Kabla ya Pesa Kulikuwa na Upendo♥️

Kabla ya Pesa Kulikuwa na Upendo♥️

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
17,625
Reaction score
41,918
Wakati mwingine najiuliza, mapenzi ya zamani yalikuwa na ladha tofauti au sisi ndiyo tumeharibu maana yake?

Angalia Suleiman na wimbo wake

Busu zake zinibusu...(Wimbo Ulio Bora 1:2)

Nimekupata yeye ambaye nafsi yangu yampenda (Wimbo Ulio Bora 3:4)

Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu (Wimbo Ulio Bora 6:3)

Ukisoma haya maneno unaona wazi kabisa, mapenzi yalikuwa ni hisia, si mashindano ya nani ana nini

Ila saivi ukileta maneno haya unakua kama unachekesha😅
Unaambiwa usilete maua leta sasampa lol 😆

Lakini leo kabla hata ya kuuliza mtu ana tabia gani, kwanza tunaangalia ana nini. Kabla ya kujua moyo wake ukoje, tunaangalia maisha yake yakoje

Mwanaume before huja m approach mwanamke anaangalia
Mbali na jigijigi nini kingine atapata kwake

Na kwa mwanamke ukitongozwa unaangalia kwanza utanufaika nini kwa huyo Mwanaume
Kuna msemo una sema bora kulia ukiwa kwenye dinga kuliko kulia huku unapuliza moto tena kuni mbichi😅😅 mafua tafrani

Lakini inaonekana zamani watu walipendana kwanza kisha mengine yakafata yenyewe

Hivi ni kweli 👇
Upendo una nguvu kama mauti... maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo.(Wimbo Ulio Bora 8:6-7)

Pesa ni muhimu, hilo halipingiki, lakini zinapochukua nafasi ya hisia, upendo unapoteza ile ladha yake ya kweli

Inawezekana mapenzi hayajaharibika… labda ni sisi tumeanza kuyapima kwa mizani isiyo sahihi

Usiku mwema guys
ShesRise_1 🤚
 
But Suleiman mwenyewe alikuwa na wake 700 na masuria 300, na iliwezekana yeye kuwa na wanawake wengi kiasi hicho kwa sababau ya utajiri alio kuwa nao.
Hivi wote aliwapenda kweli?
Vipi kuhusu nguvu za kiume maana 1000🙌🙌
 
Kila zama na kurasa zake, zamani hadi upewe papa ni ilikuwa kazi kuliko, yaani hadi uivue chupi ni kama umehitimu shahada ya kwanza. Leo aaah, mtu anakuja hana chupi, the very first day! Noma sana.
 
Zamani na sasa mambo ni yale yale tu hamna jipya, suleiman alikua na mali nyingi alikula kila aina ya utelezi, queen of sheba hakuliwa na mkimbiza boda, Daudi alimnyandua mke wa General wake kwa sababu alikua na cheo na mali. Tangu zamani pesa, cheo, muonekano, umaarafu vilikua privileged sema kizazi cha sasa kinazingatia sana.
 
Kumbe mambo ni yale yale duh
So now ni mwendelezo 🤔
 
Ni kweli kwamba upendo wa dhati ndio msingi mkuu wa uhusiano imara, ukitoa msamaha, uvumilivu, na furaha ya kweli ambayo fedha haiwezi kuinunua. Hata hivyo, pesa hutumika kama kichocheo kinachorahisisha maisha na kuondoa changamoto nyingi zinazoweza kuleta migogoro katika uhusiano.
 
Wakati mwingine najiuliza, mapenzi ya zamani yalikuwa na ladha tofauti au sisi ndiyo tumeharibu maana yake?

Angalia Suleiman na wimbo wake

Busu zake zinibusu...(Wimbo Ulio Bora 1:2)

Nimekupata yeye ambaye nafsi yangu yampenda (Wimbo Ulio Bora 3:4)

Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu (Wimbo Ulio Bora 6:3)

Ukisoma haya maneno unaona wazi kabisa, mapenzi yalikuwa ni hisia, si mashindano ya nani ana nini

Ila saivi ukileta maneno haya unakua kama unachekesha😅
Unaambiwa usilete maua leta sasampa lol 😆

Lakini leo kabla hata ya kuuliza mtu ana tabia gani, kwanza tunaangalia ana nini. Kabla ya kujua moyo wake ukoje, tunaangalia maisha yake yakoje

Mwanaume before huja m approach mwanamke anaangalia
Mbali na jigijigi nini kingine atapata kwake

Na kwa mwanamke ukitongozwa unaangalia kwanza utanufaika nini kwa huyo Mwanaume
Kuna msemo una sema bora kulia ukiwa kwenye dinga kuliko kulia huku unapuliza moto tena kuni mbichi😅😅 mafua tafrani

Lakini inaonekana zamani watu walipendana kwanza kisha mengine yakafata yenyewe

Hivi ni kweli 👇
Upendo una nguvu kama mauti... maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo.(Wimbo Ulio Bora 8:6-7)

Pesa ni muhimu, hilo halipingiki, lakini zinapochukua nafasi ya hisia, upendo unapoteza ile ladha yake ya kweli

Inawezekana mapenzi hayajaharibika… labda ni sisi tumeanza kuyapima kwa mizani isiyo sahihi

Usiku mwema guys
ShesRise_1 🤚
Inawezekana mapenzi hayajaharibika… labda ni sisi tumeanza kuyapima kwa mizani isiyo sahihi💕
 
Hivi wote aliwapenda kweli?
Hapana, nadhani aliyekuwa akipendwa zaidi anaweza kuwa labda Sulamitha ambaye alikuwa tofauti na wengine wote.
Vipi kuhusu nguvu za kiume maana 1000🙌🙌
Inasemekana jamaa alikuwa na nguvu za ajabu pia, lakini bado binafsi sikubaliani na suala la kuwaridhisha wanawake wote hao, Impossible!
 
Zamani pia ndoa zilikuwa zinapangwa na familia, watu wanatafutiwa mke au mume.
 
Ni kweli kwamba upendo wa dhati ndio msingi mkuu wa uhusiano imara, ukitoa msamaha, uvumilivu, na furaha ya kweli ambayo fedha haiwezi kuinunua.
Yes Yes
Hata hivyo, pesa hutumika kama kichocheo kinachorahisisha maisha na kuondoa changamoto nyingi zinazoweza kuleta migogoro katika uhusiano.
Ndio kusema mapenzi sio pesa ila ikikosekana yanapungua okay 👍
 
Back
Top Bottom