watu wanapoteza muda na wimbo wa AMANI, tengenezeni justice system inayofanya kazi, mtu akienda kinyume na sheria ANASHUGULIKIWA.
sasa hivi hakuna sheria TANZANIA, kama huna "connection" au hela hupati kitu, hata kilicho chako unanyang'anywa. Na wananchi wengi wanalijua hili.
Mnataka hawa wananchi wa Tegeta wafanye nini? mtu anaishi na familia yake kwenye nyumba yake , alioijenga kwa jasho lake, unataka kuja siku mmoja umtoe, alafu familia akailaze wapi? tena zaidi ya hapo wamepiga simu polisi lakini polisi wamekataa kwenda. Serikali haijali kama fujo hazitishiii utawala wake. Pale UDSM wanafunzi hata nje ya compound hawakutoka, FFU wakaanza kuwapiga na kuzuia maandamano yao. Sasa unataka huyu mwananchi wa Tegeta anyanyaswe kiasi gani na wananchi wenzake, polisi na mahakama hadi achukue hatua.
Tu focus effort yetu kuhakikisha haki inapatikana, mtu akileta fujo tunatumia sheria iliopo na kutoa hakumu kwa HAKI. Watu wataona hata aibu kufanya haya mambo.