Mwanzo nilikuwa ninachukulia hii habari kama nyingine ila baada ya kuona hii clip nimeshawishika kuwa hii ni habari kubwa na nyeti sana kwenye ustawi wa public safety kwenye nchi yenye Govt for the people by the people hasa ukiangalia mlolongo wa matukio
- Mabaunsa 400 wameletwa na Kampuni ya udalali kuvunja nyuma bila kumtafuta mwenyekiti wa mtaa na kuomba ulinzi wa vyombo vya dola wakati wa utekelezaji, kama walikuwa na haki ya kufanya hivyo
- Mwenyekiti wa mtaa na viongozi wanawasiliana na vyombo vya dola kwa lengo la kuepusha maafa lakini, kwa jeuri na uzembe wa hali ya juu hasa kwa kujua hawakuitwa na kiongozi wa juu wa serikali kulinda masilahi ya CCM basi wanaona kuwa maisha ya binadamu wengine is useless
- Polisi wanatoa kauli za dharua wakati wa dharula kuwa acha wananchi wauane na wa mwisho atakuja kuripoti polisi, hii ni kauli inayoweza kufanya wizara nzima inayohusika na usalama wa raia kuvunjwa na kuundwa upya katika nchi za demokrasia ya kweli na zenye kulinda masilahi ya wananchi. Isipofanya hivyo uchaguzi ujao inakuwa ni issue kubwa ya kupoteza kura
- Watu watano wanapoteza maisha hapo ndipo tutakapoona Full force ya kamatakamata kwa lengo la kujikosha na ku-sucrifice polisi aliyejibu utumbo kwa kumuhamishia sehemu ingine.
My Take: Hili suala linatakiwa kuondoka na Askari wote waliopigiwa simu kuwa kuna ugomvi, yaani kuanzia Mwema, Kova na wengine wote wa upande wa mawasilino. Pia kwa upande wa wanasiasa waziri muhusika anatakiwa kuwajibika kwa makosa ya askari wake ili kuongeza public trust
Waliouwawa ni mabaunsa ambao kwa jinsi inavyooneka wengi wao ni jobless ndiyo maana wakawa tayari kurisk maisha yao kwa ujira wa Tshs 50,000. Kundi hili ni lazima litakuwa linajumuisha wavuta bangi na vibaka. wasiwasi wangu ni kuwa kwa wale waliopona na kukimbia wanweza kuwa na moyo wa kulipiza kisasi kwa kupoteza wenzao watano na kuamua kuvamia mivumoni usiku wa manane kutoa kibano cha haja kwa mkazi mmojammoja hasa wale waliowa identify kuwa ni frontliners. Hapa busara itumike hasa kuwapoza mabaunsa waliosalia kwani nina hakika kuwa aliyewaleta anawafahamu. Upande mwingine ni kuwa aliyewaleta nae anaweza kugeukwa na mabaunsa hawa baada ya kuwapeleka machinjioni na kuwakimbia.
Nina hakika kabisa kuwa kama KOVA angepigiwa simu kuwa CHADEMA wanaandamana bila kibali basi isingechukua dakika kumi na tano kwa magari FFU waliosheheni silaha zote nzito kufika eneo la tukio kuwavurumusha ili apate credit kwa viongozi wa CCM