wa sheria ya matangazo ya kielektroniki kuwa ni kosa la jinai. Kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho cha Bashite kilikuwa kimeongeza kosa jingine la kijinai kudaiwa kutendwa na mteule huyo wa Rais, hatua zilizochukuliwa na Nape zilikuwa na faida au athari gani kwa serikali inayotokana na watu? Je, haiwezi kuwa kwamba motive behind kwa Nape ilikuwa ni kuihami serikali dhidi ya mtazamo hasi kutoka kwa wananchi?

4.Nape alipofika Clouds ni kweli alitamka kuwa kama kweli kile kitendo kimefanyika kama ilivyoelezwa na Ruge basi itakuwa ni kunajisi uhuru wa habari. Swali linaweza kuwa kama kauli hii ya Nape ni mbaya mno kustahili kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, unamaanisha mtazamo wa mteule wake ni kinyume cha kauli hiyo ya Nape? Na kama ni ndiyo wewe pia unakubaliana hivyo kwamba kuvamia na mabunduki studio kwa lengo la kushinikiza kurushwa kwa habari yako ya kuchafua mtu sio kunajisi uhuru wa habari?

5. Unadai ile kamati ilikuwa ni "uchwara" kwa kuwa ilihusisha wajumbe wengi ambao wako katika "print media". Hoja hii nimeona imeletwa pia na msemaji wa Yanga. Labda utusaidie, mtu anayesoma shahada ya kwanza, hata stashahada ya uandishi wa habari hasomi "broadcasting"? Kwa mujibu wa "hadidu" rejea kuu ya kamati iliyoundwa na Nape, kamati ilitakiwa kupata maelezo ya upande wa pili; hapa unataka kutuaminisha wahariri wa aina ya Balile, Jesse Kwayu na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo wasingeweza kutimiza hilo kwa uweledi?

6. Swali hili liwe la mwisho japo yako mengi. Ni swali la mwisho lakini lina uzito wa kipekee kwa kuwa naona hoja iliyo katika swali hili mmekuwa mkii expose sana. Umedai kuwa kuna watu wabaya wa Makonda aka Bashite wanafanya shinikizo ili Rais amwondoe. Na unadai kuwa watu hao "wabaya" wanatumia makosa yaliyofanywa na Makonda (ni bahati nzuri wewe mwenyewe unakiri kuwa ni makosa) kumshinikiza Rais amtumbue lakini unasema huu sio wakati mwafaka.
Je, ni kwanini unadhani sasa pamoja na kelele hizi zinazopigwa kiasi cha kuharibu kabisa image ya Rais na taasisi yenyewe ya urais, sio wakati mwafaka kwa Rais kuchukua hatua ili kulinda heshima yake mwenyewe, taasisi ya urais pamoja na thamani ya kura ambazo watu walimpigia?
 
Uko wrong,somehow,kama ifuatavyo.

Yeye angekuwa smart ni kwamba alipoona rais kisha toa msimamo wake.na rais ndiye mwenye dhamana ya juu kikatiba iliyopo.
Na Nape kama dhamira yake ilikuwa ya kweli kwa maslahi ya taifa,kama alivyodai ni dhahiri angerudi ofisini akaita press conference na kutangaza kutokuunga mkono maamuzi yale na kwa hiyo dhamira yake imemsuta na anaamua kuachia ngazi kwa maslahi ya kutetea ukweli.
Na kama anabaki kuwa mtiifu kwa chama chake au la hiyo pia ingekuwa ni fursa yake kuueleza umma,tena kwa utulivu bila jazba na hata wazee ndani ya chama wangemuelewa vizuri.

Baada ya hapo angekwenda ikulu kukabidhi barua ya kujiuzuru na akakaa kutafakari mwenyewe kulingana na matakwa yake.

Hapo angekuwa amelamba 100%

Lakini yeye kaendeleza ligi tangia mwanzo kwa wema sepetu hadi mwisho hotelini kwa mbowe protea hotel ile ndugu ya hotel ingine kama hiyo protea aishi hotel/machame moshi.
What did you expect [emoji95]?

The president rhetorically encouraged the RC to carry on with his duties despite of the 'udaku' being circulated in the social media. Wakati huo (siku hiyo) mh. Nape alikuwa ameisha kemea kitendo cha kuvamia TV station akisema tasnia ya habari imenajisiwa. Chukulia jambo hili with a mind that what would you expect from the president ambaye anaonyesha wazi wazi kumkingia kifua mtu ambaye ana undisputed tuhuma dhidi yake kwamba ametumia vyeti vya mtu mwingine kufika hapo alipo, kutuhumiwa kuwa na mali nyingi kuliko kipato chake na mbaya zaidi anaonekana kuendesha gari ya kifahari aina ya BMW X6 yenye usajili wa mmoja wa watuhumiwa wa kufanya biashara ya kulevya. Ni rais huyu huyu aliyesema kama mtumishi wa umma anajijua anatumia cheti cha kughushu au cha mtu mwingine ajiondoe mwenyewe kabla hajafikiwa, sasa mmoja anaye sebuleni kwake.... maajabu matupu.

Masaa kumi na mbili kabla ya kutumbuliwa Nape aliandika kwenye twitter page yake kwamba 'no longer at ease', kwa hiyo alijua na alikuwa tayari badala ya kwenda kulamba viatu.
Kwangu mimi kwa kitendo chake namwona ni shujaa, aliongea maneno mazuri kwamba 'there is nothing to fear than FEAR itself'. Vijana jipangeni taifa hili mnalo miaka zaidi ya 60 ijayo. Just imagine your country with a president like Bashite....
 
Hoja nzuri kaka, lakini ukimsoma Nape kwa makini ni kana kwamba alikuwa anawasilisha malalamiko ya Baraza la Mawaziri, ni kama inaonyesha Mawaziri wengi hawako happy na jinsi Raisi anavyoendesha nchi, sio kwa issue ya Makonda pekee bali pia kwenye maamuzi mbalimbali, yaani Mawaziri wanakosa ile hali ya kujiamini, issue ya Makonda kuendesha zoezi la Madawa ya kulevya bila kumshirikisha Waziri mwenye dhamana ni tatizo kubwa
Nape amekuwa kama Kondoo wa kafara na sababu kubwa ni kuwa Nnape sio mwoga hivyo aliamua kupambana na Magufuli kupitia vituko vya Makonda
Shida kubwa iko kwa mawaziri wenzie, je watamuunga mkono nao wajihudhuru? Ili kuonyesha hawakubaliani na jinsi Raisi anavyoendesha nchi
Unawakilisha malalamiko ya baraza nje ya baraza huko ni kukiuka kiapo njia nzuri ilikuwa kujiuzulu mzee
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box

Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa

Nape alipaswa kujua kuwa alishachafuka toka kwenye issue ya madawa...

1. Kimsingi alikuwa na haki ya kutetea wasanii akiwa kama waziri mwenye dhamana ila hakutumia busara kujibizana na RC kwenye media, wao kama wateule wa rais walipaswa kujifunguia ndani ndio waje na consensus.

2. Nape pamoja na Mwigulu kutajwa kwenye audio ya Steve Nyerere kuwa ndio watu waliotegemewa kumuokoa Wema kwenye scandal/tuhuma ya madawa kiutawala na kiselikali haileti picha nzuri. Rais kama kiongozi na binadamu wa kawaida hilo lazma limpe mashaka juu ya amteule wake..Kama Nape na Mwigulu wana pawa ya kumtoa Wema kwenye tuhuma za madawa watashindwa kumtoa rais madarakani???..Na hakuna rais atakaye kaa bila kujiuliza hili swali..

3. Hivyo tunapaswa kujua Nape na Mwigulu walishaanza kuchafuka..Na nina uhakika kimya kingi cha Mwigulu ni kwasababu alishajua kosa lake na alishajua Steve Nyerere amewakaanga kwa mafuta yao wenyewe.

