Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 23,546
- 70,457
Hii nchi mbona tumekuwa watu wa ajabu sana? Kwanini waliopewa mamlaka ya kiuongozi wamekuwa wajinga kiasi hiki?
Hivi kweli hili nalo ni tukio la muhimu kiasi hicho? Rais kurejea nchini ni tukio la kufanya kuwa kama shughuli ya kitaifa? Kwanini lisingefanyika kwa protocol za kawaida tu?
Huu ni ufujaji wa kodi za walalahoi. Hizo gharama za hizi shughuli zingetumika kuwajengea wamachinga mnaowavunjia vibanda vyao maeneo mazuri wafanye biashara zao ili waondoke mabarabarani wanapofanyia biashara.
Kweli tulidhani kuwa tumemaliza kuyaona maajabu enzi za mwendazake kumbe sasa ndio tuna viongozi wanaojipendekeza kwa rais kiasi cha kufanya mambo yasiyo ya msingi kabisa.
Ongezeni tozo.