Mapenzi ya kutuma nauli ni sawa na kusafirisha mzigo

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,491
40,516
Mapenzi ni hisia kati ya mwanaume na mwanamke, na kinachowaunganisha ni hizo hisia walizojijengea wao katika mahusiano waliyonayo.

Kama mmoja atakuwa na hisia zaidi kuliko mwenzake, huyo lazima awe mtumwa katika hayo mahusiano; atateseka kiuchumi na kifikra katika kumfurahisha mwenzake ili asije kumkimbia.

Hayo tunasema, sio mahusiano yenye afya kwa binadamu; kwa sababu pale utakaposhindwa kutimiza mahitaji ya upande wa pili, lazima uhusiano utetereke.

Kwa mantiki hiyo, kama mahusiano yatakuwa na afya hakutakuwa na kuuziana hisia; kama kukulipia nauli ndio uje, kukununulia kitu fulani ndio unipe penzi, au mpaka nikuonge kitu fulani ndio ujenge hisia kuwa na mwenzako n.k tunasema huo ni ubatili katika mahusiano.

Naamini kama utakuwa na hisia na mwenzako, utagharamika kivyako ili muweze kuwa na mwenzako, bila kumpa mwenzio gharama akugharamikie.

Wanaume tushtuke, usisafirishe mzigo; kama ana mapenzi na wewe atakuja mwenyewe ata kwa kukopa.

Tofauti na hapo, tutakuwa tunauziana; ndio maana usafirishaji wa mizigo unakuwepo.
 
Back
Top Bottom