Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Mapinduzi yawe ni ya kilimo....

Kwa jinsi hali ya Tanzania ilivyo tayari sehemu kubwa ya ardhi wanayo wakulima wadogo wadogo (hekari 1-5)

Utatumia mfumo gani kuitoa ardhi kwa wakulima hao wadogo na kuwa mikononi mwa wakulimwa wachache wakubwa (full capitalism)???
Tanzania bado kuna ardhi kubwa imebaki inayofaa kwa kilimo.
Hata hivyo, ardhi Tanzania ipo chini ya wananchi wote na rais akiwa mdhamini wao. Mradi wowote mkubwa wa kilimo, kama utaunga mkono industrialization utachukua ardhi ya wakulima hao wadogowadogo kama itaona inafaa kufanya hivyo. Ili mradi walipwe fidia kama wanavyofanya kwenye miradi mingine.
 
Ningependa wachumi wangeijaza hii topic,sio sisi wenyewe tunabishana tuuuuu...sijui ningeiwekaje kuwavuta hao wachumi...mnghhhhh 😕😕😕😕😕😕😕😕….
 
Ushauri mzuri.Sijuwi ule mpango wa Kilimo Kwanza umeishia wapi.

hata sijui mkuu,naona hili wazo liepingwa vikali,

mie I just think tukiwekeza kwenye kilimo,

kutakua hakuna unemployment,

na kama hakuna unemployment then serkali inaweza kudirect resources zake kwingine including kujenga viwanda…

swala la tunahitaji wakulima wachache sioni kama liko sahihi,yaani uwajaze watu viwandani wakufanyie kazi,instead wangelima na kujilisha na mengine ndio wakulete kiwandani.???.hili jambo mmelichukulia too general..labda hatutaona positivity at national level ila uchumi wa mmoja mmoja wetu atainuka …kama tukitilia mkazo

second viwanda vitahitahi skilled labour na machinery sasa hivi uki compare na kilimo kipi chepesi na achievable?

Again,UZALSHAJI lazima uwe maximum ndio twende viwandani,sasa kama wakizalisha/lima kidogo utafanyia nini hizo machine???uzalishaji lazima uwe at Maximum sad it means kilimo ndio kianze kwanza...kikishafika maximum or optimum level ndio viwanda vijengwe....
 
Ningependa wachumi wangeijaza hii topic,sio sisi wenyewe tunabishana tuuuuu...sijui ningeiwekaje kuwavuta hao wachumi...mnghhhhh 😕😕😕😕😕😕😕😕….

Wazo lako ni zuri mkuu.
Tatizo limekuja pale watu walipokuja na tafsiri zao za viwanda.

Na hili ndio tatizo ambalo linaikumba sera ya uchumi wa viwanda. Ukweli ni kwamba hatujui ni aina gani ya viwanda tunavihitaji.

1. Sekta ya kilimo inafungamana na baadhi ya viwanda mfano sukari,pamba,mafuta ya kula, spices (whole and grounded).
So wakati tunahimiza mapinduzi ya kilimo viwanda hivyo ambavyo vinamafungamano ya karibu zaidi na kilimo lazima tuvikuze (viende) pamoja.

2. Then kuna swala la viwanda vya aina ya bidhaa ambazo hazitokani na mali ghafi za kilimo mfano chuma, vifaa vya umeme na vya kupikia nk. Aina hii ya viwanda ndio inabidi itiliwe mkazo baada ya hatua ya #1.

3. Kuna swala la huduma zitakazotolewa kuhudumia sekta zote hizo hilo nalo ni la muhimu. GDP ya nchi iliyoendelea huundwa na pato kubwa katika services (more than 50%), halafu industry (20%-40%) na mwisho kabisa agriculture (1%-10%)

Kwa mantiki hiyo sekta ambayo itatoa ajira kwa watu wengi na kuleta impact kubwa zaidi ni hii services. Na hii ndio sekta pekee ambayo inaingia kwenye sekta nyingine zilizobakia. Service sector inajumuisha finance, insurance, transportation, consultation, R&D,market etc
 
swala la tunahitaji wakulima wachache sioni kama liko sahih

Hapa kuna kitu cha kutofautisha kati ya peasant na farmer. Kwa bahati mbaya maneno haya tunayatafsiri kama 'mkulima'.
Peasant ambae ana ekari 3 anakumbwa na changamoto za kuendesha kilimo chake kwa gharama kubwa. Na hawezi kutumia teknolojia na mashine zenye kuongeza ufanisi katika shughuli zake.

So inakuwa ni bora kuwa na large plantation mf ekari 45 000 ambazo ziko chini ya kampuni moja kuliko kuzigawa ekari hizo kwa wakulima 15 000.