4. Makonda kuvamia clouds..Kimsingi mpaka sasa nakubaliana na hoja kuwa RC alitenda kosa kuvamia clouds ukizingatia RC mwenyewe hajatoa sababu zake za kwanini alifanya hilo tukio.
Tatizo langu ni jinsi Nape alivyolihandle hilo tatizo..na kwakutaka kumkomoa RC. How comes, waziri unatoa judgment kuwa RC amekosea hapo hapo unaorganise wabunge na watu mbalimbali kutembelea media tena unatangaza ukishindwa hilo utajiuzuru alafu baadae ndio unatangaza kuunda tume?..

That was not right, waziri alikuwa tayari ameshaipa tume yake direction ya nini cha kuandika ili kumchochea rais kumcrucify RC na kama rais angekataa yeye angejiuzuru ili kumtia aibu rais..
Kwa mtu mwenye kariba ya Magufuli na hata ningekuwa mimi nisingekubali kuchochewa kizembe na Nape.
 
The president rhetorically encouraged the RC to carry on with his duties despite of the 'udaku' being circulated in the social media. Wakati huo (siku hiyo) mh. Nape alikuwa ameisha kemea kitendo cha kuvamia TV station akisema tasnia ya habari imenajisiwa. Chukulia jambo hili with a mind that what would you expect from the president ambaye anaonyesha wazi wazi kumkingia kifua mtu ambaye ana undisputed tuhuma dhidi yake kwamba ametumia vyeti vya mtu mwingine kufika hapo alipo, kutuhumiwa kuwa na mali nyingi kuliko kipato chake na mbaya zaidi anaonekana kuendesha gari ya kifahari aina ya BMW X6 yenye usajili wa mmoja wa watuhumiwa wa kufanya biashara ya kulevya. Ni rais huyu huyu aliyesema kama mtumishi wa umma anajijua anatumia cheti cha kughushu au cha mtu mwingine ajiondoe mwenyewe kabla hajafikiwa, sasa mmoja anaye sebuleni kwake.... maajabu matupu.

Masaa kumi na mbili kabla ya kutumbuliwa Nape aliandika kwenye twitter page yake kwamba 'no longer at ease', kwa hiyo alijua na alikuwa tayari badala ya kwenda kulamba viatu.
Kwangu mimi kwa kitendo chake namwona ni shujaa, aliongea maneno mazuri kwamba 'there is nothing to fear than FEAR itself'. Vijana jipangeni taifa hili mnalo miaka zaidi ya 60 ijayo. Just imagine your country with a president like Bashite....

Ni kweli Nape alijua it was No longer at ease..But not 12 hours before. Alijua toka siku ile Steve Nyerere alipomtaja kwenye simu yake akiongea na mama wema na hiyo audio ikaenda viral..
 
Protokali za kishenzi na kipuuzi hizo...msitumia hizo protokali kuficha madhaifu...tatizo ni kuishi kwa unafiki.

Ndiyo maana mtu mzima na PhD yake, anaonyeshwa yeye hafai, lakini bado analamba miguu ya mtu aliyem-devalue na kumwonyesha hafai!!

Ati mkubwa wake? Kwani mkubwa hakosei? Yeye ni nani? Mungu
? Acheni hizo nyinyi. I never liked Nape, and I will never like him, but, I support what he did. Nape alisimamia kutekeleza majukumu yake. Sema, alikose kitu kimoja, alipaswa ajiuzulu baada tu ya rais kuongea zile pumba pale Ubungo. Hapo ningempa heshima zaidi. Siyo kama alivyofanya, ingawa kapata heshima yangu kiduchu.
Hiyo sio mimi mkuu hata mie sijapendezwa na Rais alivyofanya siku ile ya uzinduzi lakini pia the same nimeunga mkono hoja kile alichofanya Nape ila tatizo ndio hivyo serikali zetu zinavyofanya kazi mkuu yaani tamko likitolewa na mamlaka za juu maana yake wa chini hata kama analipinga so long yeye ni sehemu ya serikali anatakiwa alipotezee na vivyo hivyo na mamlaka ya chini (Waziri) akitoa tamko linakuwa halali mpaka hapo litakapokanushwa na mamlaka za juu (rejea tamko la Mwakyembe dhidi ya vyeti vya kuzaliwa likaja kukanushwa na Rais).

