Hoja nzuri kaka, lakini ukimsoma Nape kwa makini ni kana kwamba alikuwa anawasilisha malalamiko ya Baraza la Mawaziri, ni kama inaonyesha Mawaziri wengi hawako happy na jinsi Raisi anavyoendesha nchi, sio kwa issue ya Makonda pekee bali pia kwenye maamuzi mbalimbali, yaani Mawaziri wanakosa ile hali ya kujiamini, issue ya Makonda kuendesha zoezi la Madawa ya kulevya bila kumshirikisha Waziri mwenye dhamana ni tatizo kubwa
Nape amekuwa kama Kondoo wa kafara na sababu kubwa ni kuwa Nnape sio mwoga hivyo aliamua kupambana na Magufuli kupitia vituko vya Makonda
Shida kubwa iko kwa mawaziri wenzie, je watamuunga mkono nao wajihudhuru? Ili kuonyesha hawakubaliani na jinsi Raisi anavyoendesha nchi