Kampuni moja kubwa inaweza kushusha gharama za uzalishaji to the minimum kwa kutumia mashine na teknolojia.
Pia kampuni moja kubwa inaweza kucover cost za R&D kwenye kilimo unlike 15 000 peasants.
 
Asante mkuu Aba,mie ni mwanafunzi najifunza kwenu..please msichoke kutoa elimu...thanks again,,,lol
 
Angalia namna machine hizi zinavyofanya kazi ya upandaji iwe rahisi na yenye ufanisi wa hali ya juu. Je mashine hizi anaweza kumiliki mkulima mmoja??
Au ndo watu wamiliki kupitia ushirika ambao kuna ubadhirfu (rejea KNCU na vyama vingine vya ushirika)
Rebeca 83

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea kilimo. Nchi zote hujitoa kwenye kutegemea kilimo ili ziwe na maendelea halisi ambayo ni ya viwanda.
Hivyo viwanda mnatengenezea malighafi kutoka wapi ?
 
Kutegemea kilimo maana yake siyo kuacha kulima. Maana yake ni sector gani ina part kubwa kwenye GDP?
Nchi ambazo kilimo ni part kubwa kwenye GDP au kinaajiri watu wengi kuliko sector yeyote, nchi hiyo ni masikini.
Kwa hiyo industrialization maana yake ni kuondoa kilimo kama mtoa ajira mkuu au kama sehemu kubwa ya uchumi.
Hapo ndiyo utakapo pata maendeleo ya haraka.
Naona mkuu kilimo una kitafsiri kwa sura nyepesi sana!

Kilimo ukikitafsiri kwa namna waliopitia wenzetu, ni pale unapoichukua mbegu ukaiweka shambani then ukaifanyia postharvesting through food chain operation to the table for consumption hapa tutatoka kupitia kilimo!

Unajenga kiwanda cha nguo bila kulima utakilisha nini iko kiwanda?

Kiwanda cha mafuta ya alizeti, mzulia na magunia bila katani kitafika wapi?
Tomato sosi bila kulima nyanya utafika?

Kilimo kipewe msaada mkubwa na kwa upana wake kisiishie kwenye production kiende hadi kwenye value addition( processing).
 
Elimu Elimu Elimu Elimu ndio Ufunguo wa kilakitu hata choo cha kuflash usipo mfundisha jinsi ya kutumia itakuwa shida
 
Elimu tukumbuke walio asisi Ifunda tec Mtwara Mosh Agricultural Kibaha,Shybush, Commercial schools Mawenzi DomSec Vurugu schools Kibohehe Charismatic Schools Morogoro Luth jrn sem Vichochoroni schools ntamalizia kesho Ukweli ukiweka vizuri Elimu itaziba mianya yote
 
Naona mkuu kilimo una kitafsiri kwa sura nyepesi sana!

Kilimo ukikitafsiri kwa namna waliopitia wenzetu, ni pale unapoichukua mbegu ukaiweka shambani then ukaifanyia postharvesting through food chain operation to the table for consumption hapa tutatoka kupitia kilimo!

Unajenga kiwanda cha nguo bila kulima utakilisha nini iko kiwanda?

Kiwanda cha mafuta ya alizeti, mzulia na magunia bila katani kitafika wapi?
Tomato sosi bila kulima nyanya utafika?

Kilimo kipewe msaada mkubwa na kwa upana wake kisiishie kwenye production kiende hadi kwenye value addition( processing).
Wewe sasa ndiyo unatafsiri kilimo kwa sura nyepesi mno.
Unaposema value addition, hapo ndipo unapozungumzia manufacturing.
Usitegemee mkulima mwenzako akutengenezee kiwanda cha mazulia au tomato sauce. Utabaki kuuza surplus nje na kununua finished products.
Ila ukiwa na maseremala kama wa keko fenicha, au wachonga vinyago wenye workshop kubwa, machine za kufanyia kazi za kisasa na mafunzo ya kuendeleza ueledi pamoja na kuwatafutia masoko, basi hata siku mona hutauza mininga, mipingo na mazao mengine ya miti yetu bora.
Bali, utauza fenicha nchi za Comoro,Kenya,Uganda n.k kwa sababu tuna ardhi kubwa na misitu mingi ambayo nchi nyingi haziwezi kushindana na sisi. Uwepo wa viwanda vikubwa vya fenicha hapa Tanzania, kunachochea sisi kutouza nje mazao yetu na siyo vice versa.
Kuuza nje bidhaa zetu na siyo mazao yetu. Ka hiyo sekta binafsi ipewe incentives za kuanzisha viwanda na tuondoe workforce kutoka kwenye kilimo. HII NI LAZIMA ILI TUENDELEE.
 
hata sijui mkuu,naona hili wazo liepingwa vikali,

mie I just think tukiwekeza kwenye kilimo,

kutakua hakuna unemployment,

na kama hakuna unemployment then serkali inaweza kudirect resources zake kwingine including kujenga viwanda…

swala la tunahitaji wakulima wachache sioni kama liko sahihi,yaani uwajaze watu viwandani wakufanyie kazi,instead wangelima na kujilisha na mengine ndio wakulete kiwandani.???.hili jambo mmelichukulia too general..labda hatutaona positivity at national level ila uchumi wa mmoja mmoja wetu atainuka …kama tukitilia mkazo

second viwanda vitahitahi skilled labour na machinery sasa hivi uki compare na kilimo kipi chepesi na achievable?

