voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Kwanza nianze kwa kuuliza, inakuwaje Waziri wa Tanganyika akaapishwe kwenye eneo ambalo sio eneo lake la kazi?
Je, Wazanzibari wanaweza kukubali Rais wao kuja kuwaapisha Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar huku Tanganyika?
Je, Tamasha la "Kizimkazi" lina umuhimu gani kwa Rais wa JMT kiasi kwamba ashindwe kuondoka huko na kuja Ikulu ya Chamwino - Dodoma na kutimiza wajibu wake na kisha kurejea huko atakakopenda?
Je, hizo gharama za misafara ya Baraza zima la Mawaziri na wafanyakazi wa wizara pamoja na maafisa wengineo wa kiitifaki, kuelekea Zanzibar na kufanya tukio lote? Sio matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi?
Posho, nauli za ndege, malazi, magari na mafuta na madereva ikiwa pamoja na gharama za kuvivusha vifaa vyote hivyo kisa tu Rais yuko kwenye "Kizimkazi Festival!" Napata picha ya West Africa inayo trend sasa!
Mbona tunachezewa namna hii?