Matukio ya namna hii ni matokeo ya kuwa na serikali isiyojali wananchi wake, hasa wa kipato cha chini. Hili linanifanya nihoji mambo kadhaa,
(a) Kama kweli kampuni ya mwangata ilipewa kibali halali cha kubomoa hizo nyumba, ilifwata utaratibu wa kuwa taarifu watu ambao wangebomolewa mapema ili wajipange na kutafuta makazi mengine?? narejea maneno ya JK kuhusu ubomoaji wa MAGUFULI , kwamba ikibidi mtu apewe hata miaka miwili ili ajipange na kupata makazi mengine.
(b) Hilo eneo lingekuwa limevamiwa na mafisadi na kujengwa manyumba ya kifahari, kungetokea hali kama hiyo?? au kwasababu wale waliojenga ni wanyonge ndio maana wakatendewa hayo???
(c) Msimamo mzima wa utendaji wa jeshi la polisi unabagua?? je ingekuwa wamepigiwa simu wakaambiwa CDM wanaandamana wange react on the same way?? na je jeshi la polisi ndio mwanzo wa machafuko Tanzania?? (1) CDM arusha, walipambana na raia wakawauwa (2) Mivumoni tegeta, wamepewa taarifa, wakazipotezea, watu watano wakafa......hii inaashiria nini??
(D) Mabaunsa kulipwa 50,000 na kukubali kujitoa mhanga na wengine kupoteza maisha kunaashiria nini?? Hali ngumu ya ajira?? kuwepo kwa vijana wengi wasiokuwa na ajira, na kwamba wako tayari kujitoa maisha yao kwa kipato kidogo?? watu hao ukiwapa 100,000 ukawaambia wakamtoe mtu roho watakataa??
(e) Je serikali yetu legelege itayafumbia macho matukio haya mpaka lini??
-Mbarali
-Karatu
-UDSM
-UDOM
-CDM Arusha
-Mivumoni
Na list inaendelea kubwa tu!
EE MUNGU TUSIKIE MAOMBI YETU NA UIEPUSHE NCHI YETU NA MAJANGA KAMA HAYA!