Hapo chini uliposema alitakiwa ajiuzulu ndio msingi mkuu wa heshima ya Nape hasa pale Rais alipomsafisha Makonda siku ya uzinduzi maana ripoti ilikuwa bado kutoka ndio ilikuwa nafasi muafaka kuachia ngazi na hii ilimtokea tena Mrema sema yeye alitumbuliwa kabisa Uwaziri kwa kwa kuwa alipinga ndani ya bunge kabisa ambapo Waziri kazi yake ni kutetea hata kama kilichowasilishwa na serikali ni kituko (tatizo wanaapa kulinda na kutetea katiba na serikali hivyo inabadi wakubaliane na madhaifu yaliyopo maana wao ndio walioyapitisha mkuu)

Hii nchi inaongozwa na Marais, Mawaziri, Wakuu wa mikoa na Wilaya na Makatibu tarafa ambao wamepewa mamlaka ya kisheria ya kutoa matamko (hii ndio nchi yetu sio sisi na funzo hapa katiba walioitengeneza wenyewe ndio hiyo hiyo inayowamaliza wenyewe)
 
Nionavyo mimi, Nape na Makonda wana "mambo yao" binafsi yaliyokuwa nje ya kazi zao za Serikali. Mh. Makonda alivyoanzisha sekeseke la ngada na kuwahusisha watu wa karibu na Nape kama Wema ilibidi Nape atoke kuwatetea "wadogo" zake kwa kauli kali sana za kuua brand za watu. Baada ya nape kutoka hadharni, tukaona vijembe kutoka kwa kila upande. Hawa watu wakawa wanatumia ofisi zao kuwindanda. Nape akaona ndiyo muda mwafanya pa kumpiga Makonda panapouma kupitia issue ya Clouds. Rejea, alivyotembelea Clouds "kuwapa pole" na kuunda "kamati" haraka haraka iliyojaa wapinzani wa Makonda. dots ni nyingi sana ...................................... tuendelee kuangalia movie baada ya stering moja kujeruhiwa vibaya sana. Je, "timu " yake itakubali kirahisi hivyo? Nipeni gahawa ninywe.
WEWE UMEELEWA VIZURI SAAANA..Umekula A+
 
Ruge anatuambia kuwa Makonda ni rafiki yake na mara nyingi anaendaga hapo clouds...sasa sijafahamu RC huwa anaendaga peke yake bila walinzi au hata mchana wa hiyo siku RC hakuwa na walinzi wenye bunduki mpaka tuambiwe ule usiku kuwa makonda ndo kaenda kuvamia,sawa kama kaenda kuvamia na wala sio kama yale matembezi yake mbona hatujaona hata igizo la mfanyakazi yoyote kujeruhiwa.

..yes, rc makonda ni " rafiki " wa clouds.

..na ni kweli clouds wamekiri kwamba rc makonda huwa anawatembelea kazini kwao mara kwa mara.

..nadhani kilichotokea usiku ule kuna kitu rc makonda alikifanya na rafiki zake wa clouds wamechukizwa nacho.

..ushauri wangu ni rc makonda anatakiwa atulie na kuenenda kama
mtu mzima.

..kuna mambo anayafanya yanakiuka maadili ya nafasi yake kama rc. Kwa mfano tukio la kumtukana mtumishi wa serikali.

..Au tukio la kwenda Kanisani na
kuanza kuhutubia masuala ya kiserikali na kuangua kilio.
 
Pamoja na maelezo yako marefu, hebu tusaidie majibu ya maswali haya machache:
1. Nape ni mara ya kwanza ameteuliwa kuwa waziri. Amekuwa na uzoefu wa mwaka na ushee kabla ya kufikwa na kilichomfika. Kama kulikuwa na tatizo (kiutendaji) katika ku handle suala la Makonda kulikuwa na ulazima wa Rais kumwondoa wakati msimamo wake Rais katika suala hilo aliuonyesha wakati tayari Nape ameishaunda hiyo kamati na iko field?