Again,UZALSHAJI lazima uwe maximum ndio twende viwandani,sasa kama wakizalisha/lima kidogo utafanyia nini hizo machine???uzalishaji lazima uwe at Maximum sad it means kilimo ndio kianze kwanza...kikishafika maximum or optimum level ndio viwanda vijengwe....

Rebeca83, iko hivi: hata huko ulaya kwenye mashamba makubwa ya wakulima wachache, palikuwepo pia wakulima wadogo hapo zamani, hata kama hawakuwa wa kilimo cha jembe la mkono tunalolijua sisi. Rudi tu miaka hamsini nyuma, hata hapo Marekani walikuwepo, na pale China wakulima hao bado wapo, hata ukiangalia movie zao utawaona wakipandikiza mpunga, tena kwa mikono. Hivyo hivyo hata Korea ya kusini. Uingereza, wadogo kabisa walikwisha siku nyingi zaidi, lakini hata leo wapo wa kati (sio wadogo sana na wala sio wakubwa).

Kilichotokea, ni kwamba kadri ya maisha ya watu yalivyozidi kuwa mazuri, na watoto wengi wakawa wanapata elimu, wengi hawakurudi tena kwenye familia zao kuendelea na kazi za kilimo. Wengi wakawa ni wafanya kazi mbali mbali mijini. Hizo kazi hazikuwa kwenye viwanda tu, lakini unajua sehemu nyingi watu wenye ujuzi wao wanakoajiriwa, ikiwa of course hata kwenye viwanda.
Hawa wazee waliobaki mashambani, siku zao zilipofika, au kwa kuishiwa nguvu kutokana na uzee, kazi zao za kilimo zilikoma. Watoto hawakurithi majukumuhayo. Sasa kama kilikuwa ni kishamba chenye tija, wanunuzi walinunua na ku-consolidate kwenye mashamba mengine na kuwa biashara kubwa ya kilimo.
Jameni, kwani hata sisi hapa yanayotokea tayari hamyaoni? Utanisamehe Rebeca83, lakini nakuona kama vile umekwishaonja maisha ya mjini na kunogewa. Sidhani kama unao mpango wowote wa kurudi kijijini kwenu kuendeleza kilimo kile alipoishia babu na bibi. Na kama utabahatika kupewa urithi ule, nina uhakika zaidi ya 50%, kishamba kile utakipiga bei. Tungekuwa tumekwishafikia hatua ya 'consolidation', nina hakika ungefuatwa haraka sana na wanunuzi wanaopanua sehemu zao za kilimo.

Lakini pamoja na hayo yote, kwa mawazo yangu binafsi, Tanzania bado tutaendelea kuwa na wakulima wadogo wadogo kwa muda mrefu kidogo. Hawa hawatatoweka miaka 10 au ishirini ijayo. Kwa sababu watu wetu wengi bado maisha yao yako vijijini.
Kwa hiyo basi, ili hawa watu tuweze kuwasaidia kwa bidii zao nyingi wanazozifanya, serikali haina budi kuweka kilimo kiwe kipaumbele cha kudumu, kikiungana na Elimu.
Maana yangu hapa ni kwamba wakulima hawa wawe na uwezo wa kilimo cha kuzalisha mazao mengi zaidi katika hivyo vishamba vya ekari 5, 10, hata 50, maradufu ya mazao wanayopata sasa hivi. Hili litakisaidia kizazi hiki cha wakulima kujipatia kipato zaidi, nyumba nzuri, watoto shule, afya, n.k..
Hiki kizazi kitaendelea kupungua mwaka hadi mwaka, na Tanzania itapata maendeleo kwa kasi zaidi (I hope haitakuwa Haiti) na kuwa na viwanda inavyotaka kuwa navyo. Na hawa vijana waliotoka vijijini wasiopenda kwenda huko tena, watakuwa na elimu ya kutosha kufanya kazi viwandani, na kwingineko. Hawarudi tena kwenda kuendeleza kishamba cha babu.

Sitaki uchoke kusoma. As for "kutakuwa hakuna unemployment" - hata tukiagiza wafanya kazi wa shambani kutoka Kenya, as for Mexico to USA- bado unemployment to some people will always be a fact of life. I hope you understand what I mean. Hivi Saudi kuna 'unemployment?
 
Back
Top Bottom