M SELENHO
New Member
- Jul 27, 2026
- 2
- 0
Maridhiano ya kweli yalipaswa kufanyika kabla ya uchaguzi wa kiini macho wa Oktoba 2025. Lakini kwa sababu walikaza fuvu, walitawala kimabavu baada ya kuua, kuteka na kubambikia raia kesi za uongo, sasa maridhiano yenye dhamira njema lazima yaanze na uwajibikaji kwanza.
1. Uchunguzi huru (pigia mstari huru) na wa kweli wa mauaji "MO29", majeraha na utekaji (Humphrey Polepole na wengine) ufanyike mara moja. Tume ya serikali peke yake haitoshi na haina uhalali. Wanaohusika, iwe polisi, majeshi au viongozi wa serikali, washtakiwe, wahukumiwe na wapewe adhabu ya haki.
2. Viongozi wa upinzani na wananchi wengine walioko jela kwa kesi za uhaini zisizo na msingi thabiti waachiliwe au wahukumiwe kwa haki waziwazi mahakamani. Kesi za kisiasa hazipaswi kuendelea kutumika kama silaha ya kutisha na kunyamazisha watu.
3. Mazungumzo ya kitaifa yaanze tu baada ya hatua za uwajibikaji, si kabla. Yahusishe CCM, CHADEMA, waathirika wa mauaji na utekaji, kubambikiwa kesi na vurugu, viongozi wa dini, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla.
4. Katiba mpya iandaliwe kwa ushirikishwaji wa wote, ikifuatiwa na uchaguzi huru na wa haki chini ya tume huru kabisa kabla ya 2028.
Bila haki, adhabu kwa wahalifu na uwajibikaji wa kweli, maridhiano ni maneno matupu tu. Amani endelevu inatokana na uwajibikaji, si kujisahaulisha au kuficha ukweli.