Mapenzi yanauma jamani

Mapenzi yanauma jamani

Dada wenzio kule IG wametoa ushuhuda kwamba ukinywa haja ndogo yako ukanuia kumsahau inatokea matokeo ndani ya siku mbili tu.
Hata mkojo wa nguruwe pia ni dawa ya kukufanya uzubae halafu usahau,maana unakuwa zoba.
 
Yaan nimeachwa kwenye mataa mapenzi yanauma jamani yaani nimekaa na huyu mwanaume kwa miaka mitano nimekataa wanaume kibao ambao alikua wanani-approach wakiwa na nia njema nahisi nimechanganyikiwa sielewi wapi pakuanzia.

Nimelia hadi sauti imekauka i regret the day i said yes to him. Wanaume shikamooni sikuwai kudhani kuwa alikua na mahusiano nje, kha nimepata life time lesson wanawake wa humu muwe macho hapa nawaza ningekua nimemzalia daaah ningekua na hali gani nahisi ningechizi.

Hebu wanajammii nishaurini ntamsahauje huyu maana naona kama siwez siku ya nne leo am not myself. Yaan kadiriki kumpa simu mwanamke wake mpya waniambie kuhusu uhusiano wao mapenzi yauma jamani najiuliza nina tatizo gani jaman jaman nitamsahauje huyu.........

Mnashauriwa kuweka ngumu kwenye kutoa papuchi, toa papuchi ukiolewa. Kuna wanaume ambao wanakuwa kwenye uhusiano wanajitambua, wanaona thamani ya mwanamke na wana huruma. Shida nyingine nyinyi dada zangu mnaona mkimnyima mwanaume ataondoka, mwache aende na ujue mwanaume anayekupenda daima atakuwa pamoja nawe.

Mwanamke anayebana anafikiriwa zaidi kuliko anayetoatoa.
 
poule,ata wanaume hua tunatendwa pia,,,ila pole sana tafuta marafiki wapya itakusaidia kupoteza mawazo
 
Hapana, mimi nimeshapata wangu wa ubani humu humu jukwaani, bado hatujaonana,lakini tushafanya tendo la ndoa mara nyingi sana.
teh teh sijui mlilifanyaje hilo tendo angali bado hamjaonana hiyo itakuwa miujiza mkuu
 
teh teh sijui mlilifanyaje hilo tendo angali bado hamjaonana hiyo itakuwa miujiza mkuu
Tuko karne ya 21,yaani KI DOT COM,AU KIDIGITALI,sisi tunafanya kitu inaitwa cybersex kielectroniki na tunatosheka na uvhovu juu.
 
Pole sana bibie, ila hakuna kitokeacho bila sababu kuna kitu utakuwa umemfanyia akaona hamuwezi kuendana. So bora kila mtu atafute watakayewezana japo nahisi atakuwa hajakuambia tatizo nini.

Kuna wanaume wengine huwa hatupendi kukomandiwa,kuendeshwa hata kupayukiwa na wenza wetu yawezekana ukawa na moja kati ya hayo.
Kuna wanaume hata umbembe mgongoni lakini hajui anachokitaka alafu ni ushamba kumuumiza mwenzio kwa kumpa mwanamke mwenzie aongee nae yaonyesha uyo kaka ndo tabia yake au hana confidence ya kujieleza maana ingekuwa vyema kama angemueleza tu personally mwenyewe
 
Pole sana dada. Ni kweli 5 yrs ni nyingi, but zitakuwa zimekuachia mafundisho mengi. Mungu ana makusudi yake. Utakuwa ok tu. Uambie moyo wako kuwa huyo sio wako tena and you need to mean it. Tulia kidogo...usianze mahusiano mapya haraka. Huhitaji kumkomoa au kuufanyia audit muonekano wako. Tumia muda wako mwingi kufanya vitu ambavyo ni productive na unavifurahia. Jitahidi kuwa bize. Usijiweke idle !!

Ila mbona hujatueleza sababu za kuachwa? Tueleze bana...ili ushauriwe vizuri na pia watu wengine wajifunze kutoka kwako. Lazima kulikuwa na viashiria fulani (red flags) kabla ya kuachwa rasmi. Labda kuna mambo kadhaa kitabia ambayo amekuwa akikulalamikia au kukushauri ubadilishe...mara kwa mara ?!!

Kwa bahati mbaya wanawake wengi wanapokuwa na wanaume/wapenzi wao kwa muda mrefu kiasi wanakuaga na tendency ya kuwa very comfortable na kuishi kwa mazoea. Hii imekuwa ikiathiri sana relationships nyingi.
 