2. Katika mazingira haya, ni nani alipaswa kumpigia simu mwenzake katika hili; mkuu wa nchi au Nape?

3. Pamoja na kwamba haijathibitishwa kimahakama, lakini watu wengi wanakichukulia kile kitendo cha Makonda aka Bashite kuvamia Clouds kwa mujibu wa sheria ya matangazo ya kielektroniki kuwa ni kosa la jinai. Kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho cha Bashite kilikuwa kimeongeza kosa jingine la kijinai kudaiwa kutendwa na mteule huyo wa Rais, hatua zilizochukuliwa na Nape zilikuwa na faida au athari gani kwa serikali inayotokana na watu? Je, haiwezi kuwa kwamba motive behind kwa Nape ilikuwa ni kuihami serikali dhidi ya mtazamo hasi kutoka kwa wananchi?

4.Nape alipofika Clouds ni kweli alitamka kuwa kama kweli kile kitendo kimefanyika kama ilivyoelezwa na Ruge basi itakuwa ni kunajisi uhuru wa habari. Swali linaweza kuwa kama kauli hii ya Nape ni mbaya mno kustahili kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, unamaanisha mtazamo wa mteule wake ni kinyume cha kauli hiyo ya Nape? Na kama ni ndiyo wewe pia unakubaliana hivyo kwamba kuvamia na mabunduki studio kwa lengo la kushinikiza kurushwa kwa habari yako ya kuchafua mtu sio kunajisi uhuru wa habari?

5. Unadai ile kamati ilikuwa ni "uchwara" kwa kuwa ilihusisha wajumbe wengi ambao wako katika "print media". Hoja hii nimeona imeletwa pia na msemaji wa Yanga. Labda utusaidie, mtu anayesoma shahada ya kwanza, hata stashahada ya uandishi wa habari hasomi "broadcasting"? Kwa mujibu wa "hadidu" rejea kuu ya kamati iliyoundwa na Nape, kamati ilitakiwa kupata maelezo ya upande wa pili; hapa unataka kutuaminisha wahariri wa aina ya Balile, Jesse Kwayu na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo wasingeweza kutimiza hilo kwa uweledi?

6. Swali hili liwe la mwisho japo yako mengi. Ni swali la mwisho lakini lina uzito wa kipekee kwa kuwa naona hoja iliyo katika swali hili mmekuwa mkii expose sana. Umedai kuwa kuna watu wabaya wa Makonda aka Bashite wanafanya shinikizo ili Rais amwondoe. Na unadai kuwa watu hao "wabaya" wanatumia makosa yaliyofanywa na Makonda (ni bahati nzuri wewe mwenyewe unakiri kuwa ni makosa) kumshinikiza Rais amtumbue lakini unasema huu sio wakati mwafaka.
Je, ni kwanini unadhani sasa pamoja na kelele hizi zinazopigwa kiasi cha kuharibu kabisa image ya Rais na taasisi yenyewe ya urais, sio wakati mwafaka kwa Rais kuchukua hatua ili kulinda heshima yake mwenyewe, taasisi ya urais pamoja na thamani ya kura ambazo watu walimpigia?

pole Ndugu yangu....
 
waberoya! unapo post kitu jaribu kutumia upeo kidogo kufikiria, yule ile ni wizara yake na ni miongoni mwa majukum yake kutatua changamoto zote zinazoikabili tasnia ya michezo na sanaa kwa ujumla, kwa iyo ww unafurahia lile tukio lililotokea pale clouds media? na angekaa kimya ili iweje? ionekane kwamba na yeye anasapot ule ujinge? tuwe wazalendo jaman na hii nchi, tusiongee tu kama maneno yanatokea tumbon, baada na ww mwananchi wa kawaida ukemee huu ujinga uliotokea ndio kwanza unamshaur wazir mwenye dhamana akae kimya sasa wale watu wakesemee wapi? kwel wa akina bashite mko wengi

Nape leo amekuwa mzalendo kwasababu ya issue ya clouds??...Miezi miwili nyuma kipindi cha kupitisha Sheria ya huduma za habari, Bunge live na mengineyo ...Nape mlimpa majina gani??? Watanzania sisi ni watu wa hatari saana kuliko hatari yenyewe...Na hakuna media za kipuuzi kama media za tz...Yaani walishindwa kugomea kurusha habari za serikali kipindi cha hayo matukio muhimu kwao leo wanakuja kugomea kurusha HABARI ZA MAENDELEO yoyote as long as mkuu wa mkoa anahusika..ILA ikiwa ni HABARI YA KUMCHAFUA..media zooote zinamuandika front page! This is RUBBISH
 
Mkuu siku anaweka jiwe la msingi ufunguzi flyover alisema Habari Ni Za udaku ndio maana Nape aliendelea Na uchunguzi ili mkuu apewe report ya uchunguzi ambayo sio ya udaku. Hata Meya wa ubungo naye baada ya kuona raisi anahitaji malalamiko officially Na sio ya mitandaoni naye akamua kufungua kesi ili vitu viwe official
 
wewe kwanini unadhani aliamini maneno tu ya kina ruge? ukumbuke alikwenda pale kupata maelezo kamili. ulichoonyeshwa wewe ni cctv footage ya mapokezi tu. ya yaliyotokea ndani hujaonyeshwa. unadhani na yeye nape hakuonyeshwa? yeye kaona na kusikilizishwa mchezo mzima sio kuambiwa mchezo mzima. aliyoyasikia kwenye ripoti hayakua mageni kwake kwa wakati ule basi tu ili taratibu ziwe zimefuatwa. huyo aliyetenda kwanini alikataa kuhojiwa? tena na waziri? sijaona mkenge wowote aliongizwa kama unadhani wewe mkuu. hili suala liko wazi. raisi ana mahaba na bashite hata kama ni kwa gharama ya kuwadhalilisha mawaziri wake. kachukia uchunguzi kufanyika. kwanini? haya leo umemsikia kachukia hata magazeti kuripoti front page tukio la nape kuvamiwa kwa bastola. mambo ya ajabu sana na yako wazi wala haitaji kutafuta consiparacy theories ambazo hazipo
Usitake kudanganya watu. Hakuna kikao cha siri kilichofanyika kati ya Nape na akina Ruge. Nape aliingia clouds tv akiambatana na waandishi wa habari. Kikao kilikuwa wazi kabisa tangia mwanzo hadi mwisho.

Halafu nani alikuambia kuwa mamlaka ya nidhamu ya kazi ya wakuu wa mikoa ni mawaziri? Maana ni mwenye mamlaka ya nidhamu ya mtumishi husika tu ndiye anaweza kuunda kamati ya aina hiyo ya uchunguzi wa huyo mtumishi kwa lengo la kumchukulia hatua kali ya kinidhamu ikiwamo kumfukuza kazi. Na kamati ya aina hiyo hupewa hadidu rejea mahususi kwa kazi hiyo. Kamati ya Nape ilikuwa haina kitu kama hicho isipokuwa kuleta majibu ndani ya saa 24! Wapi na wapi kamati ya aina hiyo iliyowahi kupatiwa muda mfupi namna hiyo. Standing Orders zinatoa muda usiopungua 14 days.

Tatizo la wanasiasa wetu wanadhani wao ndiyo mamlaka ya nidhamu ya kila mtumishi wa umma. Utakuta wanasimamisha au kufukuza kazi watu ili hali wao si mamlaka yao za nidhamu, at the end they backfire kama ilivyotokea kwa Mh. Nape. Kuna madaktari wamefukuzwa kazi na madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya/ mikoa, mawaziri na hata wenyeviti wa mitaa. Ni vurugu. Labda semina elekezi za wanasiasa hawa zilizokuwa zinafanyika Ngurudoto zirejeshwe.
 
Nape alikua waziri wa habari sidhani kama kukaa kimya ilikua ni suluhisho.Maadam rais Magufuli ameamua kumkumbatia Mkuu wa mkoa wa Dar kuliko mtu yeyote, ngoja tuone mwisho wake.Ukweli ni kwamba Makonda na Magufuri wana siri nzito na tutaijua tuu siku wakikorofishana.Maana ulimi hupeleka chakula kwenye meno lakini meno yasivyo na shukrani huwa yanang'ata ulimi wakati fulani.

