Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

maendeleo ya haraka!!?..unakimbilia wapi!!?..kutoka kilimo mpaka viwanda inachukua muda gani!!?..ukizingatia elimu ya wakulima wa tanzania!?..unalala angani nini ndo kisa unaota ndoto za ajabu...
Nimemwambia haya kwenye Bandiko namba #15. Uchumi wa viwanda unaweza faidisha nchi lakini hufanywa na watu wachahe wenye mitaji (middle class) na wenye elimu (Skilled labour)waishio mjini. Kilimo ni rahisi sana kubadilisha maisha ya watu wa kijijini ambao wengi hawajasoma lakini wana mtaji mzuri (Ardhi yenye rutuba)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuboresha sekta ya Uchumi ni jambo jema sana, ila nchi haiwezi pata maendeleo kwa kutegemea Kilimo Pekee.
hebu boresha kilimo kwa kukifanya kiwe cha imwagiliaji,kisha mkulima auze mazao yake nje...baada ya hapo uje uangalie maisha ya mkulima baada ya miaka mitatu..sio mnaongea tu wakati kulima hamlimi,takwimu za kilimo biashara hamna..kilimo kwanza then viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo
 
Kuboresha sekta ya Uchumi ni jambo jema sana, ila nchi haiwezi pata maendeleo kwa kutegemea Kilimo Pekee.
Nakubaliana na wewe kabisa, japo ukweli ni kwamba kilimo kinaweza kupunguza umasikini kwa nchi kama Tanzania bila kutumia gharama kubwa. Hayo mengine yafanywe lakini vitu kama kilimo visipuuzwe kabisa, maana mpaka leo hii nchi yetu haifanyi kilimo inavyotakiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hello JF,

Mie naona kwa vile taifa letu 80% wanategemea kilimo

Then serikali inge invest huko sio kununua ndege..

Ndege ni maendeleo lakini hio pesa ingewekwa kwenye kilimo,kusingekua na malalamishi ya mtaani kugumu…

Tuishaurini serikali iielekeze nguvu kwenye kilimo na kukomboa uchumi wa mtu mmoja mmoja….

1.Magufuli awe flexible,asikilize ushauri wa mawaziri wake,mie statement yake kuwa anakesha kuangalia ma file iliniambia mkuu anapenda kuchukua au kufanya kazi peke yake sio team player,hivyo kuwafanya mawaziri wake kuwa passive,sababu wanaona hawashirikiswi na kuna uoga wa kum confront rais.Hii atmosphere sio nzuri,ibadilike kama tunataka ku move forward...​
2.Ningependa kuona courses za kilimo kwenye vyuo vikuu ziko nyingi na tofauti,FEES kwa hizo course ziwe ALMOST FREE,itawaencourage watu kujiunga na kusoma mambo ya kilimo,kuajiri au kuajiriwa skills ziwe part ya hizi courses pia......​
3.Kuwe na workshops ndogo ndogo zinazo run throughout the year,zinazofundisha mambo ya kilimo,kwa mfano nimeona huko jukwaa la kilimo watu wanauliza nataka kujiajiri kwenye kilimo ila sijui nianzie wapi au mtaji nitenge shilingi ngapi?,au nilime nini? naamini kungekua na hizi workshop majibu yao yangepatiwa ufumbuzi na kuwapa confidence...kufanya wanayotaka….​
NYINGINE ONGEZEENI...lol​

Mkuu kilimo ni jambo muhimu lakini kilimo nacho kinategemra sekta nyingine kama viwanda kutengeneza zana za kilimo,mabenki kukopesha sekta ya wakulima,sekta ya usafirishaji kama reli,barabara,meli na ndege ili kusafirisha mazao.
Kwa ufupi kilimo kinategemea sekta nyingine ili kustawi.
Marekani miaka ya 60 ilikuwa wakulima wapatao 4% tu ya watu wake lakini wakitoshereza chakula kwa nchi yao,pia wakizalisha chakula kingi na ziada kuliko nchi yoyote duniani.
Tofautisha a peasant and a farmer.Hapa Tanzania hatuna farmers bali tuna peasants.Tunahitaji farmers wasiozidi 20 tu kutoshereza mahitaji ya taifa letu na kuuza ziada nje.
 
hebu boresha kilimo kwa kukifanya kiwe cha imwagiliaji,kisha mkulima auze mazao yake nje...baada ya hapo uje uangalie maisha ya mkulima baada ya miaka mitatu..sio mnaongea tu wakati kulima hamlimi,takwimu za kilimo biashara hamna..kilimo kwanza then viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo
Mbali na kuuza nje ya nchi na kupata fedha, kilimo bora Food Security kwasababu ya uwepo mwingi wa chakula kitu ambacho hupelekea kushuka chini kwa bei za vyakula(which is highly needed now). Hapa watu watapata mitaji ya kuwawezesha kufanya shughuli nyingine za kiuchumi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kiasi, lakini ukweli ni kwamba Tanzania bado ni nchi masikini hivyo tunahitaji sana kilimo hasa vijijini ili kuondoa utegemezi kwa Serikali. Viwanda huwa vinakuja lakini shughuli zake hufanywa sana na Middle Class ambao hupendelea kuajiri sana Skilled and Cheap labour. Uchumi wa watu wa mjini na vijijini hutofautiana sana hivyo kutumia kilimo nadhani ni njia rahisi ya kuinua per capita ya watu masikini kuliko viwanda ambavyo vinaleta maendeleo ya haraka lakini shughuli zake hufanywa na watu wachache.

