Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

Inasikitisha sana sana! Hata kama huyo anayedai kuwa hiyo ni ardhi yake na imevamiwa na wananchi, hakutakiwa kuidai kwa njia hiyo ya kuwavunjia wananchi nyumba zao! Kitendo cha kuvunja nyumba kiliamsha hasira kwa wakazi na kuona liwalo na liwe!

Hasira yangu ni kwa jeshi la polisi. Wanajibu kuwa "waache wauane akibaki mmoja atakuja kutoa taarifa". Fikiria ingekuwa ni wanafunzi wamegoma au wanaandamana kuelekea ofisi ya mkubwa fulani, vifaa vyote vya kutuliza ghasia vingetolewa ghalani!
Katiba mpya ndilo jibu halisi la kuondoa hii migogoro inayolikabili taifa letu.Migogoro ya Aridhi. Tutaidai hata kwa mabavu kama serikali ya Kikwete haitaki kusikiliza madai yetu dalili zimeisha anza kujionyesha!!!!!!
 
Mpiga picha na mtangazaji wana roho za ngumu ... yaani wanapiga picha wanahoji badala ya kutoa huduma ya kwanza! Ndivyo mnavyofundishwa huko vyuoni kwenu?

Wamefundishwa kutoa habari sio huduma ya kwanza.
Wasingefanya hivyo hata wewe usingepata hizi habari na usingaliandika hicho ulichoandika.
 
du mnasema tz kuna amani lkn ipo siki machafuko kama haya yatazuka nchi nzima tusipokuwa makini:Cry:
 
ndio nasikia hapa hiyo habari....mwee....tumeanza kufikia huko Watanzania.....
kweli kidogo kidogo ndio mwendo.....nasikia wameshtaki polisi, polisi wakasema acha wauane wamwisho ndio apeleke taarifa......
mabaunsa wanawakaba wanahabari na kuwanyang'anya usafiri.......
KUMEKUCHA.....

... vijana waliokata tamaa wamejaa JAZBA la hali ya juu. Nafananisha haya matukio mengi ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao kama HIFADHI KUBWA YA PETROLI ambayo ikiwashwa tu, MOTO wake utaunguza sana. Nchi iko pabaya sana kama matukio ya namana hii yanavyoashiria. Tahadhari ichukuliwe na waliochakachua haki za wananchi kwamba wakiendeleza UDHALIMU WAO, basi nchi hii itafika pabaya mno. Hakuna ulazima wa kujaribu kuona nguvu ya umma inaweza kufanya nini.
Tukio la jana limeniacha hoi. Tanzania ya Mwalimu imefikishwa huku?
 
NIlisha wai kusema huku Jamvini9 kuwa iko siku WATANZANIA WATASEMA WAMECHOKA NA BALAA LAKE MTALIONA sasa hii ni dalili ya kuchoshwa na mafisadi wanao kubatiwa na Serikali, Hebu jiulizeni kwaniani POLISI walipopigiwa simu walijibu vile kuwa "Waacheni wauwane atakaye pona aje kutoa ripoti" hii inamaanisa kuwa POLISI watanzania nao Wamechoka kutetea Mafisadi wanao zulumu wanyonge haki zao.

JK na watu wako kaeni chini mjipange upa TANZANIA ya leo sie ile ya Enzi za Mwalimu!!! Watu wamechoka kila kona mapigano ukija kwenye katiba vurugu, ajira vurugu watu wakijiajiri wenyewe wanavunjiwa vibanda vyao wanaibiwa mali zao, haya imeamia kwenye ardhi sasa bado safari ndefu tunayo mbele, hebu kaa chini ufikirie mara mbilimbili unaipeleka wapi hii Nchi.

Mwenyezi mungu azirehemu roho za hao marehemu na awaponye majerui wote kwani wao walikuwa wanapigania chakula cha watoto wao!
Kweli ina uzunisha sana!
 
Nimesikiliza Clouds FM wakimuhoji mjumbe wa nyumba Kumi wa eneo hilo
anasema walikuta vichaka wakafyeka na kujenga na hawajui ardhi ni mali ya nani
je ni halali kufanya hivyo bila utaratibu? kwa sentensi hiyo ni wavamizi?
serikali inatakiwa kuwahoji wananchi wa eneo hilo ili kupata ufafanuzi zaidi
pia kujua waliokwenda kubomoa majengo walitumwa na nani?
 
Inasikitisha sana, lakini inaonyesha hali halisi ilivyo katika nchi yetu kwa sasa, utawala wa kufuata sheria sasa umewekwa pembeni, watu wamekuwa na kiburi na jeuri ya madaraka na pesa, wao wanafikiri wanaweza kufanya chochote na wananchi hawatafanya kitu, hili lililotokea Tegeta ni fundisho kwa wizara iliyojaa ubabaishaji na rushwa ya Ardhi, kuna mambo mengi yanakuja, hasa pale wananchi wanapotegemea waziri husika atakuwa na maamuzi ya busara ya haraka lakini anakuwa mbabaishaji, kweli ndani ya CCM hakuna msafi yaani hata mama Tibaijuka na yeye anaelekea kushindwa!?, Kaja kwetu huku Kigamboni kafanya mkutano na wanchi, anaeleza mambo ya kuwafurahisha wananchi eti anawaomba viongozi wakazungumze na wanachi ili wakubaliane jinsi ya kulipa fidia kupisha mradi unaosemekana kuja, lakini anatoka hapo anakwenda halmashauri ya wilaya anatia sign kuidhinisha malipo yaendelee kwa wananchi!, sasa wewe umeagiza watu wakaelewane kwanza! huku unawapa rungu halmashauri waendelee na zoezi maana yake nini! sio kuleta uvunjifu wa amani kweli! wananchi wanapinga fidia inayotolewa haiendani na thamani ya ardhi kwa sasa, tena na utaratibu unaotumika ni wakitapeli tu, sasa huyu waziri wa ardhi kweli anania ya kutatua kero za wananchi?

Viongozi wetu mmeshindwa kazi, Chadema twende sasa kazi ndio kwanza wanachi wameianza.
 
Mpiga picha na mtangazaji wana roho za ngumu ... yaani wanapiga picha wanahoji badala ya kutoa huduma ya kwanza! Ndivyo mnavyofundishwa huko vyuoni kwenu?
kwahali ilivyokua mbaya hata hao wapigapicha na waandishi wa habari wangejaribu kutoa hiyo huduma yakwanza nawao wangepigwa nahata kuuwawa hali ilikua mbayasana kwamujibu wa picha tulizoona kupitia itv ilikua ni vita kamili kwakutumia silaha zajadi,wakulaumiwa hapo ni polisi walioitwa nawakakataa kwenda eneo latukio na si waandishi wahabari wakulaumiwa.
 
Hiyo ndiyo fainali ya serikali legelege. Watajitokeza na machozi ya mamba. Nawaunga mkono wanaojitetea kwa kupinga uporaji unaofanywa na wenye ubia na serikali legelege. HIYO NDIYO AMANI NA UTULIVU WANAOUIMBA
Eee Mungu tusaidie Tanzania. Tunaomba uwafanye wote waliopata kikombe kwa babu wauchukie ufisadi, wasiwe na tamaa ya mali na waichukie siasa na wajitoe katika uongozi wa siasa....... Eee mungu tukubalie maombi yetu
 
Hebu tujuze zaidi kuhusu hayo mauaji ya Tegeta, waliokufa ni waliokodiwa kubomoa au wananchi waliovamiwa na hao wapuuzi?
 
Inasikitisha sana sana! Hata kama huyo anayedai kuwa hiyo ni ardhi yake na imevamiwa na wananchi, hakutakiwa kuidai kwa njia hiyo ya kuwavunjia wananchi nyumba zao! Kitendo cha kuvunja nyumba kiliamsha hasira kwa wakazi na kuona liwalo na liwe!

Hasira yangu ni kwa jeshi la polisi. Wanajibu kuwa "waache wauane akibaki mmoja atakuja kutoa taarifa". Fikiria ingekuwa ni wanafunzi wamegoma au wanaandamana kuelekea ofisi ya mkubwa fulani, vifaa vyote vya kutuliza ghasia vingetolewa ghala
 
Nimesikiliza Clouds FM wakimuhoji mjumbe wa nyumba Kumi wa eneo hilo
anasema walikuta vichaka wakafyeka na kujenga na hawajui ardhi ni mali ya nani
je ni halali kufanya hivyo bila utaratibu? kwa sentensi hiyo ni wavamizi?
serikali inatakiwa kuwahoji wananchi wa eneo hilo ili kupata ufafanuzi zaidi
pia kujua waliokwenda kubomoa majengo walitumwa na nani?

