Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Zaidi ya watu 5 wamekufa ktk mapigano ya kugombea ardhi kati ya wananchi na mabaunsa wa kampuni ya udalali ya Mwangata huko Mivumoni Tegeta. RADIO1 STEREO

Grabbed_Frame_1.jpg

Grabbed_Frame_2.jpg

Grabbed_Frame_4.jpg

02+%25281%2529.JPG


 
Last edited by a moderator:
Kuna mapigano ya ardhi Tegeta watu 5 wamekufa na majeruhi ni wengi.
Source ITV
 
Jamani wasije wakawa wanagombea ka kikawanja kangu pale jirani na Nyamachabes
 
ndio nasikia hapa hiyo habari....mwee....tumeanza kufikia huko Watanzania.....
kweli kidogo kidogo ndio mwendo.....nasikia wameshtaki polisi, polisi wakasema acha wauane wamwisho ndio apeleke taarifa......
mabaunsa wanawakaba wanahabari na kuwanyang'anya usafiri.......
KUMEKUCHA.....
 
Hivi sasa kuna mapigano yanaendelea Tegeta na kuna watu wapatao watano wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kisa ni kupigania ardhi.

Source: ITV live now
 
Kule walikovunjiwa nini? MUNGU atuepushe na kadhia hii
 
Kuna mapigano ya ardhi Tegeta watu 5 wamekufa na majeruhi ni wengi.
Source ITV

Hiyo ndiyo fainali ya serikali legelege. Watajitokeza na machozi ya mamba. Nawaunga mkono wanaojitetea kwa kupinga uporaji unaofanywa na wenye ubia na serikali legelege. HIYO NDIYO AMANI NA UTULIVU WANAOUIMBA
 
Mapigano makali yametokea leo kuanzia saa 3 huko Mivumoni Tegeta watu zaidi ya 5 wamekufa baada ya mabaunsa wa kampuni ya udalali ya mwangata kuvamia na kuvunja nyumba za wakazi. Wengi waliokufa ni mabaunsa. Polisi walipoitwa wakasema waache wananchi wauane wa mwisho atatuletea habari.....

source Radion one breaking News na pia nimepita huko wazo saa 6.30 hivi.
 
Hiyo ndiyo fainali ya serikali legelege. Watajitokeza na machozi ya mamba. Nawaunga mkono wanaojitetea kwa kupinga uporaji unaofanywa na wenye ubia na serikali legelege. HIYO NDIYO AMANI NA UTULIVU WANAOUIMBA


Serikali ya Kikwete. Nyumba 26 za waathirika wa mabomu zinajengwa kwa gharama ya sh.96, 000, 000 zote pamoja.
 
Jamani wasije wakawa wanagombea ka kikawanja kangu pale jirani na Nyamachabes

Kumbe Nazjaz ni jirani yangu...inakuwaje siku zote hizi sijakuona nyamachabes?! Ngoja niangalie avatar yako uzuri!
 
Hali ni mbaya sana maiti zimetapakaa mashambani kama zile za Genocide kule Rwanda. Wengine wamevunjwa viungo wame lala tu wanasubiri kufa. Huwezi amini kama ni Tanzania tena Dar es salaam karibu na makao makuu ya vyombo vyote vya usalama. Tajiri mmoja amesababisha roho za watu kupotea. JAMNI WATANZANIA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom