Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

hapana lawama ianzie kwa system nzima ya uongozi wa serikali yetu imetugawa kimakundi wenye nacho na wasio nacho na inawakumbatia wenye nacho ndio maana wasio nacho wanachukua sheria mkononi migogoro ya ardhi haijaanzia jana tegeta ni ya kihistoria kwann wanashindwa kuitatua?kila mtu akapata haki yake?
LAWAMA SI ZA JESHI LA POLISI..... wahusika walioanza kupigana ndo lawama ziwaendee
 
Hao Polisi waliopewa taarifa wakasema "Ngoja wauane wote kwanza..." wawekwe ndani na kufunguliwa mashitaka, Pia mabosi wao (Kova, Mwema, Nahodha) nao wawajibishwe kutokana na uzembe huu!
 
LAWAMA SI ZA JESHI LA POLISI..... wahusika walioanza kupigana ndo lawama ziwaendee
lawama ziende kwa anayedai kumiliki eneo kutotumia mihimili husika kufikia muafaka.
Think of wabomoe nyumba yenu from no where, no details/no maelezo kabla
Ningekuwa karibu na eneo ningechochea fujo ile mbaya na ningemwagia mtu petrol na kumchomea mbali.
 
jamani hii ni tanzania au imekuwa rwanda sasa? jmani serikali ipo kweli na inayaona haya?

mambo haya yanapotokea, wanasiasa wasiendelee na kauli zao za 'tanzania nchi ya amani'. wanayodhani hayawezi kutokea tanzania yanawezekana kabisa, as long as wenye njaa wanaonewa na kunyanyaswa. ipo siku wanasema basi!!!

R.I.P.
 
Mmmm,hayo ndiyo matatizo ya kutokuwepo kwa utekelezaji wa sheria,hivyo kila mtu anatumia nguvu alizo nazo,watu wamekufa what for hawawezi rudi so,utandeji mbovu hili si la jana wa juzi
 
twende mbele turudi nyuma haya ni mazao ya uozo uliokithiri huko wizara ya ardhi. Rushwa na kutofuata taratibu ndio order of the day hapo wizarani. Tanzania tunaelekea kubaya, ubaya wa rushwa huo sasa unajidhihirisha!!
 
mambo haya yanapotokea, wanasiasa wasiendelee na kauli zao za 'tanzania nchi ya amani'. wanayodhani hayawezi kutokea tanzania yanawezekana kabisa, as long as wenye njaa wanaonewa na kunyanyaswa. ipo siku wanasema basi!!!

R.I.P.
u hv spoken ma mind.i swear pamoja na kuwa mwanamke lakini ningekuwepo ningemchoma mtu moto.Ningetoa petrol kwenye gari haraka haraka ningemlipua mtu.Hii nchi habari za majadiliano zimefeli kilichobaki mabavu tu.
 
kwani kazi kubwa ya wizara ya ardhi ni nini?
lawama ziende kwa anayedai kumiliki eneo kutotumia mihimili husika kufikia muafaka.
Think of wabomoe nyumba yenu from no where, no details/no maelezo kabla
Ningekuwa karibu na eneo ningechochea fujo ile mbaya na ningemwagia mtu petrol na kumchomea mbali.
 
Bila kujali chochote kile.

Kutoa uhai wa binadamu mwenzio kwa sababu yoyote ile ni UKATILI.

MUNGU awalaani na kuwasamehe WAUAJI hawa. Na wakamatwe wakajibu mashtaka kwenye vyombo vya haki.....Unawezaje kumuua binadamu mwenzio namna ile kisa ardhi/mali?

I wish ningeelewa vizuri hili tukio.....
 
u hv spoken ma mind.i swear pamoja na kuwa mwanamke lakini ningekuwepo ningemchoma mtu moto.Ningetoa petrol kwenye gari haraka haraka ningemlipua mtu.Hii nchi habari za majadiliano zimefeli kilichobaki mabavu tu.

hapo kwenye red&bold:

baby unachanganya mada. hakuna ushahidi wowote kuwa wewe ni 'ke'
 
hayo ndio matokeo ya dhuruma wananchi wameshachoshwa kwakuwa serikali yao haiwajali na kuwatetea sasa wameamua kujitetea wenyewe...:rip:CCM.
 
LAWAMA SI ZA JESHI LA POLISI..... wahusika walioanza kupigana ndo lawama ziwaendee

Kazi ya Polisi ni nini?.....mimi najua CROWN katika kofia zao ina slogan hii USALAMA WA RAIA.....Watoto wako wakipigana wakaumizana na wewe ukiwepo utasema lawama sio yako?:disapointed:
 
Inasikitisha sana sana! Hata kama huyo anayedai kuwa hiyo ni ardhi yake na imevamiwa na wananchi, hakutakiwa kuidai kwa njia hiyo ya kuwavunjia wananchi nyumba zao! Kitendo cha kuvunja nyumba kiliamsha hasira kwa wakazi na kuona liwalo na liwe!

Hasira yangu ni kwa jeshi la polisi. Wanajibu kuwa "waache wauane akibaki mmoja atakuja kutoa taarifa". Fikiria ingekuwa ni wanafunzi wamegoma au wanaandamana kuelekea ofisi ya mkubwa fulani, vifaa vyote vya kutuliza ghasia vingetolewa ghalani!
 
Ndio tumechoka lakini is too much...Kitendo walichofanya hawa mabaunsa hakikua cha kiungwana,na kitendo cha waliowaleta pia hakikua cha kiutu hasa ikizingatiwa yangeweza kutokea km yaliyotukia!....kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi nacho ni cha kikatili na kisichokua cha kiutu! Yatosha sasa kusema mamlaka zote zinazohusika kwa namna moja ama nyingine katika hili sakata kutoa taarifa za kushindwa ili tujue pa kukimbilia pindi yakitufika!

Kwa hiyo wewe ulitaka wananchi wakae tu wakichekelea kuona nyumba zao zikibomolewa huku kesi ikiwa bado iko mahakamani? Jaribu kufikiria kama nyumba uliyoijenga kwa kudunduliza kwa zaidi ya miaka 30, tena pengine baada ya kupata kiinua mgongo cha kustaafu inabomolewa kirahisi namna ile. Ingekuwa wewe ungefanyaje?
 
Mwanzo nilikuwa ninachukulia hii habari kama nyingine ila baada ya kuona hii clip nimeshawishika kuwa hii ni habari kubwa na nyeti sana kwenye ustawi wa public safety kwenye nchi yenye Govt for the people by the people hasa ukiangalia mlolongo wa matukio

  1. Mabaunsa 400 wameletwa na Kampuni ya udalali kuvunja nyuma bila kumtafuta mwenyekiti wa mtaa na kuomba ulinzi wa vyombo vya dola wakati wa utekelezaji, kama walikuwa na haki ya kufanya hivyo
  2. Mwenyekiti wa mtaa na viongozi wanawasiliana na vyombo vya dola kwa lengo la kuepusha maafa lakini, kwa jeuri na uzembe wa hali ya juu hasa kwa kujua hawakuitwa na kiongozi wa juu wa serikali kulinda masilahi ya CCM basi wanaona kuwa maisha ya binadamu wengine is useless
  3. Polisi wanatoa kauli za dharua wakati wa dharula kuwa acha wananchi wauane na wa mwisho atakuja kuripoti polisi, hii ni kauli inayoweza kufanya wizara nzima inayohusika na usalama wa raia kuvunjwa na kuundwa upya katika nchi za demokrasia ya kweli na zenye kulinda masilahi ya wananchi. Isipofanya hivyo uchaguzi ujao inakuwa ni issue kubwa ya kupoteza kura
  4. Watu watano wanapoteza maisha hapo ndipo tutakapoona Full force ya kamatakamata kwa lengo la kujikosha na ku-sucrifice polisi aliyejibu utumbo kwa kumuhamishia sehemu ingine.
My Take: Hili suala linatakiwa kuondoka na Askari wote waliopigiwa simu kuwa kuna ugomvi, yaani kuanzia Mwema, Kova na wengine wote wa upande wa mawasilino. Pia kwa upande wa wanasiasa waziri muhusika anatakiwa kuwajibika kwa makosa ya askari wake ili kuongeza public trust

Waliouwawa ni mabaunsa ambao kwa jinsi inavyooneka wengi wao ni jobless ndiyo maana wakawa tayari kurisk maisha yao kwa ujira wa Tshs 50,000. Kundi hili ni lazima litakuwa linajumuisha wavuta bangi na vibaka. wasiwasi wangu ni kuwa kwa wale waliopona na kukimbia wanweza kuwa na moyo wa kulipiza kisasi kwa kupoteza wenzao watano na kuamua kuvamia mivumoni usiku wa manane kutoa kibano cha haja kwa mkazi mmojammoja hasa wale waliowa identify kuwa ni frontliners. Hapa busara itumike hasa kuwapoza mabaunsa waliosalia kwani nina hakika kuwa aliyewaleta anawafahamu. Upande mwingine ni kuwa aliyewaleta nae anaweza kugeukwa na mabaunsa hawa baada ya kuwapeleka machinjioni na kuwakimbia.

Nina hakika kabisa kuwa kama KOVA angepigiwa simu kuwa CHADEMA wanaandamana bila kibali basi isingechukua dakika kumi na tano kwa magari FFU waliosheheni silaha zote nzito kufika eneo la tukio kuwavurumusha ili apate credit kwa viongozi wa CCM
Jamani Ndg Zangu Watanzania wapendwa, tumeisha sema mara nyingi ili kuondoa migogoro yote ya umiliki wa aridhi lazima tuwe na katiba mpya. Huwezi kusema aridhi ni mali ya taifa ili inufaishe mafisadi wawadhurumu watu walioishi kwenye hiyo aridhi tangu enzi za mababu!!!!!!!!! Katiba italitazama swala la aridhi ili liwe na msingi mzuri wa kunufaisha waliopo kwenye eneo lao!!!!!!! Aridhi ni mali ya taifa watu wamezikwa wazima wazima Nyarugusu, Tundu Lisu na wanaharakati wengine wamefatilia saana swala hili, na haki bado kupatikana shauri ya katiba legelege. TUNAHITAJI KATIBA MPYA ILI TUWEZE KUONDOA MIGOGORO YA ARIDHI ILIYOPO TAIFA LISIINGIE KWENYE UANGAMIVU!!!!!
 
Back
Top Bottom