Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Marafiki wa Nape: Kwanini Nape hakutulia?

Hata alivosema kuna kibaya gan jana nape alichoongea hadi muwe na hofu ya namna hiyo? Anataka kutoa shukrani kwa rais na aliofanya nao kazi, Mtu anataka kuongea unamwekea mtutu, kwanza kupewa cheo lazima, kama ameondolewa kwa manufaa ya nji kwa nn azuiwe kusema?

Ni kibaya mkuu, labd kama haujui utendaji wa serikali

kimya ni busara sana, unaweza ukasababisha taharuki ya kitaifa kwa mikutano kama ile

Nape alizidi kukosea, Mtei alipohitilafiana na Nyerere aliondoka mwenyewe! hakufukuzwa
 
Utoto ndio unamsumbua, Magu alitofautiana na JK kipindi fulani, alitaka kuvunja nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara nadhani ni Morogoro road, akazimwa na Pinda na jk,
Akaamua kukaa kimya, mbona kawa Rais wa TZ juzi kati kazipiga chini, tena bila fidia. KUKAA KIMYA NI UUNGWANA PIA,

Ingekuwaje mama Anna kilango angebwabwaje alivyopigwa chini ukuu wa mkoa, mara nyingi watu wazima, na waungwana wanachunga midomo yao.

Kabisa ndugu

Ukimya unaficha mambo mengi na unakukuza sana!! Nape katika hilo kafeli!

Many great leaders huwa sio wepesi wa kufanya maamuzi vipindi vya presha!

Nguvu yake na faraja yake ilikuwa kwa waandishi ambao wengi tunawajua ni waganga njaa tu
 
Hlafu ujue jambo moja. Nape alifanya uchunguzi na kujua ni nini hasa kilichotekea ndipo akatoa maamuzi. Yeye Magufuli alitoa maamuzi bila kufanya uchunguzi na kujua undani wa scandal yenyewe ulikuwaje! Hivyo Nape alitumia nafasi yake kama waziri kumsaidia rais kutekeleza majukumu yake!

Hakumsaidia rais....rais aliposema neno tu pale ubungo alitakiwa awasiliane na bosi wake na kumuuliza kama 'bosi' anahitaji report?

Nape asingeridhika basi alikuwa na hiyari ya kujiuzulu

Nape alijua fika anafanya nini
 
Ni kutofahamu mipaka ya utendaji wake, ni kwa nini hakumpigia simu Rais kwa ajili ya kuomba ushauri kuhusu dhamira yake ya kuunda Tume, yeye anawajibika kwa nani, hiyo taarifa angeipeleka kwa nani kwa ajili ya maamuzi. Hili liliotoke ni kazi ya Mungu ili Nape naye ajionee machungu ambayo wengine wamekwa wakikabiliana nayo na wakati mwingine naye akitoa maelekezo washughulikiwe. Nasikia hata enzi za Mwalimu, mtu aliyechangia katika kupitisha Sheria ya Kuweka watu Kizuizini, aliponea chupu chupu kuwekwa kizuizini, akakimbi nchi.

Hii ni point muhimu sana japo wengine watabisha!

Kuna nchi ambazo rais anaweza pia kuwa waziri wa wizara fulani

Nape amewekwa kumsaidia rais, na yeye Nape hakuwa taasisi inayojitegemea!! anafanya kazi kwa job description ya rais, anauwa monitored na rais, na alipaswa kujua views za rais

Naam, kama angeona kuna mahali haridhiki, angejiuzulu ( tena angetoa sababu) na binafsi ningemwona hero
 
Sasa mtu kwanini usiachie ngazi?

Mapema sana, alipoona anakinzana na mkuu wake, angeondoka tena ingekuwa kishindo

kuondoka kwake kungeleta ushujaa na sio unafiki nafiki ambako alijua kabisa mwisho wa kamati yake na report yake ni rais...akajifanya kipofu
 
Hata Mimi ningekua Nape nisingeweza kuvumilia kitendo kilichofanywa na Paul Makonda hasa ukizingatia suala hilo ni mdau na vyombo vya habari viko chini ya wizara ya habari. Hata kama Rais hakupendezwa Mkuu wa Mkoa ashughulikiwe hii ni binafsi lakini kimsingi Nape amesimamia kazi yake na hajakosea.