mimi hapa nailaumu serikali, inge invest kwenye ELIMU watu wangejua nini cha kufanya, wewe watu wengi Tanzania hii wanaishi maporini/vichakani hata huduma ya hospitali hawapati sasa unataka leo waanze kutafuta ofisi za ardhi nakutaka kujua nani mmiliki wa ardhi ? inakua ngumu sana, na hawa watu nawapongeza maana walianzia polisi , lakini serikali kupitia polisi wake ikawaangusha na kukataa kuwasaidia, lakini cha ajabu zaidi ,POLISI WALIWAPA HAWA WANANCHI MAELEKEZO YA NINI CHA KUFANYA, maelekezo hayo ni kwmaba wakachinjane , atakeyebaki aje atoe taarifa, sasa kama serikali kupitia chombo chake kinatoa tamko wananchi wanatii alafu mnawalaumu wananchi wakati agizo zenyewe lina wa favour hao hao wananchi.....

Mimi nakuhakikishia huyo polisi aliyetoa hayo "maagizo" angekua na elimu ya maana hasinge sema aliyosema......
 
Sheria ianze kwa huyu Dalali Mwangata maana yeye ndio chanzo cha vifo vyote na majeruhi hao, maana hata kama alikuwa na kibali halali alitakiwa afuate sheria na taratibu zote, alitakiwa apeleke list yenye majina ya nyumba za kubomoa pamoja na barua ya mahakama ikimruhusu yeye kuvunja nyumba hizo vitu hivi vyote alitakiwa kupeleka kwa mwenyekiti wa kijiji ama mjumba wa nyumba kumi lakini hakupeleka vielezo hivyo, pia alitakiwa apitie kwenye kituo cha POLISI kwa ajili ya msaada wa ulizi hakufanya hivyo, tatu jana ilikuwa ni sikuya mapumziko ya kitaifa hakuna ofisi ya serikali iliokuwa iko wazi sasa yeye atafanyaje kazi kama hiyo wakati sio siku ya kazi kwa maana moja ama nyingine amejichukulia sheria mkononi kisa pesa alizopewa na mafisadi matokeo yake damu imemwagika juu yake. 😡
 
Serikali kupitia chombo chake cha dola, polisi ndio walihalalisha mauaji ya Tegeta.
Wananchi walipo omba msaada polisi kwa njia ya simu na kisha kufika kituoni, polisi walitoa maagizo ya kwamba wakachinjane, atakae baki ndio aje atoe taarifa.

SOURCE ITV NEWS

Mwenyekiti wa Serikali za mitaa Bw Deogratius Kamugisha amesema ofisi yake iliwasiliana na jeshi la polisi hawakupata Msaada.
Wakampigia Said Mwema, Said Mwema akaambia wampigie Kova, Kova akasema analeta polisi.
Wananchi wakaona haitoshi, wakamtuma mtu (Ali Mgulu) aende polisi moja kwa moja kuomba msaada, Ali lalipofika polisi kuomba msaada akajibiwa na polisi "ngoja wakaune alafu huyo wa mwisho atakaye pona aje atoe taarifa" na Diwani aliingia wakati polisi wanatoa hayo matamko.
 
Serikali kupitia chombo chake cha dola, polisi ndio walihalalisha mauaji ya Tegeta.
Wananchi walipo omba msaada polisi kwa njia ya simu na kisha kufika kituoni, polisi walitoa maagizo ya kwamba wakachinjane, atakae baki ndio aje atoe taarifa.

maneno mazito hayo mkuu. natamani uweke uthibitisho, au unyamaze tu tuendelee kuomboleza.
 
Whatever, the reason is, this act of killing others is bad. Hii ni ulaji wa nyama ya watu na haitaishia hapa! It is bad indeed!!!
 
Serikali kupitia chombo chake cha dola, polisi ndio walihalalisha mauaji ya Tegeta.
Wananchi walipo omba msaada polisi kwa njia ya simu na kisha kufika kituoni, polisi walitoa maagizo ya kwamba wakachinjane, atakae baki ndio aje atoe taarifa.

Hapa TZ tuna serikali au polisi? Ni wasanii na wasaka pesa na vyeo tu. Kama hujui subiri siku unapoibiwa na utajua kuwa polisi wako tayari kushirikiana na mwizi kuuza mali yako.
 
Back
Top Bottom