Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,152
- 128,807
Dada Rebeca, hapa umesema kweli, yeyoye atakayekubishia, anabisha tuu.hello JF,
Mie naona kwa vile taifa letu 80% wanategemea kilimo
Then serikali inge invest huko
Tuishaurini serikali iielekeze nguvu kwenye kilimo na kukomboa uchumi wa mtu mmoja mmoja….
1.Ningependa kuona courses za kilimo kwenye vyuo vikuu ziko nyingi na tofauti,FEES kwa hizo course ziwe ALMOST FREE,itawaencourage watu kujiunga na kusoma mambo ya kilimo,kuajiri au kuajiriwa skills ziwe part ya hizi courses pia......2.Kuwe na workshops ndogo ndogo zinazo run throughout the year,zinazofundisha mambo ya kilimo,kwa mfano nimeona huko jukwaa la kilimo watu wanauliza nataka kujiajiri kwenye kilimo ila sijui nianzie wapi au mtaji nitenge shilingi ngapi?,au nilime nini? naamini kungekua na hizi workshop majibu yao yangepatiwa ufumbuzi na kuwapa confidence...kufanya wanayotaka….
Japo asilimia ya wanaotegemea kilimo imeshuka. Wakati wa Nyerere ndio tulikuwa asilimia 80%, sasa watu wamekimbilia mijini, wanaotegemea kilimo, wamebaki asilimia 67% ambayo bado ni nyingi.
Hivyo kwa taifa linalotogemea kilimo, kutengeneza Tanzania ya viwanda ya ukweli, ni Tanzania ya Agro Processing Industries. Ili hili lifanyike, tulipaswa kuanza na Mapinduzi ya Kilimo ili kizalishe malighafi ya viwanda vya bidhaa za chakula. Ni aibu Tanzania tunaagiza mchele!, sukari, mafuta ya kupikia. Ngano yote ya viwanda vyote vya unga ni imported!. Hata hizi juices za Azam, 80% ya pulp is imported, wakati machungwa yanaozea mitini pale Lushoto, na maembe ya Unyanyembe ni chakula cha popo!.
Tanzania ndio nchi ya tatu kwa mifugo mingi barani Africa Kusini mwa Jangwa la Sahara, lakini kwenye meat export hatupo, export ya hides and skins tuko nyuma, tunaagiza ngozi, maziwa, siagi, jibini!.
Tanzania ndio nchi inayoongoza barani Africa kwa kuwa na vyanzo vingi vya maji!. Bahari ipo na imejaa samaki wa bure, lakini huwezi amini, tuna import vibua kutoka China!.
Ni mengi siwezi kuyamaliza.
Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums
Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums
P.