Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!

ardhi.jpg

Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024


Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
 
Chuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Wala hakuna kesi hapo, na chuo hakitakiwi kuthibitisha jambo lolote, wahusika wameshakiri wenyewe, kinachofuatia hapo ni kuwafutia hayo matokeo yao.

Ujinga unaenda kuwaharibia future hao watoto, kama matokeo yakifutwa maana yake hata vyeti walivyopewa kwa kufaulu masomo havitakuwa valid tena, na kwasababu hiyo, hata kazini kama walipata kazi kwa qualification zao, wataenda kupoteza ajira zao/yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom