Mnavyo viandika dada zangu hamviishi mwanawake huwaga mnachanganyikiwa sana ukakuta ana mtu unampenda sana na upo kwenye mahusiano naye, ila akatokea mtu mwengine mwenye hela akakuonyesha upendo mixer vizawadi huwaga mnapagawa sana na mna msemo wenu maarufu "......Bora kulia kwenye V8 kuliko kucheka kwenye baiskeli........".
Dunia tunayoenda wanawake wanapenda sana hela,tatizo wengi wao hawajui MAHITAJI YAO YA MSINGI,ila siku hizi Iphone, Gucci,LV,matolea mapya ya mabegi nguo,mahotel makubwa ,vivutio vikubwa vya utalii nk kwao wameviingiza kwenye MAHITAJI YAO YA MSINGI. Wanaume wengi uwezo wa kuwapa mahitaji yenu ya msingi tunao,tatizo lenu mnaendekeza luxury.
Ktk wanawake 100 ni hawazidi wanawake watatu watakao kubali kukomaa na mtu wake anayempenda mwenye uwezo wa kawaida na kukimwacha mwenye hela. Halafu baadae mkishaingia kwenye ndoa na hao wenye fedha ndio mnakumbuka kuna unconditional love,unamkumbuka mwana uliye mwacha ambaye moyo wako unampenda mno unamshawishi awe kidumu.
Kuna mwanangu demu alianza nae tokea advance, demu yupo O-Level ,jamaa akaanza kazi demu ndio yupo chuo ila alikuwa ana msupport mwana mshahara wake ulikuwa around 1.5m.
Demu field alipata benki moja kubwa mjini. Demu amemaliza akapata intern kwenye hiyo bank, meneja watawi la hilo bank si kamwona kampindua mwana. Na jamaa mwaka ambao anatuambia sisi anaenda kuchumbia ndio mwaka huo huo (2017) demu anachumbiwa na huyo meneja. Mwana alisha mwambia kwamba huu nitakuoa, demu anaitikia siku ya siku anaziilona picha kwenye status ya demu,mwana kapagawa alikuwa na kitambi kikakata ghafla kwa stress.
Imeenda kama mwaka na miezi kazaa,demu anataka kurudi kwa mwana ,tukamchana aachane nae atamsababishia matatizo na demu mpaka kesho anataka mwana awe kidumu chake yaani anataka kucheza huku na huku.