Mara ya kwanza kuingia Gerezani 2017, sikulala hakika Sitosahau

Hebu Ngoja kwanza. Ni wewe au Unatuletea Hadithi za Kutunga.? Mambo ya. ITAENDELEA yanatoka wapi
Huu ni uzwazwa kuleta tamthilia za fasihi and andishi kama Stori za Shigongo ..sa kama hakujipanga kwa nn alete uni kam huu alafu atuahidi anarudi ..basi km vp apogee tu asirudi
 
SEHEMU YA PILI

Wakati kesi ikiendelea Katika Mahakama ya wilaya mkoani x nilianza kushauliwa na ndugu na Jamaa wangu wakaribu kuwa niende kwa Mganga kumaliza hii kesi

Baada ya kupewa ushauri , Mimi nilikataa kutumia Ndumba zozote Bali nilisema ikitokea nimefungwa itabidi nitumikie tu kifungo .

Wakati kesi ikiendelea nilimuomba sana Mungu anivushe maana sikukusudia mtukana Rais bali ni yeye Raisi ndo alituletea Maneno ya kuhudhi kipindi kile amekuja Bukoba na kudai kuwa Hatowapatia Wahanga wa Tetemeko hela zao tulizowachangia. Na Mimi ndipo Nilimtukana Live kwa kumuita katili asiyekuwa na Huruma dhidi ya Binadamu wenzio .

Jambo hilo lilizua Gumzo kwani niliongea hayo Maneno Mbele yake na nilikuwa na umri Mdogo 19 years tu.

Zipi sababu za kufariki wapelelezi was kesi yangu wote .

Ukweli hawa wapelelezi waliniomba sana pesa ili kunisaidia na niliwaambia hakuna pesa ya Bure. Jambo ili liliwakera hadi kuanza kunikandamiza Mahakamani ili tu nifungwe.

Nilichofanya Ni kuwaombea Dua tu kuwa washindwe wao na nia zao hasi juu yangu.

Maaajabu hii kesi watu 90% walikuwa upande wangu kuanzia hakimu , wanasheria wa serikali hadi Wananchi.

Hivyo Basi Hakimu na mwanasheria was serikali na DPP wote walisema dogo yupo kwenye haki na anabidi kuachiwa huru maana huyu Rais amezidi kuendekeza kunyanyasa watu.

Jambo hili lilinifanya nimshukuru sana Mungu kwani ukiwa upande wake hakuna linaloshindikana.

Maisha ya Gerezani , ukweli Gerezani hasa Tanzania sio sehemu salama maana watu wengi wananyimwa haki zao muhimu Kama kula , kuabudu , kusoma n.k

Kuhusu ushoga Mimi Jambo hili sijaliona Wala kulisikia maana Mimi nilitengwa nikawa tunakaa sero yenye watu 04 tu VIP maana Mimi nilikuwa moja ya watu waliokuwa wanaogopwa wakidhani eti Mimi natumiwa na Tiss hakika maaskari wetu kitaaluma Bado sana.

Hali za watu Gerezani
Kiukweli niliwaona watu wamekonda na wamechoka sana na wamekaa Gerezani Muda mrefu wakiwa mahabusu , Aisee hapa panaumiza watu haki. Zao zinavunjwa sana

MSAADA WANGU NIKIWA GEREZANI WAFUNGWA

Nilifanikiwa kuwaandikia watu 05 rufaa zao waliokuwa na kesi mbalimbali na sasa wapo huru 03 na wawili wamepunguziwa Adhabu kutoka life sentences hadi miaka kadhaaa.

Ni hayo tu ndugu zangu.

NYONGEZA

Ukweli ni kwamba wapelelezi walifariki baada kesi yangu kufutwa mahakamani pia hata Mwanasheria wa serikali aliyepewa Ujaji alipewa baada ya kuwa amefuta kesi yangu

Japo haya Matukio yalifatana sana. Ilikuwa ni ndani ya Mwezi mmoja .
Miaka 19 unauwezo wa kuandika rufaa za kesi, imekaaje hii
 
Ilikuwa 2017 nilipoingia Gerezani kwa mara ya kwanza kwa kosa la kutoa lugha ya kuudhi dhidi ya Rais wa Tanzania kipindi hicho John Pombe Magufuli.

Kweli wakuu Nilimtukana Rais wa JMT tena kwa lugha Kali hii ni baada ya Kupata hasira za hapa na pale.

Ilikuaje nikamtukana Rais maneno makali, hapa ni baada kusikia kuwa hela za Tetemeko tulizowachangia wahanga hazitowafikia hata senti 100.

Hakika jambo hili lilinifanya kumtukana Rais matusi ya kutosha.

Baada ya kumtukana Rais nilikamatwa na Makachero na kuniweka kizuizini siku 08 ndipo nilipewa dhamana.

Baada ya dhamana niliendelea kuripoti kituo Cha police kila siku.

Na baada ya hapo nilipelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka 03 yote yanahusu kumtukana Rais na kumdhalilisha.

Baada ya kufika mahakamani nilikana kosa na kupelekwa Gerezani moja kwa moja maana nilikosa wadhamini.

Nilikaa Gerezani siku 23 ndipo nilipatiwa dhamana.

Kesi yangu ilichukua Mwaka 1 tu na niliachiwa huru na wale wote wapepelezi kutoka upande wa Jamhuri walifariki wote na Mwanasheria aliyeniachia huru kupitia Nole sahivi Ni jaji wa Mahakama kuu Maana aliteuliwa na Magufuli 2019.

Maisha ya jela
Ukweli Ni kwamba Gerezani Kuna watu wanaishi vizuri sana kama vile wapo nje pia kuna watu wanaishi motoni

ITAENDELEA
JE ILIKUAJE NIKAACHIWA HURU KWA KESI NZITO KAMA HIYO LICHA YA KUTOKUWA NA PESA.
VAR inasemaje kuhusu malinda yako?
 
hii chai imepoa kabisa eti uliwaandikia mahabusu wenzako 05 rufaa zao kwanza hapo ulikuwa na elimu gani na uzoefu upi hadi ukaandikia rufaa mahabusu wenzako kwanza tangu lini mahabusu akawa na rufaa kabla ya kuhukumiwa maana umesema mwenyewe kipindi hiko ulikuwa na miaka 19 tu..acha kutufanya sisi mazuzu
Anatuona sisi maphalerr huyu
 
Rufaa Ni Kama barua mkuu hapo ni huwezo wako mzuri wa kuwasilisha hoja na kujua kuandika kizungu tu ebu fatiliya kwanza
ww kweli ujielewi ujui hata kipi hasa unachokitetea humu kwa miaka yako wakati huo 19 kibongo bongo wengi kuwa na elimu gani umri huo.. ata kama kizungu kinapanda ndo ulikuwa unajua kabisa lugha ya kisheria na vifungu vyake hadi kuandikia barua za rufaa kwa kuonesha matobo ya kisheria tena kwa facts na vifungu kwenye hukumu ya mahakama ya wilaya kwa miaka 19 yako! au pengine mimi ndio sijui labda barua za kukata rufaa ya hukumu zinaandikwa kama barua ya hawara tu
 
Rufaa Ni Kama barua mkuu hapo ni huwezo wako mzuri wa kuwasilisha hoja na kujua kuandika kizungu tu ebu fatiliya kwanza
Rufaa? Hii hii rufaa?? Acha ujinga na uongo
Hapa umefeli, miaka 19 huwezi kuandika rufaa
 
hii chai imepoa kabisa eti uliwaandikia mahabusu wenzako 05 rufaa zao kwanza hapo ulikuwa na elimu gani na uzoefu upi hadi ukaandikia rufaa mahabusu wenzako kwanza tangu lini mahabusu akawa na rufaa kabla ya kuhukumiwa maana umesema mwenyewe kipindi hiko ulikuwa na miaka 19 tu..acha kutufanya sisi mazuzu
Ngese sana hii dogo.
 
Rufaa Ni Kama barua mkuu hapo ni huwezo wako mzuri wa kuwasilisha hoja na kujua kuandika kizungu tu ebu fatiliya kwanza
Kiswahili hujui kizungu ndiyo utajua?
Huwezo ilitakiwa uandike uwezo.
Fatiliya ilitakiwa uandike fuatilia.

Enzi za Jiwe kuna hakimu au mtumishi yeyote ambaye angeweza kuwa upande wako?

Ulikuwa na miaka 19 na huna uzoefu wa kesi wala mambo ya mahabusu na mambo ya mahakamani huwezi kuandika rufaa ya mtuhumiwa.

Pia rufaa siyo barua,kuna lugha ya sheria na vifungu vya kisheria vinatakiwa viwepo.

Huu ni uongo mkubwa,labda kama unataka kutangaza uganga wako,wenye kesi wakutafute nao wakawaue wapelelezi wa kesi zao.
 
Ni kweli kuna watu huwa nguli wa masuala ya kisheria wanapokuwa jela lakini ni mpaka waishi humo kwa muda mrefu.

Wewe siku ulizokaa jumla ni mwezi mmoja huo uzoefu wa kuandikia watu rufaa ukaupataje?
 
Gereza ni sawa na kuzimu, nyampara kijana mdogo anampiga mzee mtu mzima bila heshima kwa kosa dogo, ila kuna ambao wanaona gereza ni paradiso, wanakula chakula cream na wana afya kuliko maisha yao ya nje. Nyampara ndio huishi vizuri gerezani
Hivi nyampara ni mfungwa mwenzako au askari magereza?
 
Back
Top Bottom