Hakutakiwa kukaa kimya..coz asingekuwa na mahala pa kuiweka sura yake mbele za media na wasanii..
LAKINI..alipaswa kufanya alilofanya kwa umakini na sio kutumia mihemko ya mifarakano iliyotokea kati yake na RC..
Nimeangalia hotuba ya rais wakati wa kuapisha wateule wapya ameongelea suala la Mawaziri kupenyeza habari kwa media nini cha kuandika...kama una akili nzuri utaconnect the dots na kilichomtokea Nape.
 
waberoya! unapo post kitu jaribu kutumia upeo kidogo kufikiria, yule ile ni wizara yake na ni miongoni mwa majukum yake kutatua changamoto zote zinazoikabili tasnia ya michezo na sanaa kwa ujumla, kwa iyo ww unafurahia lile tukio lililotokea pale clouds media? na angekaa kimya ili iweje? ionekane kwamba na yeye anasapot ule ujinge? tuwe wazalendo jaman na hii nchi, tusiongee tu kama maneno yanatokea tumbon, baada na ww mwananchi wa kawaida ukemee huu ujinga uliotokea ndio kwanza unamshaur wazir mwenye dhamana akae kimya sasa wale watu wakesemee wapi? kwel wa akina bashite mko wengi
Hujaelewa hata hoja yake nawe umejbu yakwako.
 
Umeshauri Nape angefanya ''utumbo'' uliofanya Afrika tubakie kwenye maisha ya kimaskini na duni! Kufanya unafiki! Magufuli alichofanya ni kutetea uhalifu. Nape alichofanya ni ku-expose uhalifu. Magufuli sio Mungu amabaye hakosei kwa kila afanyalo.

SIO KWELI,
Nape ameanza lini kuwa mfichua maovu??
 
Nape angelijua kuna kutumbuliwa asingelisubiri hilo angejiuzulu, Na asingetokwa na povu
Inavyo onekana alikuwa na mengi ila ameya mezea tu. Ukiangalia kwa manufaa yake kisiasa, target inawezekana ilikuwa ni kumuachia mkulu abonyeze button ya mwisho. Na ndio kilicho tokea. Na hicho ndio kimempa credit zaidi. Ila ange jiuzulu mwenyewe ingekuwa ni rahisi kwa mkulu kupata cha kuongea na Nape kusahaulika mapema.
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box

Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa
Rais ana uwezo wa kutoa msamaha kwa yeyote aliehukumiwa kwa jinai mahakamani, kwa hili la Bashite, hata akipatikana na hatia mahakamani Rais anaweza kumpatia msamaha haraka sana, na jaji alietoa hukumu akafukuzwa kazi immediately!
 
Nape alipaswa kujua kuwa alishachafuka toka kwenye issue ya madawa...

1. Kimsingi alikuwa na haki ya kutetea wasanii akiwa kama waziri mwenye dhamana ila hakutumia busara kujibizana na RC kwenye media, wao kama wateule wa rais walipaswa kujifunguia ndani ndio waje na consensus.

2. Nape pamoja na Mwigulu kutajwa kwenye audio ya Steve Nyerere kuwa ndio watu waliotegemewa kumuokoa Wema kwenye scandal/tuhuma ya madawa kiutawala na kiselikali haileti picha nzuri. Rais kama kiongozi na binadamu wa kawaida hilo lazma limpe mashaka juu ya amteule wake..Kama Nape na Mwigulu wana pawa ya kumtoa Wema kwenye tuhuma za madawa watashindwa kumtoa rais madarakani???..Na hakuna rais atakaye kaa bila kujiuliza hili swali..

3. Hivyo tunapaswa kujua Nape na Mwigulu walishaanza kuchafuka..Na nina uhakika kimya kingi cha Mwigulu ni kwasababu alishajua kosa lake na alishajua Steve Nyerere amewakaanga kwa mafuta yao wenyewe.

