Backagain Afterages
Senior Member
- Jan 23, 2017
- 151
- 118
Usitake kudanganya watu. Hakuna kikao cha siri kilichofanyika kati ya Nape na akina Ruge. Nape aliingia clouds tv akiambatana na waandishi wa habari. Kikao kilikuwa wazi kabisa tangia mwanzo hadi mwisho.
Halafu nani alikuambia kuwa mamlaka ya nidhamu ya kazi ya wakuu wa mikoa ni mawaziri? Maana ni mwenye mamlaka ya nidhamu ya mtumishi husika tu ndiye anaweza kuunda kamati ya aina hiyo ya uchunguzi wa huyo mtumishi kwa lengo la kumchukulia hatua kali ya kinidhamu ikiwamo kumfukuza kazi. Na kamati ya aina hiyo hupewa hadidu rejea mahususi kwa kazi hiyo. Kamati ya Nape ilikuwa haina kitu kama hicho isipokuwa kuleta majibu ndani ya saa 24! Wapi na wapi kamati ya aina hiyo iliyowahi kupatiwa muda mfupi namna hiyo. Standing Orders zinatoa muda usiopungua 14 days.
Tatizo la wanasiasa wetu wanadhani wao ndiyo mamlaka ya nidhamu ya kila mtumishi wa umma. Utakuta wanasimamisha au kufukuza kazi watu ili hali wao si mamlaka yao za nidhamu, at the end they backfire kama ilivyotokea kwa Mh. Nape. Kuna madaktari wamefukuzwa kazi na madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya/ mikoa, mawaziri na hata wenyeviti wa mitaa. Ni vurugu. Labda semina elekezi za wanasiasa hawa zilizokuwa zinafanyika Ngurudoto zirejeshwe.
1.wewe ulionyeshwa live tangu anakwenda clouds anaingia na kilichoendela hatua kwa hatua au uliishia kuona akihutubia waandishi wa habari akiwa clouds?. anafika tu na kukaa kikaoni au anafika na kukutana na mangement ya kituo kupata taarifa kabla ya kuhutubia waandishi? jaribu kufikiri kwanza.
2. alikua waziri wa wizara inayosimamia tasnia hiyo. mamlaka yake ilikua ikimruhusu kufuatilia suala hilo. na hakusema atamchukulia hatua bali angewasilisha ripoti kwa mamlaka husika. unataka kusema kwa mfano waziri wa mambo ya ndani hana mamlaka ya kuagiza uvamizi wa Daudi uchunguzwe kwa hatua zaidi? unaongea vitu gani mkuu?