Yes, then angejiuzulu mapema sana, maana kulikuwa hamna namna ya yeye kuendelea kuwemo wakati moves zake zilikuwa nje ya bosi wake
 
Nape alianza kushughulikia na kutoa maaumuzi kwenye hilo swala kabla ya hotuba ya raisi kuhusu swala hilo hilo, ulitaka afanyeje wakati a;isha tuma tume?
Yeye mwenyewe ukifuatlia twits zake alijua nini kinafuata kwa hiyo hakuna la ajabu, atakuwa alijiandaa.

Kwani report angeipeleka kwa nani mkuu?? si kwa rais??

Then maamuzi ya Magufuli unavyoona wewe yangebadilika?
 
Huyu ni kiongozi mkubwa katika nchi na amepitia katika kipindi cha presha

Kwa nini hakutulia??? au kulikuwa na ulazima wa yeye kusema kitu? what if kama Magufuli alikuwa anataka ampe nafasi ingine ya serikalini?

Nyuma ya pazia kuna nini ambacho Nape anahisi kachukiwa sana wakati kitu alichofanya is obvious ilikuwa lazima ajiuzulu yeye , bila hata kuondolewa. Hakukuwa na haja ya Kamati wakati mwisho wa matokeo ya kamati ni kupeleka report kwa Rais ambaye aliishaamua na kusema pale ubungo

Naamini rais sio malaika, wala sio kuwa Nape hana namba ya simu ya Magu kiasi ambacho wangeongea kuhusu hili swala na kupata baraka zake, kufanya jambo kama lile au kuendelea nalo likiwa linakinzana na bosi wako lina maana gani?? (tuache mihemko wengi tuna mabosi hapa)

Namna ya kudeal na lile swala ilikuwa lazima kuwe na kamati? au angebadili methodology? what was the mission behind? tuwaze nje ya box


Nape inaonekana alijua anafanya nini, na alijua outcome ya mission ilikuwa aidha

1. Rais awe kwenye wakati mgumu wa maamuzi
2. au Nape aondoke yeye

mkuu kamuwahi

ila siamini kama kwa level ya Nape hakujua kuwa kuna kitu kinaendelea..(?????) Yes unaweza kuwa hero, unaweza kuwa na malengo mema na mazuri kabisa ( kutimiza wajibu wako) ila kufanikisha kazi yako kwa ufanisi kunahitaji akili pia na approach kufikia lengo

mimi mtu wa chini niliona kabisa Nape anakinzana na rais, yeye hakuona? au yeye anafanya kazi kama msaidizi wa nani? kama sio msaidizi wa rais....naona Logic inagoma kuona kama Nape alikuwa yeye kama yeye na hana affiliation na Magufuli ambaye ni bosi wake

Imani yangu na msimamo wangu, Makonda ataondoka kupitia mahakama kwa sasa, kuvamia clouds was the best opportunity ya kumuweka kwenye majengo ya mahakama....ingemlazimisha rais kumuondoa
kwa uonavyo wewe nape alikua sahihi au hakua sahihi? kama unaona hakua sahihi basi ulitaka awe mmoja kati ya wenye nidham za woga. tukiwa na watu kama hao katika serikali basi masikini atawasemea nani? kama unaona alikua sahihi unatakiwa kumpongeza kwani watu kama hao ndio huchochea upatikanaji na uheshimiwaji wa haki za raia wanyonge. mchezo mzima unaonekana wazi rais alikua na taarifa kabla ya uvamizi uliokuwa ukienda kutokea clouds media. uvamizi ulikua na baraka zake ule ndio maana kakasirika nape kuufuatilia sasa hilo ni sahihi? mambo mabaya kwa jamii yanapotendeka ni lazima mwenye sauti ayakemee kwa niaba ya wasio na sauti hata kama ni kwa gharama ya kupoteza ugali wake. anatakiwa kupongezwa. mimi sioni kapoteza nini. alichokifanya kilikua ni sehemu ya kelele wanazopiga wananchi juu ya kutendeka kwa haki kwa bashite kufukuzwa kazi kama wanavyofukuzwa wanyonge wengine. alikua akisaidia kupaza sauti zetu
 
