..Basi mimi mwenyewe ndiyo niliyaanzisha yale
mazungumzo kwa kumuuliza anampango gani?
Hiyo mimba yake atanithibitishiaje kuwa
ni ya kwangu?
Akaniambia hapo sasa ndiyo pa mimi na wewe kuongea.
Ananiuliza wewe msimamo wako ni upi?
nikamwambia wewe msimamo wangu si uliukataa tokea mwanzo?
Akaniambia kufanya kama nilivyokuwa nataka mimi ingekuwa ngumu sana..
nikamwambia sasa mimi kama hiyo mimba ni yangu na wewe
una uhakika nitamleaje mwanangu?
Nikamwambia nataka kumlea mwanangu mimi,
Na sio alelewe na baba mwingine.
Hapo akaanza kuchange akaniambia, naomba nikuambie
ukweli, akasimama akaanza kuvua blauzi aliokuwa amevaa,
Mama yangu!!!
moyo ulinipasuka kwa kile nilichokiona roho ikaniruka kwa hasira za ajabu.
kumbe tumboni alikuwa kajifunga kigodoro flani hivi
ili tumbo lake litune na nimwamini kuwa anamimba.
Akaniambia sijawahi kupata mimba na bado sijawa tayari
kuzaa na yule jamaa aliyenioa nahitaji mtoto na wewe.
Tarehe zangu ziko vizuri sana leo tuki do ni lazima ninase,
jana nilikusisitizia kukutana na wewe kwa nguvu zote nikijua huu ndiyo
wakati muafaka wa mimi kubeba mimba yako.
Nimekuwa makini sana kwa mume wangu asinipe mimba
coz he dont deserve it, ur the one to do it
Naomba uwe baba wa mtoto wangu wa kwanza! hao wengine ntazaa na mume wangu
Nilichannganyikiwa kabisa, miguu ikalegea
kumbe huyu alianza mapema kunidanganya kuwa anamimba yangu
akijua ndiyo mbinu rahisi sana kunipata.
Kiukweli nilichanganyikiwa na Vannie alilielewa hilo...