Sent using Jamii Forums mobile app
Actually kilimo hufanywa na watu wachache na manufacturing hufanywa na watu wengi. Unapoanzisha viwanda, unachochea migration ya wakulima na unachochea ukuaji wa miji midogo kuwa mikubwa au vijiji kuwa miji.

Pia kuna vitu kama REA. Huu mradi kama hautakuwa coupled na industrialization drive, faida yake aitakuwa kubwa, watu watalima mahindi na mihogo na watashindwa hata kulipia gharama za huo umeme.

Ukichochea uzalishaji wa kilimo tu, utakuwa na surplus for export, na hii haitakufikisha popote pale bali kukubakisha kuwa taifa linalolima na kuuza mazao nje na kununua manufactured products.

Unapochochea manufacturing unachochea population inayofanya kazi za viwandani ambayo itataka kula na itakuwa tayari kununua vyakula vinavyolimwa na watu wachache than before factories were established. Wakulima wachache, wenye soko kubwa la ndani watalima efficiently through mechanization,genetic engineering etc na kuchochea biashara na service industry.

Viwanda pia vinaleta technological transfer. naamini hata tu kwa mfano mdogo sana wa waajiriwa wa Tazara overpass, kuna watu wamejifunza welding, ujenzi, kuendesha bulldozers etc.. au angalau kuchochewa kujifunza hayo.

So, industrialization itoe focus kwenye investment of capital in manufacuring either from private sector or PPP. Na itanguliwe au iende sambamba na uendelezaji wa infrastructure.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
Tupe data?
Viwanda vinategemea malighafi,
Malighafi nyingi zinatokana na kilimo
Binadamu ili aishi anategemea mazao ya kilimo.
Narudia tupeni data halisi hacha kupotosha watu.
 
maendeleo ya haraka!!?..unakimbilia wapi!!?..kutoka kilimo mpaka viwanda inachukua muda gani!!?..ukizingatia elimu ya wakulima wa tanzania!?..unalala angani nini ndo kisa unaota ndoto za ajabu...
Elimu ya wakulima wa Tanzania italetwa na kupewa pembejeo za bure?
Unadhani kutoka kilimo mpaka viwanda inakuja automatically au inabidi ije by design? Wewe sasa ndiyo unaota ndoto za ajabu.
Yaani, viwanda vitakuja tu tartibu baada ya miaka 100 au 200?
Unataka kupeleka korosho asia na kubaki na ulaka. halafu mwakani mrudie tena hayohayo.
 
nini kifanyike?
 
Tupe data?
Viwanda vinategemea malighafi,
Malighafi nyingi zinatokana na kilimo
Binadamu ili aishi anategemea mazao ya kilimo.
Narudia tupeni data halisi hacha kupotosha watu.
Nchi zote za Ulaya magharibi, Marekani na Canada.
 
Actually kilimo hufanywa na watu wachache na manufacturing hufanywa na watu wengi. Unapoanzisha viwanda, unachochea migration ya wakulima na unachochea ukuaji wa miji midogo kuwa mikubwa au vijiji kuwa miji.

Pia kuna vitu kama REA. Huu mradi kama hautakuwa coupled na industrialization drive, faida yake aitakuwa kubwa, watu watalima mahindi na mihogo na watashindwa hata kulipia gharama za huo umeme.

Ukichochea uzalishaji wa kilimo tu, utakuwa na surplus for export, na hii haitakufikisha popote pale bali kukubakisha kuwa taifa linalolima na kuuza mazao nje na kununua manufactured products.

Unapochochea manufacturing unachochea population inayofanya kazi za viwandani ambayo itataka kula na itakuwa tayari kununua vyakula vinavyolimwa na watu wachache than before factories were established. Wakulima wachache, wenye soko kubwa la ndani watalima efficiently through mechanization,genetic engineering etc na kuchochea biashara na service industry.

Viwanda pia vinaleta technological transfer. naamini hata tu kwa mfano mdogo sana wa waajiriwa wa Tazara overpass, kuna watu wamejifunza welding, ujenzi, kuendesha bulldozers etc.. au angalau kuchochewa kujifunza hayo.