HARAKA YOTE ILIKUWA YA NINI HASA KUNA MTU ALIUAWA PALE AU KUNA MALI ILIPOTEA MPAKA KAMATI IPEWE SAA 24 KWA LIPI HASA?
TUSIPELEKWE NA MIHEMUKO NA JAZBA TUKASAHAU UKWELI NI KWAMBA NAPE ALIKUWA NA CHUKI NA MAKONDA KUANZIA KWENYE SUALA LA MADAWA ALIANZA KUMLAUMU HADHARANI KWAMBA ANAFANYA MAKOSA JAMBO AMBALO KIUTENDAJI SERIKALINI HALITAKIWI, LAKINI BADO NAPE ALITHIBITISHA PASIPO SHAKA KWAMBA ANATAKA MAKONDA AHARIBIKIWE KAMA ANGELIKUWA NA NIA KWELI YA KUTETEA WAAANDISHI WA HABARI KAMA ALIVYOJINADI ANGEANZA NA YULE DC ALIYEMUWEKA MAHABUSU MWANDISHI WA HABARI WA ITV IWEJE LEO MAKONDA KWENDA STUDIO IMEKUWA NONGWA MPAKA AUNDIWE TUME YA KUFANYA KAZI MASAA 24 IWE IMETOA REPORT??? HAPO MWENYE AKILI NA AELEWE HUU WEMA WA NAPE KWA WAANDISHI WA HABARI UMEANZA LINI WAKATI NI YEYE HUYOHUYO AMESIMAMIA MAGAZETI KADHAA KUFUNGIWA NA BUNGE LIVE KUONDOLEWA ?? UKWELI NI KWAMBA WAUZA MADAWA WALIMTUMIA NAPE VILIVYO NA AKATAKA KUTUHADAA KWAMBA ANATETEA WAANDISHI WA HABARI NI UWONGO WA WAZI AKADANGANYE WAJINGA WENZIE. MAKONDA NI KWELI HAKUWA SAHIHI LAKINI NGUVU KUBWA ILIYOTUMIWA NA WAZIRI INADHIHIRISHA WAZI KABISA NAPE HAKUWA NA NIA NJEMA KWA MAKONDA SASA KIBAO KIMEMGEUKIA YEYE MWENYEWE NA ANAVUNA ALICHOPANDA.
Hata Makonda hatuwezi kusema hakuwa sahihi maana Nape hakutaka kupata maelezo yake confidentiality kwanza. Maana inaweza ikawa kilichofanyika hakikupaswa kuwa open. Sasa Nape kaunda kamati ya wazi imhoji Makonda, sasa ataanikaje siri ya serikali? Kwa nini Nape aliamini maelezo ya akina Ruge kwamba Makonda alifuata footage ya hawara wa Gwajima? Jee hawezi kuwa Makonda alifuata mzigo wa unga pale baada ya kupata mtonyo from the security apparatus ama masuala mengine nyeti na wakina Ruge kujihami kwa kusambaza picha za cctv zao kwamba wamevamiwa? Nape kaingizwa mkenge kjlaini na wajanja wakina Ruge. Uwezekano ni mkubwa the man behind all this ni Gwajima, mtu mwenye ukwasi mkubwa anayeshukiwa kuwa drug dealer ambaye ana ugomvi na Makonda baada ya kutajwa na Makonda.
 
Hata Makonda hatuwezi kusema hakuwa sahihi maana Nape hakutaka kupata maelezo yake confidentiality kwanza. Maana inaweza ikawa kilichofanyika hakikupaswa kuwa open. Sasa Nape kaunda kamati ya wazi imhoji Makonda, sasa ataanikaje siri ya serikali? Kwa nini Nape aliamini maelezo ya akina Ruge kwamba Makonda alifuata footage ya hawara wa Gwajima? Jee hawezi kuwa Makonda alifuata mzigo wa unga pale baada ya kupata mtonyo from the security apparatus ama masuala mengine nyeti na wakina Ruge kujihami kwa kusambaza picha za cctv zao kwamba wamevamiwa? Nape kaingizwa mkenge kjlaini na wajanja wakina Ruge. Uwezekano ni mkubwa the man behind all this ni Gwajima, mtu mwenye ukwasi mkubwa anayeshukiwa kuwa drug dealer ambaye ana ugomvi na Makonda baada ya kutajwa na Makonda.
wewe kwanini unadhani aliamini maneno tu ya kina ruge? ukumbuke alikwenda pale kupata maelezo kamili. ulichoonyeshwa wewe ni cctv footage ya mapokezi tu. ya yaliyotokea ndani hujaonyeshwa. unadhani na yeye nape hakuonyeshwa? yeye kaona na kusikilizishwa mchezo mzima sio kuambiwa mchezo mzima. aliyoyasikia kwenye ripoti hayakua mageni kwake kwa wakati ule basi tu ili taratibu ziwe zimefuatwa. huyo aliyetenda kwanini alikataa kuhojiwa? tena na waziri? sijaona mkenge wowote aliongizwa kama unadhani wewe mkuu. hili suala liko wazi. raisi ana mahaba na bashite hata kama ni kwa gharama ya kuwadhalilisha mawaziri wake. kachukia uchunguzi kufanyika. kwanini? haya leo umemsikia kachukia hata magazeti kuripoti front page tukio la nape kuvamiwa kwa bastola. mambo ya ajabu sana na yako wazi wala haitaji kutafuta consiparacy theories ambazo hazipo
 
