Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Unajua neno "ushahidi usiotia shaka"😅😅
Huo ushahidi usio tia shaka unahusika na kwenye examination office inayoenda kuamua!? Au unafikiri ni mahakama inaenda kuamua.
Kukamatwa tu na kikaratasi umesha disco huo ushahidi usio tia shaka huwa uko wapi!?
Huo ushahidi usio tia shaka ni kwa watu wenye pesa.
Wewe utafungwa hata kwa kusingiziwa kama huna malundo.
 
content kwa kuharibu reputation ya chuo kwa cheating?
hiyo DR mangungo au.?kichwani umejaza kamasi.
Kamasi zimeingiaje hapo..
Vijana wa siku hizi mnakosa Kabisa Uwezo wa kujenga hoja..
Umesoma nilichoandika?

Nilichozungumza ni Kama wao wakihojiwa na wakajibu hivyo kuna mtu Wa kuwashitaki?
Chuo kimeguswa wapi kwa kauli yao hiyo?
Je kuna mahali walikashfu chuo?

Wakati mwingine mjifunze kujenga hoja Sio mnaropoka tu kwa kuwa mna uwezo wa kuropoka..

Yule mwenzenu SUKUNUNU kumbe ni Kinyozi halafu anatukana Viongozi..

Unakuta hata wewe maskini Ya Mungu..Unakaa kwa shemeji yako..Na unalala Sebuleni au ni mwalimu wa Shule ya Kindergarten halFu unaniambia Nimejaza kamasi..?

Shame on you! Na ujifunze kujenga hoja bila matusi! matusi sio hoja
 
Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!


Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024

View attachment 2927199

Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Uchunguzi utafanyika na itathibitika sio kweli na wahusika wataomba radhi kulinda image ya chuo
 
Back
Top Bottom