Mkuu hayo uliyoandika, huyo Katibu Mkuu Slaa ni Mangi Meza, wenzao huku CCM ,chama kisikivu, kama kuna mtendaji anayepigiwa kelele kwa ubovu, huondolewa.
Tulikuwa na Mzee Makamba, Mzee Mukama sasa Kinana-kama tuhuma zinajitosheleza au utendaji ni hafifu, kwa kuokoa chama mtu huyo anapumzishwa kwa heshima zote.
Huko CHADEMA jamaa wameng'ang'ania kama luba, hawaoni wala hawasikii!
Nia kubwa kila mtu ni kujaribu bahati yake kupiga penalti ya kuingia Ikulu-kitu ambacho sasa wameanza kuelewa kuwa hawawezi.
Mapungufu ya Dr Slaa ni mengi mno kuliko mazuri yake kisiasa, tokea maisha yake binafsi, utendaji na hata mahusiano binafsi.
Kwa vile aliwahi kuwa mhubiri, ukimpa mike hapo ndo mmekwisha, lakini na hapo ndio mwisho wa weledi wake.