So, industrialization itoe focus kwenye investment of capital in manufacuring either from private sector or PPP. Na itanguliwe au iende sambamba na uendelezaji wa infrastructure.
Bwana Kobello unavyosema Industrialization inaajiri watu wengi kuliko Agriculture umechukua takwimu za nchi gani hadi ukasema hivi ? Industrialization imeajiri watu wengi sana kwenye nchi za Magharibi ambazo ni za kibepari kiasilia, hivyo basi kilimo huwa na watu wachache sana kwasababu ni Large Scale tofauti na sisi ambao ni Subsistence Agriculture. Kule watu wanaofanya kilimo nchi zilizoendelea hufanya kilimo kwa biashara tu, sisi tunazalisha ili tule na tuuze. Tafadhali ona hii tofauti yetu Tanzania na Marekani.

Hebu ngoja nimalize kazi ntakuja kukujibu hizi hoja zako zote. Maana hadi huko kwenye REA nilibahatika kuwepo na hivyo nafahamu changamoto zake chache....

Sawa, lakini jua kwamba hata hizo nchi ulizozitaja, zilikuwa na asilimia kubwa ya uchumi wake chini ya kilimo na watu wengi walikuwa wameajiriwa na kilimo.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
Kuna kipindi New zealand kilimo na bidhaa zake ndiyo walikuwa wanachangia sehemu kubwa kubwa ya GDP yake na kipindi hicho ilikuwa moja ya nchi yenye per Capita kubwa sana.
Kwa Tanzania ambayo ni nchi maskini mapinduzi ya kilimo yanaweza double pato la mwananchi au hata kutriple. leo hii wastani ni kama dola 1,000 kwa mwaka. Tikiwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na tukauza huo mpunga nje hata bila kuukoboa, tukauza hayo maharage na mahindi,viazi, vitunguu, ngano nk tunaweza kumtoa mwananchi toka 1000 hadi 3000. hatakuwa tajiri lakini yatakuwa ni maendeleo makubwa sana. Leo hii watanzania kama 40 kati ya mia wana udumavu sababu ya lishe duni
huu hupelekea na udumavu wa akili. Mapinduzi ya kilimo yatadoa hii ishu na si ununuzi wa ndege. yanini kukimbilia mambo magumu makubwa na hali una njia rahisi ya kuinua uchumi wa wananchi wako.
 
Rebecca hili suala lilitakiwa kupata mjadala mkubwa na Serious. Hapa tunahitaji viwanda vya mbolea, viwanda vya zana za kilimo, Ujenzi mkubwa sana wa miundo mbinu ya umwagiliaji. Tanzania ni ya pili baada ya DRC kwa kuwa na maji baridi mengi Africa. Pia tuna 29ml acres za kufaa umwagiliaji. Tuna kila kitu ila utasikia Thailand nchi tuliyoizidi ukubwa mara tatu ndiyo inaongoza duniani kwa kulima mpunga.

Kingine kikubwa ni masoko.Haitakiwa hizi mambo za kuzuia watu kwenda kuuza nje ya nchi. Hiyo inavunja watu moyo kuwekeza pakubwa kwenye kilimo na in a long run husababisha njaa na wakati ilitakiwa kuzuia njaa. Nashauri hata tungeanzisha soko huru la chakula la EA.
Tutumie kilimo kwa potential yake yote kuinua maisha yetu kisha ndiyo tuanze na vitu complex kama biashara ya Anga.
 
Nimemwambia haya kwenye Bandiko namba #15. Uchumi wa viwanda unaweza faidisha nchi lakini hufanywa na watu wachahe wenye mitaji (middle class) na wenye elimu (Skilled labour)waishio mjini. Kilimo ni rahisi sana kubadilisha maisha ya watu wa kijijini ambao wengi hawajasoma lakini wana mtaji mzuri (Ardhi yenye rutuba)

Sent using Jamii Forums mobile app
Kilimo cha wengi hudumaza uchumi na kuchochea umaskini. Kilimo siyo njia ya haraka ya kututoa kwenye umaskini.
Lets stay away from peasantry and industrialize.
 
Kwa nchi maskini kama Tanzania, nafikiri Mapinduzi yaliyotakiwa yaanze kwanza yalikuwa ni ya kilimo; unaanza kujenga viwanda je umejiuliza:
1. Ni viwanda gani hasa unavyovijenga, vitazalisha nini? na soko la bidhaa hizo litakuwaje?
2. Je watu wako umewaanda kwa mabadiliko hayo? hasa vijana wa kufanya kazi katika hivyo viwanda
3. Je malighafi ya kutumika viwandani itapatikana wapi? ni lazima iwe hapa nchini tena kwa walau 80%
4. Mafundi Mchundo (Technicians) wa kitanzania wameshaandaliwa ku-operate hivyo viwanda?
5. Je umefanya bulding capacity kwa watu wako? umefanya tathmini ya mapokeo ya mapinduzi haya kabla hujaanza uli uone kama yana mapokeo? (sauti ya wengi)

Utaona moja kwa moja kwamba mafanikio ya haraka yangekuwa ni ya KILIMO. ambacho hivi tunavyoongea kingekuwa kimeajiri vijana si chini ya 10,000 katika kila wilaya hapa Tanzania tena kwa fedha kidogo.
 
Back
Top Bottom