Yaani kuna siku nilisha wahi kuachwa na demu nili data hadi nikamtafuta mwanasaikologia akanipa msaada japo msaada wake kwa kiasi flani ulinisaidia now na miaka 7 sijawah kuwa na mahusiano na mwanamke nikiwa na shida naenda ilala naende kuchukua mzingo wa buku mbili jero natulinza mtima wangu!

Ha ha ha..mkuu kuwa makini banaa. Hao wa buku 2 na jero sio hao. Anza tu upya kupenda. Tafuta tu wa kuunganisha naye vikojeleo huku afya yako ikiwa ni priority.
 
Ndo maana wanawake wajanja sasa hivi wanaangalia pochi hawaangalii Moyo, na ndio sababu wanaume mnaleta sana thread za kulalamika kupigwa mizinga ya pesa,Dada songa Mbele mimi nilishaachagwa na mtoto wa miez, jamaa akazaa na mwanamke mwingine tena ila hawakudumu hata miezi 6 inauma ila unakaza moyo sasa hivi nipo kwenye michakato ya ndoa na step Daddy wa Mwanangu maisha ni saafi, umelia vya kutosha sasa simama mpenz just Move on don't humiliate ur self Dear
 
Pole dada vaileth zainab wanaume hatuko hivyo kuna kitu utakua umemuuzi! Jikeep busy utamusahau tu, miaka mitano mbna kidogo sana mi nikajua mumezaliwa wote mkakua wote, fikiria kipindi hujamfahamu kwani uliishije.
Yaan nimeachwa kwenye mataa mapenzi yanauma jamani yaani nimekaa na huyu mwanaume kwa miaka mitano nimekataa wanaume kibao ambao alikua wanani-approach wakiwa na nia njema nahisi nimechanganyikiwa sielewi wapi pakuanzia.

Nimelia hadi sauti imekauka i regret the day i said yes to him. Wanaume shikamooni sikuwai kudhani kuwa alikua na mahusiano nje, kha nimepata life time lesson wanawake wa humu muwe macho hapa nawaza ningekua nimemzalia daaah ningekua na hali gani nahisi ningechizi.

Hebu wanajammii nishaurini ntamsahauje huyu maana naona kama siwez siku ya nne leo am not myself. Yaan kadiriki kumpa simu mwanamke wake mpya waniambie kuhusu uhusiano wao mapenzi yauma jamani najiuliza nina tatizo gani jaman jaman nitamsahauje huyu.........
Dada pole sana,yaliyokupata wewe yalinipata mimi,ingawa mie ni mwanaume.Yupo dada mmoja nilimpenda sana sana,na nilimkuta darasa la 7 nikamsomesha akafika diploma,nikampangia nyumba na nikamtafutia kazi,mie nina mke wangu wa ndoa yeye akawa nyumba ndogo.Tuliishi nae miaka 7 na kila nikimpa mimba anatoa,akaomba nimbunulie gari nikafanya hivyo na kila alichoomba nilijitahidi kumpa.Siku moja alinipigia simu akiwa na mama take mzazi na kuniambia nimkome na kwamba hana shida na mimi bali alikuwa na shida na hela zangu hivyo nisimjue tena.Nilisikia uchungu sana nikamjibu asante.Kila siku nilikuwa namuomba mungu anipe uwezo nimsahau na ansamehe yule dada,baada ya mwaka nilimsahau kabisa na nilipata mdada mwingine ambae tunaishi nae vizuri sana,sasa baaday ya miaka 4 hivi yule dada alipigika ile mbaya sasa hivi yupo tu hapa mjini anafanya vibarua vya kufagia ofisi za watu,nakuomba ujifunze kitu kwenye huu mkasa wangu
 
Ninajua aina ya maumivu inayopitia maana nilishawahi kukutana na Kisanga cha aina hiyo indirectly. Binafsi nilihama kabisa na kuepuka vitu ambavyo vilikuwa vinanipa kumbukumbu Zake. Nikawa mtu wa kanisani zaidi. nilipoona kumuepuka imeshindikana kupunguza maumivu nilihama nchini kwa muda. Hii ilifanya kazi kwani ni mwaka tu nikamsahau kimoja. So na wewe anza kufuta namba yake, futa meseji zote za kila aina mlizotumiana, vunja picha zake, nguo zake Choma moto, epuka kukutana au kuongea na watu watakaokukumbusha habari zake, ma mwisho kabisa kuwa busy na mambo ya kanisa au msikitini. kumbuka kumsahau mtu ni process hivyo kidogo kidogo itazoea.

Ushauri supa....!!
 
pole,ni jambo la kawaida katika mapenzi,ila ungeweka picha yako japo tukuone unavotia huruma
hahahahahahha jamaniiii unaweza uka imagine tu mtu anayetia huruma yukoje na wewe umuonee huruma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom