Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Hizi data za kupika hatufikishi kokote
Ukweli unabaki pale pale kwamba tukikurupuka kujiingiza kwenye viwanda wakati kilimo kinasuasua hatuendi kokote. Kilimo kinagusa karibia kila sekta. Viwanda vitategemea mazao ya kilimo, viwanda vitatengeneza pembejeo kwa ajili ya kilimo, viwanda vitatengeneza madawa kwa ajili ya kilimo, viwanda haviwezi kuwepo bila kilimo ila kilimo kinaweza kuwepo pasipo viwanda.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
"Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo----" maana halisi ipo hapo. Nchi hizo huendeleza kilimo, na huendelea mbele zaidi kwa kuendeleza viwanda baada ya kuwa na msingi fulani wa kilimo.

Lakini pia tusichukulie kuwa nchi zote zinafanana. Kilimo na viwanda vya Marekani haviwezi kuwa 'model' ya maendeleo ya Tanzania. Kwa mfano, wakulima wa Marekani ni wenye mashamba makubwa, tena wachache. Sijui kama Tanzania tunaweza kuwaondoa wakulima wote wadogo tuwapeleke mijini kupisha mashamba makubwa. Nadhani Tanzania itanufaika zaidi kuwaimarisha hao wakulima wadogo wadogo kuwa na kilimo cha tija.
Ndio, maendeleo yataimarika zaidi kwa kuanzisha na kuimarisha viwanda, lakini sio viwanda kuwa mbadala wa kilimo katika kuleta maendeleo ya haraka, hasa huko vijijini.
Tufanye kilimo na Elimu viwe vipaumbele vya kudumu katika mipango ya maendeleo, wakati tukiendelea kushughulikia hivyo vipaumbele vingine, kama miundombinu, viwanda na kadhalika.
 
hello JF,

Mie naona kwa vile taifa letu 80% wanategemea kilimo

Then serikali inge invest huko sio kununua ndege..

Ndege ni maendeleo lakini hio pesa ingewekwa kwenye kilimo,kusingekua na malalamishi ya mtaani kugumu…

Tuishaurini serikali iielekeze nguvu kwenye kilimo na kukomboa uchumi wa mtu mmoja mmoja….

1.Magufuli awe flexible,asikilize ushauri wa mawaziri wake,mie statement yake kuwa anakesha kuangalia ma file iliniambia mkuu anapenda kuchukua au kufanya kazi peke yake sio team player,hivyo kuwafanya mawaziri wake kuwa passive,sababu wanaona hawashirikiswi na kuna uoga wa kum confront rais.Hii atmosphere sio nzuri,ibadilike kama tunataka ku move forward...​
2.Ningependa kuona courses za kilimo kwenye vyuo vikuu ziko nyingi na tofauti,FEES kwa hizo course ziwe ALMOST FREE,itawaencourage watu kujiunga na kusoma mambo ya kilimo,kuajiri au kuajiriwa skills ziwe part ya hizi courses pia......​
3.Kuwe na workshops ndogo ndogo zinazo run throughout the year,zinazofundisha mambo ya kilimo,kwa mfano nimeona huko jukwaa la kilimo watu wanauliza nataka kujiajiri kwenye kilimo ila sijui nianzie wapi au mtaji nitenge shilingi ngapi?,au nilime nini? naamini kungekua na hizi workshop majibu yao yangepatiwa ufumbuzi na kuwapa confidence...kufanya wanayotaka….​
NYINGINE ONGEZEENI...lol​

mawazo yako ni mazuri ingawaje umeyatoa kwa mfumo wa kutokubali kile kinachofanywa na serikali ya awamu hii ya 5 kitu kilichosababisha usione uhalisia wa kinachofanyika ila kwa kuwa umetoa nafasi ya kuongeza naeza nikaeleza kulingana na uwelewa wangu..
moja naeza kusema kiwanda na kilimo ni sector mbili tofautu zinazofanya kazi kwa ushirikiano..na ukiangalia sera mazubuti ya serikali hii ni viwanda kitu kinachoopelekea mkulima kupata sokoo la kile ancholima kwa kuwa kiwanda kinategemea raw material kutoka kwa mkulima kwa naeza nikasema sera ya viwanda inaeza ikakuza uchumi kupitia viwanda huku inaipa tija kilimoo kwa kuongeza wigo wa soko kwa hiyo kilimo akijaachwa nyumaa...pili naeza nikasema serikali haijasahau kilimo kamo unavyosema ingeelekeza nguvu kwa ninicho kiona kuna nguvu kubwa tuuh imeelekweza huko ukiangalia mfumo wa kodi ulivorahisihwa kwa wakulima kwa awamu hii..ukitazama kweny mbolea na baadhi ya madawa yameekewa rdhuku ya kutosha kitu kinachowezesha mkulima kupta pmbjeo kwa bei rahisii kwa kweli mi ninacho ona ni ujapendezwa na bombadier tuuh so ukaamua kutoa duku duku lako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo----" maana halisi ipo hapo. Nchi hizo huendeleza kilimo, na huendelea mbele zaidi kwa kuendeleza viwanda baada ya kuwa na msingi fulani wa kilimo.

Lakini pia tusichukulie kuwa nchi zote zinafanana. Kilimo na viwanda vya Marekani haviwezi kuwa 'model' ya maendeleo ya Tanzania. Kwa mfano, wakulima wa Marekani ni wenye mashamba makubwa, tena wachache. Sijui kama Tanzania tunaweza kuwaondoa wakulima wote wadogo tuwapeleke mijini kupisha mashamba makubwa. Nadhani Tanzania itanufaika zaidi kuwaimarisha hao wakulima wadogo wadogo kuwa na kilimo cha tija.
Ndio, maendeleo yataimarika zaidi kwa kuanzisha na kuimarisha viwanda, lakini sio viwanda kuwa mbadala wa kilimo katika kuleta maendeleo ya haraka, hasa huko vijijini.
Tufanye kilimo na Elimu viwe vipaumbele vya kudumu katika mipango ya maendeleo, wakati tukiendelea kushughulikia hivyo vipaumbele vingine, kama miundombinu, viwanda na kadhalika.
Huwezi kuwa mkulima mdogo, halafu uwe na tija katika kilimo. Kilimo kina tija zaidi kikiwa mechanized, na kutumia mbegu bora na ardhi bora au iliyoboreshwa. Sasa mechanization ya heka tatu tatu is not viable, utashindwa competition kama ikiwa fair.

The largest animal migration (annual) ni Chinese New Year na Siyo Serengeti. China ndivyo ilivyojiendeleza pamoja na nchi hiyo kuwa na historia ya kutegemea kilimo walikuwa wanakufa njaa kwa kutegemea peasantry.

Peasantry has proven to be an obsolete form of economy. Not suitable at this time. Kilimo waachiwe watu wa large scale.
 
Kuna kitu kinachozuia 'mechanization' ya kilimo kidogo? Mbona Israel kuna wakulima wadogo!
 
Kilimo ni asilimia 2.5% ya GDP ya Israel. Ni asilimia moja tu (1%) ya waisrael ndiyo wanaojihusisha na kilimo.
Sasa chukua hizo data kutoka ILO halafu linganisha na asilimia 67 ya watanzania wanaojihusisha na kilimo. Pia, tafuta data za agricultural production ya Tanzania na Israel uniambie nini maana ya "Israel ina wakulima wadogo"
 