4. Makonda kuvamia clouds..Kimsingi mpaka sasa nakubaliana na hoja kuwa RC alitenda kosa kuvamia clouds ukizingatia RC mwenyewe hajatoa sababu zake za kwanini alifanya hilo tukio.
Tatizo langu ni jinsi Nape alivyolihandle hilo tatizo..na kwakutaka kumkomoa RC. How comes, waziri unatoa judgment kuwa RC amekosea hapo hapo unaorganise wabunge na watu mbalimbali kutembelea media tena unatangaza ukishindwa hilo utajiuzuru alafu baadae ndio unatangaza kuunda tume?..

That was not right, waziri alikuwa tayari ameshaipa tume yake direction ya nini cha kuandika ili kumchochea rais kumcrucify RC na kama rais angekataa yeye angejiuzuru ili kumtia aibu rais..
Kwa mtu mwenye kariba ya Magufuli na hata ningekuwa mimi nisingekubali kuchochewa kizembe na Nape.

Uko sahihi...kwangu mimi kwa kosa la (makosa ya) Nape...na hata hatua ya kuongea na media kama ningekuwa Rais ningeweza hata kumweka detention kwa muda Fulani ...Waziri huwezi kufanya mashinikizo ya waziwazi kum-undermine Rais....
 
kwa uonavyo wewe nape alikua sahihi au hakua sahihi? kama unaona hakua sahihi basi ulitaka awe mmoja kati ya wenye nidham za woga. tukiwa na watu kama hao katika serikali basi masikini atawasemea nani? kama unaona alikua sahihi unatakiwa kumpongeza kwani watu kama hao ndio huchochea upatikanaji na uheshimiwaji wa haki za raia wanyonge. mchezo mzima unaonekana wazi rais alikua na taarifa kabla ya uvamizi uliokuwa ukienda kutokea clouds media. uvamizi ulikua na baraka zake ule ndio maana kakasirika nape kuufuatilia sasa hilo ni sahihi? mambo mabaya kwa jamii yanapotendeka ni lazima mwenye sauti ayakemee kwa niaba ya wasio na sauti hata kama ni kwa gharama ya kupoteza ugali wake. anatakiwa kupongezwa. mimi sioni kapoteza nini. alichokifanya kilikua ni sehemu ya kelele wanazopiga wananchi juu ya kutendeka kwa haki kwa bashite kufukuzwa kazi kama wanavyofukuzwa wanyonge wengine. alikua akisaidia kupaza sauti zetu

Umetanguliza hisia zako kwenye suala nyeti...Eti "rais alikua na taarifa kabla ya uvamizi...uvamizi ulikuwa na baraka zake..."...these are very strong words na ambayo ukiambiwa u-prove hutaweza...kama wewe ni mtu mzima ujiepushe na kauli za aina hii...Awali ya yote kile kinachoitwa 'uvamizi' kinatiwa chumvi mno ...

Kwa wanaojua utendaji na taratibu za serikali na kanuni zake hapana shaka yoyote ile kwamba Mhe. Nape alikosea mno..Mhe. Nape alifanya kosa la insubordination (dharau mbaya) kwa Rais....Mhe. Nape hana mamlaka ya kuteua Kamati kuchunguza suala linalomhusu Mkuu wa Mkoa...Mabosi wa Mkuu wa mkoa ni Rais na Waziri Mkuu, hao ndio wangeunda kamati na ambayo bila shaka ingekuwa na watu senior katika jamii au serikali kama vile majaji, makamishna wa polisi na wengine ... Kamati ya Nape ilikuwa ni 'Kamati Uchwara'... Pale Rais alipotamka kuwa 'Makonda chapa kazi' ilipaswa uwe ndiyo mwisho wa 'Kamati uchwara'..

Nape siyo shujaa hata kidogo na ni wazi hajaiva kiutendaji na kisiasa...ni jambo baya mno na hasa kwa waziri kufanya jambo linalomshinikiza Rais kufanya maamuzi kinyume na matakwa yake....

Mhe. Makonda anaweza kuwa amefanya kosa na ataondoka 'muda muafaka' ukifika na siyo sasa...
 
Back
Top Bottom