luna mahali napre nae kateleza tuseme ukweli,najua tu katenguliwa kwa sasa ila kuna kazi inamngoja,hapa napt bado haelewi somo kwamba wakati wake umepita,kwasasa kuna Bashite,ndio pale kutaka kuonyesha kwa nao bado wamo ndo matokeo,huyo kapumzishwa tu asipanick anaandaliwa kazi ingine njema tu na atatulia.
 
Mkuu, mtei alipotofautiana na Nyerere aliondoka asubuhi!!

nape alichelewa sana, hakutakiwa kusubiri kufukuzwa....
Mkuu, Mtei aliongea na Nyerere tete a tete si mara moja. Ilipoonekana ameshikilia msimamo wake na 'hawata afikiana' katika majadiliano Mtei akampa nafasi Rais kwa kujiuzulu

Hili la Nape ni tofauti . Ilipotokea usiku kesho yake mapema Nape akaenda Clouds
Lengo lilikuwa kusikiliza pande zote na kuunda tume kutokana na taharuki iliyotokea kwa jiji na nchi

Kwa maana nyingine alijaribu kutafuta solution wakati permanent solution inafuata

Alitambua mtu anayehangaika naye ana ukaribu, lakini pia alitambua wajibu wake kama msaidizi wa Rais ni kwenda na majibu na si kusikiliza nini aambiwe nini afanye

Katika hali ya kawaida, Mheshimiwa alipaswa kumwita na kumwambia ajiuzulu

Tofauti na hapo asubuhi kibarua kikaisha, sina uhakika kama alipata haki ya kusikilizwa

Endapo Nape alifanya kosa, kiongozi gani mwingine ameonyesha mbadala wa kile alichofanya?

Of course Nape alijua inaweza kuwa na gharama lakini katika mizani ya alichofanya na alichofanya mwanamfalme havilingani hata kidogo.
 
mbona nape alijua kama kunauwezekano wa kutolewa kwenye uwaziri.na ndio maana alisema kua kazi hii inagharama.ilifikili ni gharama hela?
hivyo alivyofanya nape ndio kazi.yake inatakiwa kufanywa.
na kwa mwanasiasa tukio hilo ni lakawaida kabisa.


Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
waberoya! unapo post kitu jaribu kutumia upeo kidogo kufikiria, yule ile ni wizara yake na ni miongoni mwa majukum yake kutatua changamoto zote zinazoikabili tasnia ya michezo na sanaa kwa ujumla, kwa iyo ww unafurahia lile tukio lililotokea pale clouds media? na angekaa kimya ili iweje? ionekane kwamba na yeye anasapot ule ujinge? tuwe wazalendo jaman na hii nchi, tusiongee tu kama maneno yanatokea tumbon, baada na ww mwananchi wa kawaida ukemee huu ujinga uliotokea ndio kwanza unamshaur wazir mwenye dhamana akae kimya sasa wale watu wakesemee wapi? kwel wa akina bashite mko wengi
Leo unamuita mzalendo mtu aliyesema atawapiga bao la mkono kwenye sanduku la kupigia kura...hapo kwenye hilo sanduku umejaza akili au uji mgando (ugali)
 
Wewe ni muoga rais ikibidi unambadilikia sio ndio mzee tu afterall hii ni mipango wabunge wot wa ccm wamejipanga kudhibiti hali inayojitokeza kwa sasa ya mkuu kuwapiga mkwara kila mara km ilivyotokea kwenye mkutano wajuzi Dodoma. Akisema kama wabunge wataendelea kumhujumu atalivunja bunge aitishe uchaguzi mwingine! Wanaona km hcho ni kitisho kwao!!
 
Tatizo la nape aliamua kuchagua upande wa kina Mengi kugain popularity na jasa ukichukulia presha ya makonda kwa sasa,.akaacha upande uliomuweka pale..hata Mimi ningekuwa rais ningemuacha aende..kwa sasa shughuli imekwisha
 
Inavyo onekana Nape alijua anacho kifanya na alijua kitacho tokea, Uzuri wa wana sihasa wana uwezo wa kubadilika kutokana na mazingira. Nape kasoma nyakati na kafanya alicho kifanya. Kwa kiasi flani ni kama amefanikiwa mission yake.
 
Back
Top Bottom