Niliposema Israel kuwa na wakulima wadogo ni jibu juu ya kilimo cha wakulima wadogo kutokuwa na tija unakokusema wewe. Lakini pia tunaweza kujadili hizo asilimia za wakulima uliowataja, iwe ni Israel au Tanzania, kilimo kinaweza kabisa kubadili hali waliyonayo hao asili mia 67 ya Tanzania, wakati huo huo tukishughulika na kujenga na kuimarisha uchumi wa viwanda.
Hizo data za Israel unazosema nizitafute ndio hasa nataka Tanzania tuzitumie kwa wakulima wetu wadogo. Usiwe na picha hiyo hiyo tu ya mkulima wa jembe la mkono anayepanda mbegu zilizooza, n.k.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
Hivyo viwanda vitatoa wapi malighafi kama ukijitoa kwenye kilimo?
Kiwanda cha nguo-pamba
Kiwanda cha sukari -miwa
Unga mahindi
Bia-ngano, sukari(miwa)
Sigara-tumbaku
Juice -matunda
nk
Viwanda bila kilimo ni sawa na kuwa na walimu bila wanafunzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hello JF,

Mie naona kwa vile taifa letu 80% wanategemea kilimo

Then serikali inge invest huko sio kununua ndege..

Ndege ni maendeleo lakini hio pesa ingewekwa kwenye kilimo,kusingekua na malalamishi ya mtaani kugumu…

Tuishaurini serikali iielekeze nguvu kwenye kilimo na kukomboa uchumi wa mtu mmoja mmoja….

1.Magufuli awe flexible,asikilize ushauri wa mawaziri wake,mie statement yake kuwa anakesha kuangalia ma file iliniambia mkuu anapenda kuchukua au kufanya kazi peke yake sio team player,hivyo kuwafanya mawaziri wake kuwa passive,sababu wanaona hawashirikiswi na kuna uoga wa kum confront rais.Hii atmosphere sio nzuri,ibadilike kama tunataka ku move forward...​
2.Ningependa kuona courses za kilimo kwenye vyuo vikuu ziko nyingi na tofauti,FEES kwa hizo course ziwe ALMOST FREE,itawaencourage watu kujiunga na kusoma mambo ya kilimo,kuajiri au kuajiriwa skills ziwe part ya hizi courses pia......​
3.Kuwe na workshops ndogo ndogo zinazo run throughout the year,zinazofundisha mambo ya kilimo,kwa mfano nimeona huko jukwaa la kilimo watu wanauliza nataka kujiajiri kwenye kilimo ila sijui nianzie wapi au mtaji nitenge shilingi ngapi?,au nilime nini? naamini kungekua na hizi workshop majibu yao yangepatiwa ufumbuzi na kuwapa confidence...kufanya wanayotaka….​
NYINGINE ONGEZEENI...lol​

Mkuu ulipaswa uwe waziri wa maji na umwagiliaji
Uko vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
Revolution katika kilimo iliweza kuzipitisha nchi kadhaa kuelekea katika viwanda.

Kilimo kikiwa stable uhakika wa raw materials unakuwepo.

Kilimo kikiwa stable wananchi wanapata akili ya kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo vya usindikaji

Kilimo kikiwa stable exportation will take place.

Lengo ni kuwaondoa hao wananchi wanaotegemea kilimo, wategemee viwanda (manufacturing).
Tuna watu wengi wanaolima, na hilo ni tatizo kubwa.
Tanzania Ina watu wachache sana wanaolima

The others (small small scale)
Wanajitafutia rizki ya siku mbili Tatu.

Hivyo viwanda vitatoa wapi malighafi kama ukijitoa kwenye kilimo?
Kiwanda cha nguo-pamba
Kiwanda cha sukari -miwa
Unga mahindi
Bia-ngano, sukari(miwa)
Sigara-tumbaku
Juice -matunda
nk
Viwanda bila kilimo ni sawa na kuwa na walimu bila wanafunzi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pengine ana picha ya viwanda vya kuunda na kuunganisha magari, electronics, kufua vyuma, kutengeneza mitambo n.k.
Unajua, watu wanapozungumzia viwanda kwa nchi kama Tanzania ilipo sasa, kilimo hakiepukiki kamwe.
Madini tunayoruhusu yachimbwe ambayo yangekuwa ni msingi mzuri wa kuanzisha viwanda vyetu muhimu, yote tunauza nje, tena kama mali ghafi bila hata ya kuongeza thamani yoyote.

