Hayo maneno aliyoyasema yakanishtua kidogo!
Pepo wa hasira akanitoka gafla.
Nikamsikia ananiambia, nimalizie nipumzike kwa amani
Niliwahi kujaribu kujiua kwa ajili yako(hapa nadhani
Tyta unakumbuka).
Sasa umefanya mwenyewe.
Kweli mwanzo inaweza kuwa mwisho.
Nilidhani leo ningepata nafasi tena yakufurahia mapenzi..
Lakini ndiyo inakuwa mwisho.
Second chance hamnaga duniani.
Alisema yote hayo huku anagugumia.
Afu akatulia ila bado alikuwa anahema kwa nguvu sana!
Nilipata wazo la kumpeleka hospital
nikambeba kuelekea kwenye gari, ile nataka kutoka walinzi waliniona bahati nzuri yule mmoja anatujua, ni hoteli tuliotumia sana wakati na date na vanie kipindi kile!
akaniambia vp bwana? kulikoni? nikamwambia ame faint kidogo ngoja nimkimbize hospitalini..
hawakuhoji sana kwani jamaa na wenyewe walishangaa kuona anavyohema kwa nguvu.
nikamweka ndani ya gari milango hakuilock ila funguo hazikuwepo pale kwenye switch
nikarudi ndani faster kuzichukua, nikabeba na kale kabegi kenye laptop na simu!
nilimkuta bado a