ukweliusemwekweupe
Member
- May 2, 2026
- 59
- 51
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NDUGU, JOHN MNYIKA, UNAPOTOSHA WATANZANIA.
Na David Maphone.
Nimebahatika kusikiliza vizuri sana, Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilicho sajiliwa nchini Tanzania .
Akizungumza nje ya mahakama, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Ndugu John Mnyika, amesema kuwa wamepokea barua rasmi kutoka Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchi wakihoji maswala mbalimbali kutokana na vitendo na matamko ya chama kuwa ni muendelezo wa njama dhidi ya CHADEMA
Soma pia Mnyika: Bado Ofisi ya Msajili inatafuta njia Shughuli za CHADEMA zisimamishwe, tumeandikiwa barua tujieleze
SOMO,
KATIBU Mkuu wa CHADEMA anapaswa kujua Kwamba baada ya maamuzi ya Mahakama ya
Rufaa Chadema kama chama kinarudi kutekeleza Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 (sura 258) inayosimamiwa na Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kama vyama vingine vyote 19 vyenye usajili wa KUDUMU.
Hivyo maamuzi ya Mahakama ya Rufaa hayajatoa maelekezo kwamba Chadema isifuate na kutekeleza Sheria ya vyama vya siasa na ukisoma Sheria ya vyama vya siasa utakuta kuna chama au Kiongozi wa chama kuandikiwa barua za ONYO, barua za kuomba kutoa ufafanuzi, kusimamishwa kwa Viongozi, kufungiwa Ruzuku ya chama na adhabu kubwa Kuliko zote ni kufutiliwa mbali usajili wa Chama.
,UONGO UKIACHWA UNAWEZA KUAMINIWA.
Mahakama Kuu masijala ndogo ya D'salaam ilipokea shauri la Said Issa na wenzake wanachama halali wa Chadema dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya wazamini wa Chadema na sio Said Issa na waliomshawishi au kumshauri dhidi ya Katibu Mkuu wa Chadema na Bodi ya wazamini shauri la aina hiyo bado kabisa halijafika kwenye Mahakama
Mwanamke ana kwenda Mahakama kudai haki zake za ndoa, mwanaume ana jianda vizuri kwenda kuithibitishia mahakama kuwa haki za ndoa anazitoa kwa ukamilifu wake kwa UTHIBITISHO huu na huu na sio kuwasha tochi kuanza kutafuta nani kamshauri mke wangu kwenda mahakamani huo ni ubabaifu.
Ukweli ni Kwamba kwenye Taasisi zote za umma na binafsi ukienda na suala lako wakiona ila utata au utatuzi wake unaweza zusha jambo lingine, kelele au lawama mara zote tumekuwa tukipokea maelezo au ushauri kuwa nenda Mahakamani halijawahi kuwa kosa
Sote tunaamini Mahakama ndio chombo sahihi cha kutoa haki ndio maana Chadema walipata haki kwenye Mahakama ya Rufaa hivi karibuni. Kwanini mnatupigia makelele kuwa Said Issa alishawishiwa ?
Mwandishi
David Maphone.