Tunazungumzia viwanda, hata vijana wetu hatuwawekei mikakati ya elimu ya kuwawezesha kuendesha viwanda hivyo.
Tutazungumzia sana viwanda, lakini ukweli ni kwamba hatuandai mazingira ya kuendesha viwanda vya aina yoyote kwa ufanisi.
 
Hebu taja hizo nchi, ujue nyie mliokimbia umande mnatupa hasira

Huelewi concept.
Mtu mmoja alime korosho Mtwara nzima, mwingine Pwani nzima halafu kuwe na viwanda vya mafuta ya korosho, kubangua na kupakia korosho, na kutengeneza pombe za ulaka au juice ya mabibo.
Pia mbolea, mashine za mashamba yake, repair, banks na huduma za wafanyakazi wa shamba hilo kubwa na viwanda vinavyozunguka, mahoteli, etc .. ndiyo vitachochea ukuaji wa uchumi wa Mtwara au Pwani.

Haya mambo ya heka tatu na vyama vya ushirika mtakaa miaka mia mbili hamuendi popote.
 
Pengine ana picha ya viwanda vya kuunda na kuunganisha magari, electronics, kufua vyuma, kutengeneza mitambo n.k.
Unajua, watu wanapozungumzia viwanda kwa nchi kama Tanzania ilipo sasa, kilimo hakiepukiki kamwe.
Madini tunayoruhusu yachimbwe ambayo yangekuwa ni msingi mzuri wa kuanzisha viwanda vyetu muhimu, yote tunauza nje, tena kama mali ghafi bila hata ya kuongeza thamani yoyote.

Tunazungumzia viwanda, hata vijana wetu hatuwawekei mikakati ya elimu ya kuwawezesha kuendesha viwanda hivyo.
Tutazungumzia sana viwanda, lakini ukweli ni kwamba hatuandai mazingira ya kuendesha viwanda vya aina yoyote kwa ufanisi.
Ni kweli kabisa mkuu,
Hata unapozungumzia viwanda vya magari bado kuna viti(pamba, ngozi) tairi (rubber) na nakshi za ndani (ngozi na pamba) zinategemea kilimo
Hata wafanyakazi(wa kiwanda) wanahitaji kula ili waproduce

Tatizo kubwa la kwanza ni mentality yetu watz toward kilimo
Hata familia wakiona una degree halafu umejiajiri kwenye kilimo wanaona umepotea..

Mtu akisema kilimo tunawaza jembe la mkono na kusubiri mvua hatuwazi trekta na umwagiliaji
Mawazo ya kizamani sana haya

Kwa wenzetu Ulaya na Marekani wakulima ni watu matajiri kuliko watumishi wa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Revolution katika kilimo iliweza kuzipitisha nchi kadhaa kuelekea katika viwanda.

Kilimo kikiwa stable uhakika wa raw materials unakuwepo.

Kilimo kikiwa stable wananchi wanapata akili ya kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo vya usindikaji

Kilimo kikiwa stable exportation will take place.

Wrong .. It's vice versa.
Viwanda vya tumbaku ndivo vilivyoanzisha uhitaji wa mashamba ya tumbaku na kutafuta makoloni.
Ulimaji wa tumbaku bila viwanda ni sawa na kuwa na shamba la miarobaini.
 
Hivyo viwanda vitatoa wapi malighafi kama ukijitoa kwenye kilimo?
Kiwanda cha nguo-pamba
Kiwanda cha sukari -miwa
Unga mahindi
Bia-ngano, sukari(miwa)
Sigara-tumbaku
Juice -matunda
nk
Viwanda bila kilimo ni sawa na kuwa na walimu bila wanafunzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaelewa.
Hizo mali ghafi hazihitaji watu milioni 20 au 30 walime. Tatizo mnataka kilimo kitoe ajira, na huo ni uongo. Ni saa na kuingia baa ina mabaamedi 60 wateja wanne.
 
Back
Top Bottom